#COVID19 Neno UVIKO-19 wamelipata wapi?

May 25, 2021
32
95
Habari zenu wana Jamiiforums, poleni na majukumu ya kutwa nzima.

Bila kupoteza muda, ugonjwa wa Corona baada ya kuonekana kutokuwa kwenye mjumuisho wa magonjwa hatari yanayotambulika na shirika la afya dunia yaani WHO,

Hivyo WHO waliamua kuuingiza kwenye orodha ya magonjwa hatari na kuutafutia jina Covid-19.

Hivyo nikiwa karibu na vyombo vya habari Kama redio nikiwa nasikiliza taarifa huwa nasikia Covid-19 inaitwa Uviko 19 na viongozi wa kiserikali na pia watangazaji wa stations, na hili neno sijwahi kulisikia kabla Corona haijapamba moto,

Swali langu, je hili jina limetoka wapi au walikaa viongozi wakalitunga?

Au mimi tu ndio sijui lugha labda maana ya Covid kwa Kiswahili ni Uviko hivyo waliamua kuongeza kwa mbele namba 19,

Mnaoelewa mnifahamishe nami nielewe duku duku moyoni mwangu liishe la kujiuliza na jibu sipati.
 

luangalila

JF-Expert Member
Jan 12, 2014
3,776
2,000
Mtoa UZI unajichanganya changanya mnoo mara unazungumzia mtambo wa mume wa waziei mara unaulizia asili ya neno UVIkO19

Kimsingi neno UVIKO 19 tafsiri yaake ni Ugonjwa wa Virusi vya Korona 19. Kimsingi neno hili limetoholewa au kurudufishwa kutoka neno la lugha ya english
 

Anonymous Caller

Senior Member
Sep 8, 2016
197
250
Maneno mengi mapya,
ambayo zamani hukuwahi kuyasikia,

yamelazimika kutungwa ili kukidhi matakwa ya tafsiri kutoka lugha za kigen tena hasa yatokanayo na kukua kwa teknolojia.

Kwahyo kumbe maneno yanatengenezwa pia.
ni kazi ya TUKI bila shaka

Mubashara, barokoa, uviko, usaili, simu janja, king'amuzi, ujasiriamali, yapo mengi tu.

Hakuna neno lolote kati ya hayo ambalo lilikuwapo miaka ya 90's

Ukinunua baadhi ya visimu tochi vina translation ya kiswahili kwny user setting, vina changamoto kuvitumia.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom