Neno ‘ufisadi’ linawatisha wawekezaji - Ole Naiko | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Neno ‘ufisadi’ linawatisha wawekezaji - Ole Naiko

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Ngongo, Jan 29, 2009.

 1. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #1
  Jan 29, 2009
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  MKURUGENZI wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), Emmanuel ole Naiko, amesema neno ufisadi linawatisha wawekezaji, hivyo kuwataka wananchi kulitumia kwa umakini huku wakiweka uzalendo mbele.

  Alisema wakati taratibu za kupambana na rushwa zikiendelea, kipaumbele kielekezwe kwenye uchumi na maendeleo kwa ujumla ili kulikwamua taifa, kwani kiwango cha rushwa kilichopo si kama kilichopo katika nchi zilizoendelea.

  Naiko alisema hayo jana katika mahojiano maalumu na Tanzania Daima, yaliyofanyika katika ofisi za TIC, jijini Dar es Salaam.

  Mkurugenzi huyo alisema hakuna shaka kwamba rushwa na uwekezaji, haviendi pamoja lakini ni vema suala hili likachukuliwa kwa umakini na kutanguliza uzalendo kwa masilahi ya taifa.

  “Tunatakiwa tuwe na uzalendo pale penye sifa mbaya, tulichukulie kwa umakini ili tusiendelee kulijengea sifa mbaya taifa letu. Tuziache taratibu na sheria zetu zifanye kazi, ikiwemo kuwapeleka mahakamani watuhumiwa,” alisema.

  Alisema Tanzania haiongozi kwa rushwa lakini inaonekana hivyo kutokana na msimamo wa serikali kuweka wazi masuala ya rushwa.

  Akitolea mfano wa meya aliyeuza kiti cha useneta huko Illinois, nchini Marekani, Ole Naiko alisema hali hiyo inaashiria ni kwa jinsi gani kulivyo na rushwa katika nchi tajiri kuliko zile maskini.

  “Sisi tuna rushwa ndogo ndogo, hatuwezi kuongoza kwa rushwa, nchi tajiri ndizo zinazoongoza kwa rushwa. Kwanza tuna taasisi za kupambana na rushwa na tunayaweka haya masuala wazi, wenyewe kamwe hawawezi, kwani hawataki nchi zao zionekane mbaya,” alisisitiza.

  Kutokana na hali hiyo, Mkurugenzi aliwataka Watanzania kulifikiria taifa lao wakati likipambana na rushwa na kusisitiza kuwa wananchi wajadili jinsi ya kuliletea taifa maendeleo.

  Akizungumzia mafanikio ya mkutano wa Sullivan uliofanyika mwaka jana, alisema huandaliwa kwa lengo la kuwaunganisha Wamarekani na Waafrika katika kujadili mustakabali wa jinsi ya kuondokana na hali ya umaskini inayowakabili.

  Pamoja na hilo, alikiri kwamba mafanikio yameonekana hasa kwa wawekezaji wa Kimarekani, kwani mkutano huo umeifanya Marekani itoke nafasi ya nane hadi ya nne kwa uwekezaji nchini, ikifuatiwa na nchi za Uingereza, Afrika Kusini na Kenya.

  Kuhusu safari za Rais Jakaya Kikwete nchini Marekani, Naiko alisema zimewawezesha Wamarekani kuifahamu vema Tanzania, hivyo kuvutika kuwekeza zaidi.

  Alisema kwa sasa kituo chake kina mpango mahususi wa kutumia balozi zake katika kuitangaza Tanzania, ikiwa ni pamoja na kuweka balozi zake katika nchi zenye uwezo wa kuwekeza nchini.


  Source:Tanzania daima
   
 2. L

  Lorah JF-Expert Member

  #2
  Jan 29, 2009
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 1,193
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  ole naiko hivi uwekezaji ule wa MLimani city ulipewa kiasi gani maana nasikia ulikuwa mbogo kweli hata kwa wanasheria waliotaka kukukatisha kwa vipengele vyao visivyo na maaana! ngoja kwanza tumalize EPA kama na wamasai nao wameanza ufisadi tutajua...
   
 3. C

  CottonEyeJoe JF-Expert Member

  #3
  Jan 29, 2009
  Joined: Jan 8, 2008
  Messages: 330
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Ole Naiko ukimshika tuu, utaanza kusikia oooh mnatuonea sisi watu Mmasaai, Oooh mbona watu wa Monduli mnatuonea...blah blah blah...
   
 4. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #4
  Jan 29, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Huyu bwana anazungumza kama tuko mwaka 47 wakati upatikanaji wa habari ulikuwa mgumu. EPA, BOT, RADA nk ni rushwa ndogo!!!. Halafu unaposema sisi tuna rushwa ndogo yawezekana, lakini na mapato yetu ukilinganisha na hao wenye rushwa kubwa hapo pakoje.

  Taasisi ya kupambana na rushwa tunayo, anataka kutuambia eti nchi zilizoendeea zinaficha rushwa kwa kuwa taasisi zao zinaogopa nchi zao kuonekana zina rushwa. Wakati wao taasisi zao za rushwa ziko huru na wazi kabisa. Haya ni mawazo mfu.
   
Loading...