Neno ‘ufisadi’ linawatisha wawekezaji - Ole Naiko

CottonEyeJoe

JF-Expert Member
Jan 8, 2008
331
72
MKURUGENZI wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), Emmanuel ole Naiko, amesema neno ufisadi linawatisha wawekezaji, hivyo kuwataka wananchi kulitumia kwa umakini huku wakiweka uzalendo mbele.

Alisema wakati taratibu za kupambana na rushwa zikiendelea, kipaumbele kielekezwe kwenye uchumi na maendeleo kwa ujumla ili kulikwamua taifa, kwani kiwango cha rushwa kilichopo si kama kilichopo katika nchi zilizoendelea.

Naiko alisema hayo jana katika mahojiano maalumu na Tanzania Daima, yaliyofanyika katika ofisi za TIC, jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi huyo alisema hakuna shaka kwamba rushwa na uwekezaji, haviendi pamoja lakini ni vema suala hili likachukuliwa kwa umakini na kutanguliza uzalendo kwa masilahi ya taifa.

“Tunatakiwa tuwe na uzalendo pale penye sifa mbaya, tulichukulie kwa umakini ili tusiendelee kulijengea sifa mbaya taifa letu. Tuziache taratibu na sheria zetu zifanye kazi, ikiwemo kuwapeleka mahakamani watuhumiwa,” alisema.

Alisema Tanzania haiongozi kwa rushwa lakini inaonekana hivyo kutokana na msimamo wa serikali kuweka wazi masuala ya rushwa.

Akitolea mfano wa meya aliyeuza kiti cha useneta huko Illinois, nchini Marekani, Ole Naiko alisema hali hiyo inaashiria ni kwa jinsi gani kulivyo na rushwa katika nchi tajiri kuliko zile maskini.

“Sisi tuna rushwa ndogo ndogo, hatuwezi kuongoza kwa rushwa, nchi tajiri ndizo zinazoongoza kwa rushwa. Kwanza tuna taasisi za kupambana na rushwa na tunayaweka haya masuala wazi, wenyewe kamwe hawawezi, kwani hawataki nchi zao zionekane mbaya,” alisisitiza.

Kutokana na hali hiyo, Mkurugenzi aliwataka Watanzania kulifikiria taifa lao wakati likipambana na rushwa na kusisitiza kuwa wananchi wajadili jinsi ya kuliletea taifa maendeleo.

Akizungumzia mafanikio ya mkutano wa Sullivan uliofanyika mwaka jana, alisema huandaliwa kwa lengo la kuwaunganisha Wamarekani na Waafrika katika kujadili mustakabali wa jinsi ya kuondokana na hali ya umaskini inayowakabili.

Pamoja na hilo, alikiri kwamba mafanikio yameonekana hasa kwa wawekezaji wa Kimarekani, kwani mkutano huo umeifanya Marekani itoke nafasi ya nane hadi ya nne kwa uwekezaji nchini, ikifuatiwa na nchi za Uingereza, Afrika Kusini na Kenya.

Kuhusu safari za Rais Jakaya Kikwete nchini Marekani, Naiko alisema zimewawezesha Wamarekani kuifahamu vema Tanzania, hivyo kuvutika kuwekeza zaidi.

Alisema kwa sasa kituo chake kina mpango mahususi wa kutumia balozi zake katika kuitangaza Tanzania, ikiwa ni pamoja na kuweka balozi zake katika nchi zenye uwezo wa kuwekeza nchini.

Source: Tanzania Daima - Sauti ya Watu
 
Cottoneyejoe, Ole Naiko ashauriwe atafute ushauri wa Ndugu Edo Lowassa juu ya hili!!!
 
Huyu naye bora atangaze tu kujiunga na Sisi M. na akagombee ubunge maana ameshaanzisha propaganda zake hapa.
Uongo uongo uongo
 
Ole naiko hapa kachemka watanzania ni wazalendo ndio maana wanakemea ufisadi. Ukikaa na mwizi nyumbani na kumtetea mbele za wageni kuwa si mwizi ni mtu mzuri kwaajili ya kuwafurahisha wageni, siku akija waibia wageni utaaibika vibaya zaidi. Hivyo uzalendo wetu nikuhakikisha tunaendelea kukemea ufisadi mpaka uishe nasi tutatulia wala haihitaji kutukemea. watu wafanye kazi kwataratibu za kisheria na uungwana neno ufisadi litafutika.

Namtakia mafanikio katika kuitangaza nchi angalizo wasije kuchukua mali zetu bali kuwekeza kama anavyo sema. Pia kunamiradi mingine ni hatairi kwa taifa mfano mradi wa ''Jatropher tree'' kilimo cha mboni kwaajiri ya utengenezaji wa biofuel. Wataalam ikiwepo NEMC walishatoa riport kuwa mimea hii inaharibu udongo 'kiasi kwamba baada ya kilimo hiki ardhi haiwezi tumika kwa kilimo cha mazao mengine. Hatahivyo naambiwa uwekezaji huu unazidi kushamiri Tanzania. Waliopo huku tuhabalisheni zaidi
 
Back
Top Bottom