Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 29,189
- 39,954
Sisi binadamu huwa tunajisahau kushukuru pale tunapotendewa mambo makubwa na watu fulani, tukiamini ilikuwa ni haki yako kutendewa vile. Wapo wanaojengewa nyumba au kupewa maisha mazuri na watu fulani, lakini badala ya wale wanufaika kushukuru, wao wanaona ilikuwa ni lazima au haki yao kuyapata.
Mfano mgonjwa aliyekata tamaa ya kuishi na baadaye kufanyiwa upasuaji wa viungo vyake iwe; miguu, mikono, moyo, uzazi, tumbo, macho, mapafu n.k na baada ya matibabu akapona kabisa; na baada ya kupona akashindwa kutoa neno la shukrani kwa wauguzi au madaktari waliompatia huduma mpaka kuishi, atakuwa hajafanya uungwana kwa waliompatia huduma.
Neno 'appreciation' ni muhimu sana kwa mtu aliyekufanyia makubwa, na pia ni uungwana.
Wengine watasema ilikuwa ni wajibu wake kupata hizo huduma; Swali, je wangezembea kidogo, ingekuwaje?