Neno 'Samaki' lipo kwenye ngeli gani?

Dah! Haya mambo ndo yalisababisha nipate Kiswahili "C" haya!

Ya-wa tena?!

Ashukuriwe ambae alileta mambo ya kusoma vitabu na kwenda kutirika kwenye paper manake hadi namaliza Form IV, ilikuwa nikishasoma compression na kujibu maswali, kisha nikienda kwenye Fasihi, nikimaliza tu; huyoooo, nasepa zangu na mambo sijui ya tungo changamano sijui nyambulisha Kiima na Kiarifu, sijui mofimu (hivi ndo kinini hiki?!) nawaachia wenyewe coz' always hizo parts 2 zilikuwa zinanihakikishia C!!
Comprehension bila shaka...kama Compression ipo naomba kusahihishwa.
 
nimevuta picha nimesahau nikitambo sanaa ila ngoja niwekee hii akija mtu anaielewa Ngeli ya Yu atanisahisha
Mfano
Umoja.. Samaki yupo
wingi ..samaki wapo
Kwa huu mfano uliotoa unaweza kuonesha ulipo mzizi wa neno hilo ulilotumia kuweka hicho kiambishi ulichotumia ngeli ya YU - A WA?
Kwasababu ngeli huendana na kitenzi.
 
Mfano uliotoa hausadifu. Hata kama ni mbadala lakini muhusika amehitaji ngeli husika na sio ngeli mbadala.
Mkuu nimetaja jina la ngeli full... ila A- Wa ndo ngeli maarufu ila nilifundishwa kuwa kuna mda ngeli ya a inaweza isikubali...ko kama likitokea hilo ngeli yu huwa mbadala...

nazan nimeeleweka sasa
 
Chifu sikuwahi kuwa vizuri kwenye sarufi ya Kiswahili, na hii ilikuwa na mchango mkubwa sana wa kufanya hata "A" ya Kiswahili kuwa ni msamiati kwangu, manake maswali yake, hususani baada ya kufika Kidato cha III, ikawa sipotezi muda hata kuyaangalia tu!!
sarufi ni ngumu sanaaa🙌 ashukiliwe Ngoswe,joti,takadini, Peter,zita,kulwa,mama ntilie na wengine kwa kutuepusha na F za kiswahili
 
Kwa huu mfano uliotoa unaweza kuonesha ulipo mzizi wa neno hilo ulilotumia kuweka hicho kiambishi ulichotumia ngeli ya YU - A WA?
Kwasababu ngeli huendana na kitenzi.
hakuna mzizi na mfano sio official .. Ndiyo maan nimeomba anayeikumbuka vizuri anisaidie kama atakuwepo .... nitumie mfano yuaja kutetea ngeli ya Yu
 
Mkuu nimetaja jina la ngeli full... ila A- Wa ndo ngeli maarufu ila nilifundishwa kuwa kuna mda ngeli ya a inaweza isikubali...ko kama likitokea hilo ngeli yu huwa mbadala...

nazan nimeeleweka sasa
Chief kwenye ngeli hunidanganyi kitu, kila ngeli na matumizi yale kwenye sarufi, kuna ngeli ya:
A - wa
Yu - a - wa
Ki - vi
I - zi
U - zi na
U - i - zi
Katu usibadilishe matumizi ya ngeli ya Yu a wa kwa kuona tu yanafanana na awa kuna sehemu tu utakwama kwasababu ngeli hutumika kwenye vitenzi vinginevyo utakwama.
 
👏 shukran Mkuu nimekuelewa.....naomba ufafanuzi kwenye ngeli ya pili mfano wake
 
hakuna mzizi na mfano sio official .. Ndiyo maan nimeomba anayeikumbuka vizuri anisaidie kama atakuwepo .... nitumie mfano yuaja kutetea ngeli ya Yu
Chifu unakwama wapi, kuna ngeli huwa hazikubali kwa viumbe nje ya binadamu. Na ndio maana hata maiti ina ngeli yake japokuwa ni ya binadamu.
Mtoa mada ametaka ngeli ya Samaki. Jibu samaki ngeli yake ni A -WA.
 
Mkuu nimekusoma lakini lengo ni kujifunza jibu ni A-wa Sawaaa ila nilikumbuka ngeli ya Yu-A-Wa niliisoma pia... nikaomba mwenye uelewa Zaid anifungue hapo maana me ninachokielewa sina hakika kama niko sahihi...
 
Chief, ni hivi ngeli ya YU - A - WA matumizi yake huwa na mbadala yaani isipotumika YU kwenye umoja basi itatumika A, lakini kwenye wingi ndio itatumika WA.
Mfano:
Mtoto yualishwa
Mwalimu yuafundisha
Mzee yuazeeka
Hii ngeli ya YU - A - WA ipo kilahaja zaidi na sio kiswahili sanifu kwani si katika hali ya kawaida kumkuta mtu anatumia neno yualishwa, yualia, yuafundisha au yuanakula badala ya kutumia analishwa, analia, anafundisha, anakula.
Kwa Tanzania baadhi ya maeneo ya mwambao pamoja na maeneo ya Visiwa vya Zanzibar, sana sana kisiwani Pemba ndio inatumika lahaja hiyo (lafudhi).
 
Mtoa mada sana, leo umesababisha nimekumbuka hadi ngeli nyingi sana, ikiwemo
LI - YA
PA-MU-KU
U - YA
U - ZI
I - ZI
 
Chief, ni hivi ngeli ya YU - A - WA matumizi yake huwa na mbadala yaani isipotumika YU kwenye umoja basi itatumika A, lakini kwenye wingi ndio itatumika WA.
Mfano:
Mtoto yualishwa
Mwalimu yuafundisha
Mzee yuazeeka
Hii ngeli ya YU - A - WA ipo kilahaja zaidi na sio kiswahili sanifu kwani si katika hali ya kawaida kumkuta mtu anatumia neno yualishwa, yualia, yuafundisha au yuanakula badala ya kutumia analishwa, analia, anafundisha, anakula.
Kwa Tanzania baadhi ya maeneo ya mwambao pamoja na maeneo ya Visiwa vya Zanzibar, sana sana kisiwani Pemba ndio inatumika lahaja hiyo (lafudhi).
nimekupata mkuu🙏🙏🙏🙏
 
Mkuu nikumbishe hiyo ya PA-MU-KU
Ngeli ya PA - MU - KU.
PA - Hutumika kuonesha mahali maalumu(Panapodhihirika), mfano:
padogo, palipowazi au pamezibwa.
Ngeli ya KU - Hutumika kuonesha mahali fulani kwa jumla au eneo fulani (Pasipodhihirika au mbali), mfano:
Kule kunafaa
Ngeli ya MU - hutumika kuonesha mahali ndani ya kitu kingine kama vile ndani ya nyumba, shimo, mfano:
Ndani ya shimo mumejaa siafu
Ngeli za mahali hubaki vivyo hivyo katika umoja na wingi.
 
Back
Top Bottom