Dr Lizzy
Platinum Member
- May 25, 2009
- 30,778
- 59,133
Ladies, kwako mume/mpenzi wako anapokukosea una-prefer aombe samahani ya aina gani?
Ipi unadhani ni ya dhati?
Anyamaze kimya ila ajaribu kuku-WIN kwa kukununulia zawadi na kukufanyia vitu vizuri ambavyo alikuwa hafanyi mwanzo mf. Kukutoa out, kukusaidia vikazi vidogo vidogo nyumbani, kujali hisia zako na mahitaji yako binafsi, kuwahi kurudi nyumbani, kukushirikisha mambo yake n.k
Au kukuambia SAMAHANI, NILIKUKOSEA, HAITOTOKEA TENA halafu basi?
Wakaka/wababa huwa mnamaanisha nini pale mnapogoma kusema samahani na badala yake kuanza kumwaga mazawadi na pesa kwa wenzi wenu?