Neno nyumba ndogo linatumika visivyo, Serikali iingilie kati

Trainee

JF-Expert Member
Sep 22, 2018
2,205
2,804
Habari wadau...

Neno hilo limekuwa likitumika tangia zamani hasa kwa wale wenye mke zaidi ya mmoja. Mke wa kwanza kuolewa na mwanaume fulani amekuwa akitambulika kama mke mkubwa au NYUMBA KUBWA kisha atakayefuata kuolewa na mwannaume huyohuyo basi amekuwa akitambulika kama mke mdogo au NYUMBA NDOGO. Kadhalika wakiwa wake watatu na zaidi imekuwa ni kawaida kusikia hadi NYUMBA YA KATI

Wanawake husika walioolewa na mtu mmoja wamekuwa wakitambuana kihivyo na mume naye hulazimika kuwatendea au kuwatimizia haki zao kwa usawa kwa kadri ya atakavyojaliwa

Jambo la ajabu hivi karibuni kumeingia utumiaji mbaya wa neno nyumba ndogo kwani watu wamehamishia neno hilo kwa mahawara na michepuko. Hali hiyo imepelekea hata wengine wasio na mila hiyo (ya kuoa wake zaidi ya mmoja) kuutumia mwanya huo kudhihaki, kukashifu na kuponda wanawake (waliopewa jina la nyumba ndogo) ambao kisheria wana haki zote za ndoa kama ilivyo wengine

Wito wangu kwa serikali iingilie kati kwa kupiga marufuku matumizi holela ya maneno hayo au kama neno hilo lina maana zaidi ya moja ikiwemo hiyo iliyotawala sasahivi basi kuangaliwe namna bora ya kuwarudishia heshima wake za watu walioolewa mitala

Nawasilisha
 
Back
Top Bottom