NENO MOJA TU LILIVYOBADILI MAISHA YA MTU...HALA HALA MANENO HUJENGA AMA HUBOMOA


Mr Amour

Mr Amour

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2016
Messages
223
Likes
107
Points
60
Age
21
Mr Amour

Mr Amour

JF-Expert Member
Joined Oct 4, 2016
223 107 60
.
SIKU moja, Thomas Alva alirudi nyumbani na kipande cha karatasi mkononi. Akamkabidhi mama yake huku akimwambia: "Mwalimu amenipa barua hii, na kunisisitiza nimkabidhi mama yangu."
Macho ya mama yake yalitota machozi kadri alivyokuwa akiisoma barua. Baada ya kujifuta machozi, alitabasamu huku akimpapasa kichwa mwanaye. Kisha akamsomea kwa sauti barua ile: "Kwa mzazi wa Thomas, mtoto wako ana akili nyingi mno (genius). Bahati mbaya, shule yetu ina vifaa dhaifu na walimu wenye uwezo mdogo kumfundishia mwanao. Tafadhali mfundishie wewe mwenyewe tu nyumbani."
Pamoja na kuondolewa shuleni, Thomas alifarijika kwamba, yeye ni mtoto mwenye akili nyingi - atayekuja kufanya makubwa duniani. Miaka mingi baada ya mama yake kufariki, Thomas aliondokea kuwa mfanyabiashara mkubwa na mwenye akili nyingi. Siku moja, Thomas aliperuzi makablasha ya zamani ya marehemu mama yake, akaiona ile barua aliyokabidhiwa na mwalimu. Aliifungua na kukuta ujumbe huu: [Kwa mzazi wa Thomas, mtoto wako ni mgonjwa wa akili. Hatumruhusu tena kuendelea na masomo katika shule yetu. Unaweza tu kumfundisha mwenyewe nyumbani.]
Machozi yalimbubujika Thomas baada ya kugundua kumbe, mama yake hakumsomea ukweli wa kilichoandikwa kwenye barua miaka ile. Kwa hisia kali, Thomas aliandika kwenye shajara (diary) yake maneno haya: [Thomas Alva alikuwa ni mtoto mgonjwa wa akili ambaye, mama yake alimbadili na kuwa genius kwa kauli moja tu]
FUNZO: Neno moja, kauli moja, barua moja au uongo mmoja, unaweza kumbadili mtu mara moja. Kila mmoja, atumie neno la faraja na matumaini kumbadili mtu aliyeshindikana au kukataliwa.JIFUNZE.
 
S

shiite

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2016
Messages
267
Likes
230
Points
60
Age
29
S

shiite

JF-Expert Member
Joined Jul 31, 2016
267 230 60
ni kweli kiongoz maneno yanaishi!! thanks
 
black sniper

black sniper

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2013
Messages
9,959
Likes
7,133
Points
280
black sniper

black sniper

JF-Expert Member
Joined Dec 10, 2013
9,959 7,133 280
Mama ni mama
Yaani nimetafakari sana haya maneno na matukio mengi yanayotokea kwa binadamu wengine.

Hekma aliyoitumia huyo mama kuna watu wengine wamesoma na kujitapa lakini maneno yao ya hovyo kabisa.

Kweli ni la kuzingatia sana


Sent from my SM using Tapatalk
 
Mr Amour

Mr Amour

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2016
Messages
223
Likes
107
Points
60
Age
21
Mr Amour

Mr Amour

JF-Expert Member
Joined Oct 4, 2016
223 107 60
Mama ni mama
Yaani nimetafakari sana haya maneno na matukio mengi yanayotokea kwa binadamu wengine.

Hekma aliyoitumia huyo mama kuna watu wengine wamesoma na kujitapa lakini maneno yao ya hovyo kabisa.

Kweli ni la kuzingatia sana


Sent from my SM using Tapatalk
nani kama mama?
 
caridas

caridas

Senior Member
Joined
Sep 30, 2018
Messages
181
Likes
204
Points
60
caridas

caridas

Senior Member
Joined Sep 30, 2018
181 204 60
Nimetoka na kitu hakika, Mama akiwa smart familia inasimama. thanks kwa ku share!
 
Smart911

Smart911

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2014
Messages
22,259
Likes
20,681
Points
280
Smart911

Smart911

JF-Expert Member
Joined Jan 3, 2014
22,259 20,681 280
Inapendeza sana...


Cc: mahondaw
 

Forum statistics

Threads 1,250,886
Members 481,523
Posts 29,749,609