Neno moja kwa mzazi wa huyu Mtoto.

Sefu jafary

JF-Expert Member
Jun 5, 2016
382
258
Wapo watoto ambao hupenda kuiga kila kitu ambacho mzazi anakifanya.Siku izi wapo watoto wana kunywa pombe na wengine kuvuta sigara kwa kuwaiga wazazi.
Mfano mzuri yupo Mtoto wa jirani huwa akimuona Baba yake anavuta sigara huwa analia sana akitaka apewe avute.

Hii imepelekea mzazi wake kushindwa kuzuia kilio cha mtoto wake na kuamua kumruhusu avute japokuwa umri wake ni mdogo.
Kwa wale wazazi ambao wanatumia pombe au sigara ni vema wakawa na utaratibu maalum wanapo kuwa kwenye starehe zao wasiende na watoto pia kama wana tabia ya kufanyia starehe zao nyumbani inabidi wawe waangalifu sana na watoto (hasa wadogo).

Wazazi ni mfano wa kuigwa lakini sio kila jambo analofanya mzazi linapaswa kuigwa lakini kwa watoto wadogo hawajui hili, wanachojua ni kwamba kila anachofanya mzazi ni sahihi.

Watoto ni taifa la kesho kutwa, jinsi tunavyo waandaa ndo taswira ya kizazi kijacho/Taifa lijalo.
So, bila kujua tunaweza kuandaa taifa la watoto walevi na wavuta sigara badala ya kuandaa taifa bora.
"Thank you for your attention """

ea41ffc8e396d23dd6a25280dacf7b8d.jpg
 
Back
Top Bottom