Kyachakiche
JF-Expert Member
- Feb 16, 2009
- 983
- 207
Neno "Mchakato" limekuwa maarufu sana miongoni mwa wanasiasa hususani wa CCM na Serikali yake. Kila mara watu wanapotaka kujua ama kuelezwa juu ya ahadi ama utekelezwaji wa miradi mbalimbali, mara utasikia jitihada zinaendelea kufanyika, au mchakato unaendelea, upembufu yakinifu unaendelea... na mengine kama hayo. Je kwa wananchi wa kawaida wanaelewa haya au ni ulaghai tu wa viongozi katika kuomba kura? Na nini hasa maana ya mchakato na kwanini limeshika sana kasi kwenye awamu ya nne?