Neno mapenzi lina maana gani?

Makunzo

Member
Aug 24, 2009
10
0
Nauliza, neno mapenzi lina maana ya tendo la mapenzi kati ya wapendanao au mapendo kati ya wapendanao? kama neno hilo lina maana ya mapenzi ya kimwili kwa nini mtu amwite mama yake mama mpenzi?
 
Makunzo swali lako nilishawahi kulijibu humu humu jukwaani, lakini nafanya "COPY and PASTE" kwa manufaa ya jamii. Maana ya neno hilo nimeegemea zaidi katika dini ya Kikristo kwa msaada mkubwa wa BIBLIA. Hebu twende pamoja sasa: NI NINI MAANA HASA YA NENO UPENDO Hivi neno UPENDO linamaanisha nini hasa? Maana yake ni nini hasa ukizingatia kuwa imesemwa/inasemwa/itasemwa kwamba upendo ndio uhitaji mkubwa zaidi wa Wanadamu. Tangu wanapozaliwa hadi kufa, watu hutamani kupendwa, wanaishi kwa furaha wanapopendwa na hata wanadhoofika na kufa wasipopendwa. Bila shaka, watu huongea sana kuhusu Upendo. Hata hivyo, jambo la kushangaza ni kuwa sio rahisi kuelezea maana ya Upendo. Baadhi ya wachambuzi wamefikia kukata kauli kuwa Upendo unaweza kuonyeshwa tu kupitia matendo. Kulingana na Biblia, kuna aina nne za upendo. Kwanza, ni shauku changamfu, ya kibinafsi kumwelekea mtu fulani; aina ya upendo ulioko kati ya marafiki wa karibu (Yoh 11:3). Pili, Upendo ulioko kati ya washiriki wa kifamilia (Rum 12:10). Tatu, Upendo wa kimahaba ambao mtu anaweza kuwa nao kumwelekea mtu mwingine wa jinsi tofauti (Mith 5:15-20). Mwishowe ni Upendo mkubwa zaidi kwani huongozwa na kanuni; kanuni zinazofaa-zinazopatikana katika neno la MUNGU (Zab 119:105). Upendo huo, ni kufikiri kusiko na ubinafsi wa kuwafanyi wengine lililosawa na jema kutokana na maoni ya MUNGU, iwe mwenye kupokea anastahili au la! Neno UPENDO linatokana na maneno manne (ndio aina nne za upendo) ya Kigiriki cha mwanzo, ambayo ni: • PHI•LE´O • STOR•GE´ • E´ROS • A•GA´PE PHILEO: Kitenzi kinachomaanisha kuwa na shauku, kuthamini au kupenda (kama mtu anavyompenda rafiki wa karibu au ndugu). Hutumika mara nyingi katika Agano Jipya baada ya neno Agape. STORGE: Upendo ulio kati ya watu wa familia moja. Huu ndio upendo amboa Paulo mtume alisema una/utakuwa haba katika siku za mwisho (2Tim 3:3). EROS: Upendo wa kimahaba kati ya watu wa jinsi tofauti. Upendo huu hautajwi katika Agano Jipya bali katika Agano la Kale (Mith 5:15-20). AGAPE: Upendo unaoongozwa na kanuni na unatia ndani mambo mengi; unahusisha fikira na una kusudi fulani na hauna ubinafsi. Upendo huu sio hisia tunayokuwa nayo bila kufikiri. Mara nyingi huhusisha uhusiano wa karibu wenye upendo. Kwa ujumla (mara nyingi) aina zote zinastahili na zinabidi ziende pamoja. Mfano: Ni kweli upendo wa kimahaba (eros) una sehamu yenye maana sana katika ndoa zenye mafanikio; shauku yenye kina kirefu na urafiki (philia) huongezeka kati ya wanandani na huimarishwa na upendo (agape) ambao hustawishwa kumwelekea Mungu, Kristo na Jirani Yetu (Zetu). Kwahiyo, neno hilo (Upendo) ni neno ambalo lime/lina/litatumiwa sana na wanadamu. Ni neno ambalo limeandikiwa vitabu, likatungiwa nyimbo riwaya na mashairi mengi mno. Pamoja na hayo mara/ nyakati nyingine halifafanuliwi ifaavyo/ipasavyo. Ni neno ambalo lime/lina/litatumiwa sana hivi kwamba inaonekana (limeanza) kupoteza maana yake halisi (mfano ushoga, usagaji na ukahaba). NB: Je wajua kuwa Upendo ndio sifa kuu zaidi ya Mwenyezi Mungu?
 
Kweli wewe ni Bazazi hasa.
 
Mmmuuh Nimejisikia furaha sana kwa majibu mzuri mheshimiwa Bazazi. Meseji yako nzuri sana sana hasa hasa uliponipeleka kiroho. Si wote wanajua hasa Upendo wa Mungu au mapenzi ya Mungu kwa wanadamu. Wengi hawana AGAPE: Upendo unaoongozwa na kanuni na unatia ndani mambo mengi; unahusisha fikira na una kusudi fulani na hauna ubinafsi. Mapenzi halisi yalifanywa na Mungu alipotupa Mwanawe Yesu, yaani upendo wa kujitoa hasa. Wana mapenzi ya ngonoooooo tu basi. Sidhani kama watu wote vijana kwa wazee wanajua kwamba Mungu alitupenda kwa mapenzi Makubwa mno hata akatupa mwanawe yesu ili tuokolewe. well nimefurahi........ Bazazi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom