Neno La Usiku: CCM Na Sifa Ya Mchawi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Neno La Usiku: CCM Na Sifa Ya Mchawi!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by maggid, Aug 29, 2012.

 1. m

  maggid Verified User

  #1
  Aug 29, 2012
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Ndugu zangu,


  Usiku wa saa sita umeingia tena hapa Iringa. Kabla sijaondoka kwenye meza ya kibarua changu nina neno fupi la usiku.  Naam, inasemwa, kuwa mchawi mchukie, lakini, sifa yake mpe, anajua kuroga!


  Majuzi hapa nilipokuwa kwenye shughuli za kijamii kijijini Mahango, Madibira, kuna kitu kilichonifanya nishangae, lakini, baada ya tafakuri nikauona ubunifu kwa aliyekitenda.


  Nikiri, kuwa huko nyuma nimefanya vikao kadhaa na Kamati ya Shule ya Mahango chini ya Uenyekiti wa Bw. Victor Kadama ( Pichani). Sikupata kujua kuwa Victor Kadama, mbali ya kuwa Mwenyekiti wa kamati ya Shule, pia ni Katibu Mwenezi wa CCM, Kata ya Madibira. Ndio, Victor Kadama ndiye Nape Nnauye wa Madibira.


  Maana, kwenye vikao vyetu hakuwahi hata siku moja kuvaa nguo za rangi ya chama chake wala kofia. Lakini, majuzi hapa tulipokuwa na mkusanyiko mkubwa wa wanakijiji kuwapokea wageni kutoka Norwich, Uingereza waliokuja kuzindua mradi wa ujenzi wa Maktaba ya Kijamii kijijini hapo, basi, kwa siku mbili mfululizo, nilimwona Bw. Victor Kadama akiwa ametinga kofia ya chama chake, CCM.


  Bw. Kadama kwa siku zote mbili hakuongea hata neno moja kuhusu chama chake, lakini, kofia yake ilikuwa inaongea. Kulikuwa na uwepo wa CCM kupitia kwa kofia ya Kadama. Na hata wageni waipopangiwa ziara ya miguu kuona mazingira ya kijiji, Victor Kadama na kofia yake haraka alichukua jukumu la kuongoza msafara. Aliendelea kufanya ' kazi ya uenezi' wa Chama chake.


  Kwa vyama vingine vya siasa kuna ya kujifunza kutoka kwa CCM. Pamoja na dhambi zao zote, CCM bado wana oganaizesheni inayoeleweka na yenye kufikia hadi ngazi za vitongoji. Ni mtaji wao mkubwa kisiasa. Tofauti na vyama vingine, makada wa CCM wanajipenyeza kila mahali, iwe kwenye kamati za shule au za kuchimba visima. Ndio, hata, uwe na harusi ya mwanao, bado kuna makada wa CCM watakaojipenyeza kwenye Kamati za harusi.
  Naam, mchawi mchukie, lakini sifa yake mpe, anajua kuroga, hakyamungu!


  Maggid,
  Iringa.
  0788 111 765
  Mjengwa Blog::Habari,Picha,Matangazo
   
 2. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #2
  Aug 29, 2012
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 8,252
  Likes Received: 4,274
  Trophy Points: 280
  Mkuu hapo hakuna tatizo kwani hiyo ni kazi ya ukatibu uenezi.

  Sasa hapo kwenye hiyo ni mahali pake kwahio sidhani kama huo ni uchawi isipokuwa CCM inafahamu namna ya kufanya uhamasishaji ingawa umewapa jina zito la kwamba ni wachawi.

  Chama mbadala cha upinzani cha CHADEMA nacho kinafanya kazi yake ya uhamasishaji na si unaona M4C inavyopita kila kata? na sasa watu wa CCM wamechangikiwa wanaagiza polisi wakamate watu.

  Ndugu Maggid, siasa inataka pia watu muwe tayari kufanya majibizano yenye kujenga yaani "constructive" na sio kubomoa au "destructive".

  Wananchi au "electorate" wana jukumu la kuangalia wapi kuna ujazo wa sera zenye kuaminika na kutoa maamuzi wapi wanapendelea kukabidhi ridhaa ya kuunda serikali.

  Kwa jinsi hali inavyoonekana kwa sasa kwamba wananchi wameamka (shughuli za MC4 na angalia picha za Morogoro), mambo ya uchaguzi wa 2015 kuna utata mkubwa kwa chama unachoendelea kukiamini cha CCM.

  Maana kama si kuwa na serikali ya mseto basi Bunge la Tanzania huenda likawa na zaidi ya nusu ya wabunge kutoka upinzani na hii ndio kazi ya Nape kupiga kelele kila siku kwenye vyombo vya habari kuhakikisha wanawavuruga wananchi kwa kauli mbalimbali.
   
 3. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #3
  Aug 29, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  kikubwa ni kujipanga na inawezekana hata kofia zitafute wapewe wananchi tunaweza hata sisi kufikisha ujumbe kwa njia hii wanayotumia ccm
   
Loading...