NENO LA SHUKRANI WA WANA Jfs WOTE - (MSIBA WA MAMA YANGU MZAZI)

tete'a'tete

JF-Expert Member
Feb 10, 2010
472
62
Wakuu wote!

Natumai muu wazima na mungu aendelee kuwatangulia kwa kila mlifanyalo.

Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa woote mliojumuika nami tokea nimewapa taarifa ya msiba wa mama mkaungana nami kunifariji kuniombea mungu akaniwezesha nikatapa nguvu ya kuweza kumzika kwa heshima mama yangu mzazi huko Marangu Moshi tarehe 29/03/2010 kwa kweli si rahisi kwa binadamu yeyote kupata ujasiri lakini kwa sala zenu niliweza kupata ujasiri mkubwa kwani siku ya maziko niliweza kwenda KCMC kumvalisha mama na kumhudumia mpaka alipopumzishwa katika nyumba yake ya milele.

Wakuu nimerudi jumatano kwa bahati mbaya nilikuta forum yetu imesitishwa kwa muda kwa hivyo sikuweza kutoa shukrani zangu.

Nawashukuru woote mliowasiliana nami kwa njia simu muda wote kwa kunifariji na wale woote mlionitumia message kupitia jamii forum. Mungu azidi kuwabariki.

Napenda kuwajulisha kuwa baada ya kifo cha mama nimeamini kweli tumezaliwa na ipo siku tutakufa kwani sisi binadamu ni kama mshumaa ambao unawaka na kumulika sana na mwisho wake huzimika bila hata taarifa.

Nawaombeni wanajamii wote tuendelee na moyo huu mliuonyesha katika kipindi hiki kigumu na tuendelee kusaidiana si wakati wa furaha tuu bali hata kwenye matatizo katika maisha.

Asanteni! Asanteni! Asanteni! na Mungu awabariki katika maisha yenu.

Nawapenda woteee....

RIP my beloved Mother!

Tete'a'tete
 
Ooooh!
What a saddening message!
Anyway, what we can say is that, come back to work, coz God has taken care of all your pitty moments!
Courage up dear, and we are all around you!...Siku hiyo nilipenda nifike huko, lakin nlpata safari ya ghafla!

U r most welcome dear...Pamoja!
 
Vizuri that you have the coueage and strength back, God will always be there for you wala usijali.
 
May our almighty God keeps on showering his strength to you! Pole sana dada.
 
mungu aendelee kukupa nguvu na ujasiri mpendwa ..duniani sote tunapita makao yetu ni mbiguni
Amen
 
karibu sana mama.....!
mungu akupe nguvu.
MAISHA NA YAENDELEE
 
pole sana mpendwa..karibu tena na Mungu azidi kukupa nguvu ya kuendelea na maisha yaliyopo mbele yako
 
Pole sana mkuu ni msiba mkubwa sana kuondokewa na mzazi. Kwa kuwa jukwaa halikuwapo wengine hatukuwa na habari.
Mungu akuongezee nguvu ya kushinda huzuni!
 
Pole sana kwa kuondokewa na kipenzi Mama yetu. Tuamini kuwa iko siku tutakutana naye mahala ambapo machozi yote yatafutwa. Mchakato wa maisha ndivyo ulivyo. Kuzaliwa furaha, kuolewa furaha na mwisho kufa ni majonzi. Mkuu mshukuru Mungu kwa zawadi ya maisha aliyomjalia Mama yetu. Kikubwa sasa ni kujipanga upya na kujaribu kuziba pengo ingawa halizibiki kamwe. Mungu akupe nguvu ya kuvumilia msiba huo. Karibu tena jamvini na wana JF wako daima nawe.
 
pole dear, mungu akupe faraja zaidi na zaidi, uendelee na shuguli zako, na tuendelee kumuombea mpendwa wetu,
 
Back
Top Bottom