Neno la shukrani kutoka kwa DC Ally Hapi

Egnecious

JF-Expert Member
Jul 8, 2015
875
960
NENO LA SHUKRANI KUTOKA KWA DC HAPI

Dear comrades,

Tarehe kama ya leo (18 April) mwaka 2016, Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Joseph Magufuli aliniteua kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni.

Leo hii nikiwa natimiza mwaka mmoja wa utumishi wangu; nimeona niandike machache kama sehemu ya shukrani zangu.

Kwanza, napenda kumshukuru sana Mwenyeezi Mungu mtukufu kwa kunijaalia afya njema na kunifikisha hapa nilipofika leo hii.

Pili, namshukuru kwa dhati Mh. Rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli kwa imani yake kubwa kwangu kiasi cha kunipa dhamana ya kuwaongoza wananchi wa Kinondoni.

Nitaendelea kufanya kazi kwa bidii na maarifa yote ili kumsaidia Rais wetu kufikia malengo ya serikali yake katika eneo nililopewa kuongoza.

Aidha, shukrani ziwaendee Waziri wetu wa TAMISEMI Mh. George Simbachawene(Mb), Naibu Waziri Mh. Suleiman Jafo(Mb), Katibu Mkuu wa TAMISEMI Alhaji Injinia Mussa Iyombe na Mkuu wangu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda kwa kunipa aelekezo na miongozo mbalimbali ya kazi iliyoniwezesha kuchota uzoefu na kutekeleza majukumu yangu kwa ufanisi.

Tatu, napenda kuishukuru familia yangu, ndugu, jamaa, viongozi wenzangu, watumishi wote wa manispaa ya Kinondoni, wanahabari, marafiki, wananchi wote wa Kinondoni na wote ambao kwa namna moja au nyingine wamenisaidia katika kutimiza majukumu yangu vizuri.

Mwisho, lakini si kwa umuhimu, napenda kukishukuru sana Chama changu, Chama Cha Mapinduzi CCM. Chama ambacho kimenilea katika misingi imara, maadili mema na kunifundisha uongozi wakati nikiwa mwanachama, kiongozi na mtendaji katika nyakati mbalimbali.

Mungu ibariki Tanzania,
Mungu mbariki Rais wetu.
Ahsanteni sana.

Ally Salum Hapi
DC Kinondoni"

[HASHTAG]#KinondoniYetuFahariYetu[/HASHTAG]
IMG_20170418_200329_515.jpg
 
hongera sana ukipewa kidogo ukashukuru mungu anakuzidishia ,pia hongera kwa kutambua kuwa ofisini unafanya kazi na wenzako na ni msaada kwako kutimiza majukumu yako safii sana kijana unatuwakilisha vyema vijana wenzako.
 
Back
Top Bottom