Yericko Nyerere
JF-Expert Member
- Dec 22, 2010
- 16,987
- 20,271
SHUKRANI
Jana ilikuwa siku ngumu sana kwangu baada ya kuhukumiwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu chini ya Hakimu Kasian Matembele kwenda jela miaka mitatu au kulipa faini ya pesa taslimu shilingi milioni tano katika kesi No 188/2017 kosa la kuchapisha maneno ya uchochezi mitandaoni, Lakini Watanzania mligeuza ndani ya dakika 60 tu ikawa furaha na nderemo baada ya kuchangia pesa na kulipa faini hiyo.
Nawashukuru sana Watanzania kwa Ujumla wenu kwa mwitikio mkubwa mliouonyesha, Nakishukuru Chama changu Chadema Tanzania kwakusimama nami kwa miaka sita yote niliyokuwa na kesi hii na kwa uzito mkubwa nitoe shukrani za kipekee kwa Mwenyekiti wa Chama Mh Freeman Mbowe na Katibu Mkuu wa Chama Mh John Mnyika hawa wamekuwa zaidi ya viongozi/walezi/wazazi kwangu.
Nalishukuru jopo la Mawakili lililoonhozwa na Wakili msomi Peter Kibatala na Hekima Mwasipu kwa mahiri mkubwa na kwa uvumilivu mkubwa sana kwa miaka yote sita waliyonisimamia tangu niliposoma fikishwa mahakamani November 2015.
Kipekee niwashukuru Makamanda John Pambalu Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Taifa Bavicha Taifa Tanzania na Kamanda Malisa GJ kwa namna ya miujiza waliyoifanya jana ndani ya dakika sisizopungua 60 pesa ya kulipia fani 5M ikapatikana na zaidi.
Binafsi nimebaki nimeduwaa tu hadi leo, maana awali nilikuwa na maumivu ya hukumu japo nilishajiandaa kisaikolojia kwenda Segerea, lakini ndani ya saa moja nikaelemewa na furaha isiyokifani. Watanzania mmeniheshimisha sana, Nina deni kubwa sana juu ya imani mliyonikopesha. Imani hii nitailinda daima.
Pia soma: Kisutu: Yericko Nyerere ahukumiwa jela miaka mitatu au faini ya Mil 5 kwa uchochezi, alipa faini na kuachiwa huru