Neno la shukrani alilotoa kijana aliyepiga picha expansion joints za hostel

Kasome kwanza , kijana ukijitazama kwenye kioo mwili wako una sisimuka unadhani umekomaa, hapana, mbegu za kizazi chako bado, rudi shule kwanza. Lakini nasikitika kuona umejichafu na kujilaani. Watu wabaya wanakuona, shetani naye atakuandama ungali bado mtoto. Acha siasa nenda shule. Kinga yako toka sasa niya kubahatisha bahatisha. Acha siasa sisi wazazi wako tusikupoteze mapema. Siasa ni kuchinjana , kufa au kupona.
Je angekuwa anaonesha kuwa yuko kwenye mlengo wa chama cha mafisadi ccm bado ungemuonya kuwa anajiweka katika hatari ya kuchinjw?
 
Huyo Nyerere unaemtaja sisi wengine tulikuwa secondary school wakati wa utawala wake, kulikuwa na uoga hata mwenge ukipita wilayani. Kuna wakati watu walikua wakipotea tu, Seif Sharif Hamad na akina Duni Haji kwa kusema ukweli walitiwa kizuizini na walipotoka ndio walikuja na madevu. Nchi za kiswahili hazina kanuni, ni kuomba Mungu tu. Angalia Zimbabwe, Uganda, Rwanda, Burundi na DRC Congo utaelewa zaidi
Hivi ulichokiandika kinapinga au kinaunga mkono niliyoyasema..??? Nyerere alitengeneza taifa na watu waoga sana... Leo hii badala ya kumtazama jamaa kwamba alichosema kimepelekea marekebisho kufanyika, mmebaki kumtisha na kumpa maonyo mkuu..!!!
 
Kupitia uzi huu nimeamini ule msemo usemao..... Katika watu 100 watu 90 watasema haiwezekani na 10 tu ndo watasema inawezekana...
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Mwoga nikuogopa kufanya kitu. Mtumwa wa fikira ni kuwaambia wengine waogope kama wewe. Kifo sio kitu kitakacho kufanya usifanye lile unalotaka.COWARDNES IS A THREAT.
 
Ongea na mzee Lowassa atakushauri mawili matatu kuhusu mwenendo wako nyakati hizi
 
#NENO_LA_SHUKRANI.

Na Kumbusho Dawson

Siku ya tarehe 03/12/2017 katika ukurasa wangu wa Facebook nilichapisha chapisho lililoambatana na picha zinazoonesha nyufa katika moja kati ya majengo ya Hostel Mpya, zilizopo Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Dk.J.P. Magufuli Hostel. Siku iliyofuata, Tar. 04/12/2017 Nilikamatwa na vyombo tofauti vya usalama kuanzia Auxilliary Police wa Chuo, Polisi na baadae kufikishwa Kituo cha Polisi Osterbay na Siku iliyofuata Tar. 05/12/2017, nikahamishiwa Kituo Kikuu cha Polisi Kanda ya Dar es salaam CENTRAL POLICE.
Tuhuma zilizokuwa zinanikabili na nilizoambiwa wakati nahojiwa, ilikuwa ni kupiga picha na kuzisambaza. Hili ni neno langu la shukrani kwa Ndugu, jamaa, marafiki na walimu wangu walioshiriki kwa Namna yoyote wakati nashikiliwa na Polisi. Kipekee nimshukuru Spika wangu, wa Bunge Makini na la Viwango. Mh. Deogratius Mahinyila kwa kuwa na mimi mwanzo hadi mwisho na hata kuniwekea dhamana ilipokuwa inahitajika. Nawashukuru wabunge wenzangu wa Bunge la Daruso kwa upendo na ushirikiano wao.
Aidha, nawashukuru Makam wa Rais wa Serikali ya wanafunzi Daruso Mh. Annastazia Anthony,Naibu Spika, Mh. Geofrey Saddy Mwakapijila, Waziri Mkuu, Mh. Fredrick Sintau , Mwenyekiti Wangu Mh. Vedastos Daniel Kuboja ,na rafiki zangu wote wakiwakilisha na Joseph Ntele, Luccy Shayo na Abdallah Mtonda. Hamkuwa mbali na kwa kuwakilisha wenzenu wengi walioonesha upendo wao, ninawashukuru sana na Mungu atawabariki.
Kipekee navishukuru Vyombo vya habari kwa kutokuwa mbali na tukio lile toka kukamatwa kwangu mpaka nilipoachiwa. Kipekee Zaidi, niwashukuru Watanzania wote mlioonesha upendo wenu kwangu bila ya kujali chochote. Nimebarikiwa sana na upendo wa baadhi ya watu ambao kiuhalisia nilijiridhisha walikuwa hawajui kama nilikuwa naonewa au nilikuwa nastahili kupitia hatua zile, lakini wao waliamini natakiwa kupendwa katika hali yoyote na lolote nitakalokuwa nimefanya.

#FUNZO_NILILOPATA_NA_UHALISIA_WA_KUMBUSHO_DAWSON.

Ukweli ni Ukweli tu hata kama ukisemwa na nani, Ukweli hauna Chama na hauangalii sura. Mimi binafsi nina akili huru na timamu. Sijawahi na haitakuja kutokea nikafanya kitu kwasababu Fulani kasema. Nina akili na utashi, nilifanyalo lolote ni matokeo ya uchambuzi na tafakari yangu binafsi mara baada ya kuwa na wazo la kufanya au mara baada ya kuambiwa chochote. Mtu yeyote anayekuwa na mawazo ya kijinga kwa kudhani kila nilifanyalo nimetumwa, huwa naacha kumuheshimu Siku hiyo kwasababu hakuna dharau kubwa kama mtu kukuweka katika kundi la watumikaji. Chuo kikuu cha Dar es Salaam kihistoria ni Chuo kinachozalisha vijana makini na wanaojitambua, Hakika siwezi kuwa miongoni mwa vijana wachumia tumbo, mnafiki na mwenye kujipendekeza kwa mtu yeyote na hata kufikia hatua ya kutokuwa na akili huru ya kusema mambo yakawaida kabisa nitakayoamini ni Sahihi.
Nimewamiss sana rafiki zangu wote katika mitandao ya kijamii, naendelea kusubiria rehema za Polisi kama nitapata simu zangu mbili hivi karibuni ili tuweze kuendelea na maisha yetu ya kawaida. Nasikia kujua takwimu ni jambo muhimu sana kipindi hiki. Mimi nina takwimu moja hapa ambayo nina uhakika nayo, Kati ya Zaidi ya vijiji 19,200 tulivyonavyo, hakuna hata kijiji kimoja ambacho zile Milioni hamsini tulizoahidiana kwenye kampeni za 2015 zimewafikia.

Miaka saba itapendeza sana…… Shubamiiiiiiiiiti.

MERRY CHRISTMASS AND HAPPY NEW YEAR.
Kumbusho Dawson,
Mkulima.
Dogo nkwambie kitu!!!!!achana na siasa soma kwanza ukishamaliza unaezaa ukawabanaa koz utakuwa umeelewaa nini maana ya nchi nanan anaimiliki na utaelewaa nini democracy but for now fight
 
Muache kuishi kwa mazoea hivi mnafikiri kama wakina mkwawa na machifu wengine hawakuzuia ushenzi wa wazungu leo hii mngekua na uhuru mlio nao kwenye nyumba na mitaa yenu.
Mtu akilivuruga lazima asahihishwe tuu ili siku nyingine awe makini. Tatizo lenu watanzania mna nidhamu za woga hivyo mnaendekeza upuuzi tuu.

Hebu fikiria bro kama asingeweka hizo expansion joint hapo unadhani roho za watu zingekua wapi baada ya muda mfupi maana najua hivyo vijengo havina muda mrefu hapo.
Tunahitaji mashujaa ili kuokoa maisha ya watu kama hawa sio waoga waoga tuu!
Na niwaambie tuu watanzania yote mnayoyaona sasa ni matokeo ya uzezeta wenu wa kumezea ushenzi huku mkijipa matumaini 0.
Watu waliojitambua kama Nigeria, Ghana, Kenya n.k leo hii wako mbali kwa sababu waliamua kufanya kweli na kusema ni mwiko kuendekeza upuuzi wa wajinga fulani.
Hivyo kama mnataka matokeo chanya na ya uhakika lazima mjitathimi na muachane kabisa na maisha ya ujima na mawazo mgando... Kumekucha sasa tokeni gizani.

Viva bro ulini inspire kinoma...
 
53 Reactions
Reply
Back
Top Bottom