Neno la shukrani alilotoa kijana aliyepiga picha expansion joints za hostel

Aaron

JF-Expert Member
Nov 18, 2010
3,019
4,693
#NENO_LA_SHUKRANI.

Na Kumbusho Dawson

Siku ya tarehe 03/12/2017 katika ukurasa wangu wa Facebook nilichapisha chapisho lililoambatana na picha zinazoonesha nyufa katika moja kati ya majengo ya Hostel Mpya, zilizopo Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Dk.J.P. Magufuli Hostel. Siku iliyofuata, Tar. 04/12/2017 Nilikamatwa na vyombo tofauti vya usalama kuanzia Auxilliary Police wa Chuo, Polisi na baadae kufikishwa Kituo cha Polisi Osterbay na Siku iliyofuata Tar. 05/12/2017, nikahamishiwa Kituo Kikuu cha Polisi Kanda ya Dar es salaam CENTRAL POLICE.
Tuhuma zilizokuwa zinanikabili na nilizoambiwa wakati nahojiwa, ilikuwa ni kupiga picha na kuzisambaza. Hili ni neno langu la shukrani kwa Ndugu, jamaa, marafiki na walimu wangu walioshiriki kwa Namna yoyote wakati nashikiliwa na Polisi. Kipekee nimshukuru Spika wangu, wa Bunge Makini na la Viwango. Mh. Deogratius Mahinyila kwa kuwa na mimi mwanzo hadi mwisho na hata kuniwekea dhamana ilipokuwa inahitajika. Nawashukuru wabunge wenzangu wa Bunge la Daruso kwa upendo na ushirikiano wao.
Aidha, nawashukuru Makam wa Rais wa Serikali ya wanafunzi Daruso Mh. Annastazia Anthony,Naibu Spika, Mh. Geofrey Saddy Mwakapijila, Waziri Mkuu, Mh. Fredrick Sintau , Mwenyekiti Wangu Mh. Vedastos Daniel Kuboja ,na rafiki zangu wote wakiwakilisha na Joseph Ntele, Luccy Shayo na Abdallah Mtonda. Hamkuwa mbali na kwa kuwakilisha wenzenu wengi walioonesha upendo wao, ninawashukuru sana na Mungu atawabariki.
Kipekee navishukuru Vyombo vya habari kwa kutokuwa mbali na tukio lile toka kukamatwa kwangu mpaka nilipoachiwa. Kipekee Zaidi, niwashukuru Watanzania wote mlioonesha upendo wenu kwangu bila ya kujali chochote. Nimebarikiwa sana na upendo wa baadhi ya watu ambao kiuhalisia nilijiridhisha walikuwa hawajui kama nilikuwa naonewa au nilikuwa nastahili kupitia hatua zile, lakini wao waliamini natakiwa kupendwa katika hali yoyote na lolote nitakalokuwa nimefanya.

#FUNZO_NILILOPATA_NA_UHALISIA_WA_KUMBUSHO_DAWSON.

Ukweli ni Ukweli tu hata kama ukisemwa na nani, Ukweli hauna Chama na hauangalii sura. Mimi binafsi nina akili huru na timamu. Sijawahi na haitakuja kutokea nikafanya kitu kwasababu Fulani kasema. Nina akili na utashi, nilifanyalo lolote ni matokeo ya uchambuzi na tafakari yangu binafsi mara baada ya kuwa na wazo la kufanya au mara baada ya kuambiwa chochote. Mtu yeyote anayekuwa na mawazo ya kijinga kwa kudhani kila nilifanyalo nimetumwa, huwa naacha kumuheshimu Siku hiyo kwasababu hakuna dharau kubwa kama mtu kukuweka katika kundi la watumikaji. Chuo kikuu cha Dar es Salaam kihistoria ni Chuo kinachozalisha vijana makini na wanaojitambua, Hakika siwezi kuwa miongoni mwa vijana wachumia tumbo, mnafiki na mwenye kujipendekeza kwa mtu yeyote na hata kufikia hatua ya kutokuwa na akili huru ya kusema mambo yakawaida kabisa nitakayoamini ni Sahihi.
Nimewamiss sana rafiki zangu wote katika mitandao ya kijamii, naendelea kusubiria rehema za Polisi kama nitapata simu zangu mbili hivi karibuni ili tuweze kuendelea na maisha yetu ya kawaida. Nasikia kujua takwimu ni jambo muhimu sana kipindi hiki. Mimi nina takwimu moja hapa ambayo nina uhakika nayo, Kati ya Zaidi ya vijiji 19,200 tulivyonavyo, hakuna hata kijiji kimoja ambacho zile Milioni hamsini tulizoahidiana kwenye kampeni za 2015 zimewafikia.

Miaka saba itapendeza sana…… Shubamiiiiiiiiiti.

MERRY CHRISTMASS AND HAPPY NEW YEAR.
Kumbusho Dawson,
Mkulima.
 
Hapo chuo kuna ma-doctor na maprofesa ambao ndio wananoa vijana ukiwemo, na kila mwaka wanatoa products, think twice kwa nini wao ambao wana weledi mkubwa zaidi wako makini na ndimi zao?, ni bahati mbaya ukiwa chuoni (hata sisi tulipokua hapo) unaamini wewe ni intellectual kuliko wajinga wote huko nje. Ukimaliza chuo ukaanza ku-practise real life ndio unakuja kujua uhalisia, in fact upo katika hatua ya either build or destroy your future. Be careful, just an advise!!!
 
Tunakushukuru kwa kutuhabarisha na kusaidia ukarabati wa hostel za vijana wetu, tunakuombea kwa Mungu akubariki na azidi kukulinda, endelea kuwa mkweli bila kujali watu wanaokukatisha tamaa, nadhani hata Magufuli huwa anasema kuwa msemakweli ni mpenzi wa Mungu ingawa sina uhakika kama maneno yake haya huwa yanatoka moyoni au mdomoni
 
Hapo chuo kuna ma-doctor na maprofesa ambao ndio wananoa vijana ukiwemo, na kila mwaka wanatoa products, think twice kwa nini wao ambao wana weledi mkubwa zaidi wako makini na ndimi zao?, ni bahati mbaya ukiwa chuoni (hata sisi tulipokua hapo) unaamini wewe ni intellectual kuliko wajinga wote huko nje. Ukimaliza chuo ukaanza ku-practise real life ndio unakuja kujua uhalisia, in fact upo katika hatua ya either build or destroy your future. Be careful, just an advise!!!
every individual is unique being a doctor or professor doesn't change an individual's instinct. Huku mitaani tunasema kila mtoto anazaliwa na riziki yake, don't threaten but guide them
 
Hapo chuo kuna ma-doctor na maprofesa ambao ndio wananoa vijana ukiwemo, na kila mwaka wanatoa products, think twice kwa nini wao ambao wana weledi mkubwa zaidi wako makini na ndimi zao?, ni bahati mbaya ukiwa chuoni (hata sisi tulipokua hapo) unaamini wewe ni intellectual kuliko wajinga wote huko nje. Ukimaliza chuo ukaanza ku-practise real life ndio unakuja kujua uhalisia, in fact upo katika hatua ya either build or destroy your future. Be careful, just an advise!!!

Sikatai wala kupinga unachokisema, je angekuwa na kipaji cha kucheza mpira, au riadha ungemtaka asuburi mpaka amalize masomo ndio aendelee na kipaji chake? Simshauri huyo kijana kuvutana ama kuendelea na hicho alichokisema, lakini ujasiri ni kitu mtu anazaliwa nacho na sio lazima kufanikiwa kimaisha kwa kusoma.
 
Hapo chuo kuna ma-doctor na maprofesa ambao ndio wananoa vijana ukiwemo, na kila mwaka wanatoa products, think twice kwa nini wao ambao wana weledi mkubwa zaidi wako makini na ndimi zao?, ni bahati mbaya ukiwa chuoni (hata sisi tulipokua hapo) unaamini wewe ni intellectual kuliko wajinga wote huko nje. Ukimaliza chuo ukaanza ku-practise real life ndio unakuja kujua uhalisia, in fact upo katika hatua ya either build or destroy your future. Be careful, just an advise!!!
Ujinga huu kufundisha jamii ya watu wasioweza kuhoji
Ccm mkubwa wewe
 
Hapo chuo kuna ma-doctor na maprofesa ambao ndio wananoa vijana ukiwemo, na kila mwaka wanatoa products, think twice kwa nini wao ambao wana weledi mkubwa zaidi wako makini na ndimi zao?, ni bahati mbaya ukiwa chuoni (hata sisi tulipokua hapo) unaamini wewe ni intellectual kuliko wajinga wote huko nje. Ukimaliza chuo ukaanza ku-practise real life ndio unakuja kujua uhalisia, in fact upo katika hatua ya either build or destroy your future. Be careful, just an advise!!!
Udsm wasomi walikuwa zamani
 
53 Reactions
Reply
Back
Top Bottom