Neno la shukrani alilotoa kijana aliyepiga picha expansion joints za hostel

Wanasiasa wanasajiliwa wapi!?

acha ujinga wewe!!! utakuja hapa tena useme hana chuo!!! akipigwa disco, utatueleza huwa inasajiriwa wapi

aache ubinafsi kijiji chake, mama yake, baba yake na ndugu zake wanatamani amalize chuo...kisha ayafanye mengine at least akiwa na jiwe moja begani

hata huo ubunge ataufanya vizuri akiwa na degree!!

walimu wa udsm sio wapuuzi ni intelligent na ni wazazi kamili, wakiona anasumbua wanamwachisha mapema tu

bahati mbaya uliishia viunga vya zile kozi za certificates pale manzese darajani, maana kama una degree ungemshauri asome kwanza.

hata walioko chekechea sasa hivi wengi tu ni wanasiasa, ila wanalelewa kwanza

Lissu alikuwa mwenyekiti wa faculty ya sheria na enzi anafanya siasa ndani ya UDSM, wala hakupambana na serikali. alimaliza kwanza chuo, akapiga masters akaanza yake!! kichwani yuko vizuri kafundishwa katulia, thats what all intelligent people do
 
Kijana bora kwanza upate degree yako na kwa sasa uwatumikie wanafunzi waliokuchagua hapo chuoni katika kutatua matatizo ya chuoni kupitia mamlaka za hapo......maana usishangilie ushindi wakati hata hujamaliza pambano..!
 
Aya ya mwisho na vibwagizo vya chini vitamu sana kwa mkulu ila simu ndio hawatazirejesha labda uombe msaada wa mahakama na usishangae kama una laptop wakaitaka pia!!

Nungunungu analazimisha aombewe na akumbatiwe!!!!
 
Huyu dogo anawezafika mbali sana...hata serikalini au taasisi nyeti wanapenda watu wenye guts na kujiamini.....na ni bado mdogo..hivyo ni rahisi kumuhamisha anachoamini akapewa ideology nyingine akaanza kupiga mzigo.Katika maisha wakati mwingine ni vizuri kujionesha kipaji au uwezo wako..watu watakuchukua na kukupachika sehemu tu....
Hivyo msichukulie kimtazamo hasi tu..angalieni na upande mwingine....Dogo anaweza akatoboa mkashangaa....kuna historia ya wanasiasa waliokua machachari sana vyuoni wakipambana na serikali..but walifika mbali tena ndani ya CCM
 
Ushauri tu, usishindane na wenye nchi bado una safari ndefu sana ya kimaisha. Maliza shule kwanza. Unahitaji kifua kipana kufanya hayo na kwako bado sana, soma kwanza hayo mengine waachie wanasiasa.
Ndugu Usirudie kumwambie mwanaume hivo?Wenye nchi?Unawajua wenye nchi wewe?Tatizo lenu mnajifikiria ninyi na uoga wenu wa kindezi na mnafikiri mnaweza kuambukiza uwoga wenu kwa wengine.Usisahau,kufa na kuzaliwa ni mara moja ila ukikabuli kutumiwa wewe ni maiti anayetambea kama una bisha basi mwambie mke wako kama unaye kuwa Mimba inayofuata utabeba wewe yeye akutie tu halafu niambie unajisikiaje.Shubaamit!!!
 
Ushauri tu, usishindane na wenye nchi bado una safari ndefu sana ya kimaisha. Maliza shule kwanza. Unahitaji kifua kipana kufanya hayo na kwako bado sana, soma kwanza hayo mengine waachie wanasiasa.
Acha uoga dogo.
 
Wewe mtoto ni katika wajinga wachache waliopo vyuoni. Unaona ulipata 'kick' lakini siyo lengo lililokupeleka chuoni hapo.
Uliza waliopita kabla yako hapo na waliokuwa wana tabia kama zako.
 
We need fearless generation
 

Attachments

  • VID-20180109-WA0005.mp4
    10.7 MB · Views: 14
acha ujinga wewe!!! utakuja hapa tena useme hana chuo!!! akipigwa disco, utatueleza huwa inasajiriwa wapi

aache ubinafsi kijiji chake, mama yake, baba yake na ndugu zake wanatamani amalize chuo...kisha ayafanye mengine at least akiwa na jiwe moja begani

hata huo ubunge ataufanya vizuri akiwa na degree!!

walimu wa udsm sio wapuuzi ni intelligent na ni wazazi kamili, wakiona anasumbua wanamwachisha mapema tu

bahati mbaya uliishia viunga vya zile kozi za certificates pale manzese darajani, maana kama una degree ungemshauri asome kwanza.

hata walioko chekechea sasa hivi wengi tu ni wanasiasa, ila wanalelewa kwanza

Lissu alikuwa mwenyekiti wa faculty ya sheria na enzi anafanya siasa ndani ya UDSM, wala hakupambana na serikali. alimaliza kwanza chuo, akapiga masters akaanza yake!! kichwani yuko vizuri kafundishwa katulia, thats what all intelligent people do
Kuwa na degree sio issue anachotakiwa ni kuelimika na kutumia elimu yake kupambanua changamoto zinazomkabili yeye familia na jamii inayomzunguka.Ifikie wakati tuache kuwa watu wa kufaulu mitihani ilhali kile tulichoenda kusomea hakitumiki kutatua changamoto zinazotukabili.
 
Hapo chuo kuna ma-doctor na maprofesa ambao ndio wananoa vijana ukiwemo, na kila mwaka wanatoa products, think twice kwa nini wao ambao wana weledi mkubwa zaidi wako makini na ndimi zao?, ni bahati mbaya ukiwa chuoni (hata sisi tulipokua hapo) unaamini wewe ni intellectual kuliko wajinga wote huko nje. Ukimaliza chuo ukaanza ku-practise real life ndio unakuja kujua uhalisia, in fact upo katika hatua ya either build or destroy your future. Be careful, just an advise!!!
Nyerere, kwenye moja ya hotuba zake, alisema, NANUKUU... SIKUDHANI KAMA NINGETENGENEZA TAIFA LA WATU WAOGA SANA.....mwisho wa kunukuu...

"Zile expansion joints" naamini hadi leo zingekuwepo, kama asingesema... MAANA KUSINGEKUWA NA WA KUSEMA

Kwenye kila jambo, kama hakuna wa kujitoa, hakuna maendeleo... LEO HII NYERERE TUNAMWITA BABA WA TAIFA... unajua sababu?

Leo hii raisi wetu tunamwona anafanya vizuri, tunajuwa sababu?

YES umepita chuo, umesoma pale, LAKINI NAHISI KUPITA PALE HAKUJAKUSAIDIA....

The best way, ungekaa kimya...
 
"....Some people are being strengthened by hard hands..."
Oliver Thambo
 
Kasome kwanza , kijana ukijitazama kwenye kioo mwili wako una sisimuka unadhani umekomaa, hapana, mbegu za kizazi chako bado, rudi shule kwanza. Lakini nasikitika kuona umejichafu na kujilaani. Watu wabaya wanakuona, shetani naye atakuandama ungali bado mtoto. Acha siasa nenda shule. Kinga yako toka sasa niya kubahatisha bahatisha. Acha siasa sisi wazazi wako tusikupoteze mapema. Siasa ni kuchinjana , kufa au kupona.
 
Ushauri tu, usishindane na wenye nchi bado una safari ndefu sana ya kimaisha. Maliza shule kwanza. Unahitaji kifua kipana kufanya hayo na kwako bado sana, soma kwanza hayo mengine waachie wanasiasa.
Acha ufisi ndugu..
Wenye nchi akina nani??
Acha watu wawe huru kutoa yaliyo kwenye vifua vyao..
Kama wewe muoga kaa mwenyewe kimya...
Alaaa.
 
#NENO_LA_SHUKRANI.

Na Kumbusho Dawson

Siku ya tarehe 03/12/2017 katika ukurasa wangu wa Facebook nilichapisha chapisho lililoambatana na picha zinazoonesha nyufa katika moja kati ya majengo ya Hostel Mpya, zilizopo Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Dk.J.P. Magufuli Hostel. Siku iliyofuata, Tar. 04/12/2017 Nilikamatwa na vyombo tofauti vya usalama kuanzia Auxilliary Police wa Chuo, Polisi na baadae kufikishwa Kituo cha Polisi Osterbay na Siku iliyofuata Tar. 05/12/2017, nikahamishiwa Kituo Kikuu cha Polisi Kanda ya Dar es salaam CENTRAL POLICE.
Tuhuma zilizokuwa zinanikabili na nilizoambiwa wakati nahojiwa, ilikuwa ni kupiga picha na kuzisambaza. Hili ni neno langu la shukrani kwa Ndugu, jamaa, marafiki na walimu wangu walioshiriki kwa Namna yoyote wakati nashikiliwa na Polisi. Kipekee nimshukuru Spika wangu, wa Bunge Makini na la Viwango. Mh. Deogratius Mahinyila kwa kuwa na mimi mwanzo hadi mwisho na hata kuniwekea dhamana ilipokuwa inahitajika. Nawashukuru wabunge wenzangu wa Bunge la Daruso kwa upendo na ushirikiano wao.
Aidha, nawashukuru Makam wa Rais wa Serikali ya wanafunzi Daruso Mh. Annastazia Anthony,Naibu Spika, Mh. Geofrey Saddy Mwakapijila, Waziri Mkuu, Mh. Fredrick Sintau , Mwenyekiti Wangu Mh. Vedastos Daniel Kuboja ,na rafiki zangu wote wakiwakilisha na Joseph Ntele, Luccy Shayo na Abdallah Mtonda. Hamkuwa mbali na kwa kuwakilisha wenzenu wengi walioonesha upendo wao, ninawashukuru sana na Mungu atawabariki.
Kipekee navishukuru Vyombo vya habari kwa kutokuwa mbali na tukio lile toka kukamatwa kwangu mpaka nilipoachiwa. Kipekee Zaidi, niwashukuru Watanzania wote mlioonesha upendo wenu kwangu bila ya kujali chochote. Nimebarikiwa sana na upendo wa baadhi ya watu ambao kiuhalisia nilijiridhisha walikuwa hawajui kama nilikuwa naonewa au nilikuwa nastahili kupitia hatua zile, lakini wao waliamini natakiwa kupendwa katika hali yoyote na lolote nitakalokuwa nimefanya.

#FUNZO_NILILOPATA_NA_UHALISIA_WA_KUMBUSHO_DAWSON.

Ukweli ni Ukweli tu hata kama ukisemwa na nani, Ukweli hauna Chama na hauangalii sura. Mimi binafsi nina akili huru na timamu. Sijawahi na haitakuja kutokea nikafanya kitu kwasababu Fulani kasema. Nina akili na utashi, nilifanyalo lolote ni matokeo ya uchambuzi na tafakari yangu binafsi mara baada ya kuwa na wazo la kufanya au mara baada ya kuambiwa chochote. Mtu yeyote anayekuwa na mawazo ya kijinga kwa kudhani kila nilifanyalo nimetumwa, huwa naacha kumuheshimu Siku hiyo kwasababu hakuna dharau kubwa kama mtu kukuweka katika kundi la watumikaji. Chuo kikuu cha Dar es Salaam kihistoria ni Chuo kinachozalisha vijana makini na wanaojitambua, Hakika siwezi kuwa miongoni mwa vijana wachumia tumbo, mnafiki na mwenye kujipendekeza kwa mtu yeyote na hata kufikia hatua ya kutokuwa na akili huru ya kusema mambo yakawaida kabisa nitakayoamini ni Sahihi.
Nimewamiss sana rafiki zangu wote katika mitandao ya kijamii, naendelea kusubiria rehema za Polisi kama nitapata simu zangu mbili hivi karibuni ili tuweze kuendelea na maisha yetu ya kawaida. Nasikia kujua takwimu ni jambo muhimu sana kipindi hiki. Mimi nina takwimu moja hapa ambayo nina uhakika nayo, Kati ya Zaidi ya vijiji 19,200 tulivyonavyo, hakuna hata kijiji kimoja ambacho zile Milioni hamsini tulizoahidiana kwenye kampeni za 2015 zimewafikia.

Miaka saba itapendeza sana…… Shubamiiiiiiiiiti.

MERRY CHRISTMASS AND HAPPY NEW YEAR.
Kumbusho Dawson,
Mkulima.
dogo .. no worries we got your back 101%.

sisi wahenga tulishapitaga hapo miaka ya nineteen kweusi. we know what it takes to fight the oppressors and - dogo - you're on the right track.
 
siku utakapotoka hapo chuoni na kuingia mtaani ndo tajua maisha ni nini,mind you wachout you still have long way to go....
 
Back
Top Bottom