Neno la Mpiganaji Zitto kwa mawaziri wapya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Neno la Mpiganaji Zitto kwa mawaziri wapya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by KIM KARDASH, May 5, 2012.

 1. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #1
  May 5, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  [h=3]MH. ZITTO KABWE AWAAMBIA MAWAZIRI, "HAKUNA SHEREHE, NENDENI MKAWAJIBIKE"...!!![/h]
  [h=1]
  [​IMG]
  Mh. Zitto Kabwe
  ---
  Juhudi za kurejesha misingi ya uwajibikaji katika utumishi wa umma zimeanza kuzaa matunda Baada ya Rais kutekeleza shinikizo la Bunge la kuwafukuza kazi baadhi ya Mawaziri ambao Wizara zao zimetuhumiwa kwa ubadhirifu wa fedha za umma, rushwa na utendaji mbovu. Mawaziri 6 wamefukuzwa kazi baada ya kugoma kujiuzulu wao wenyewe, manaibu Waziri 2 wamefukuzwa pia.  Ndugu George Mkuchika alitakiwa kujiuzulu, akajiuzulu lakini Rais amemrudisha kwenye Baraza Kama Waziri wa Utawala Bora. Yeye nampongeza kwani hakuwa na makuu ya kuanza kujitetea Kama wengine. Atakuwa ametoa funzo kwa wenzake.  Kwa kawaida wateule hufanya sherehe kwa kuteuliwa kwao. Nitawashangaa watakaofanya sherehe safari hii kwani hakuna cha kufurahia. Nitawashangaa Watakaokwenda kuapa na Maua kwa furaha kwani furaha itakuwa ya muda mfupi tu. Mkutano wa Bunge wa Bajeti ni mwezi ujao tu na Wateule wote watakuwa kikaangoni. Too short honeymoon.Hakuna cha kusherehekea kwa sababu nchi in changamoto nyingi sana.  Changamoto ya kuzalisha umeme wa kutosha na kuusambaza kwa wananchi wengi, changamoto ya kukuza uchumi wa vijijini na kukuza uzalishaji viwandani ili kutengeneza ajira kwa vijana, changamoto ya kuongeza mapato ya Utalii kutoka katika hifadhi zetu na kuvutia watalii zaidi katika nchi yetu.

  [/h]
   
 2. Kiganyi

  Kiganyi JF-Expert Member

  #2
  May 5, 2012
  Joined: Apr 30, 2012
  Messages: 1,244
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Imeshajadiliwa hapa!!

  Punguza ulevi
  :yawn:
   
 3. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #3
  May 6, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  ok...........i will.
   
Loading...