Neno La Leo: Yesu Akasema; Simon, Acha Kuvua Samaki, E Nenda Ukawe Mvuvi Wa Watu" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Neno La Leo: Yesu Akasema; Simon, Acha Kuvua Samaki, E Nenda Ukawe Mvuvi Wa Watu"

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by maggid, Apr 8, 2012.

 1. m

  maggid Verified User

  #1
  Apr 8, 2012
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Ndugu Zangu,


  Bwana Yesu alipotembelea mto Galilaya, aliwakuta wavuvi wakivua samaki, Simoni alikuwa ni miongoni mwa wavuvi hao. Yesu akasema; " Simoni, acha kuvua samaki,nifuate ukawe mvuvi wa watu. Naam. Watu wengi wanaangamia kwa kukosa uelewa. Kwa kutojitambua. Wanahitaji ukombozi wa kifikra.

  Na siku zote, haki uinua taifa, vivyo hivyo, dhulma huangamiza taifa. Na mahala pasipo na haki, basi, hapo hapatukuwa na amani.Oneni, maovu yametamalaki katika dunia tunaoishi. Siku zote, kujipendelea ndilo shina la maovu.

  Si tuna mifano hai. Oneni, wale wenzetu waliokaa na wakaamua kuuza nyumba za Serikali. John Magufuli ni mmoja wa watu hao. John alisimamia utekelezaji wa dhulma ile kwa Watanzania. Lililopelekea uamuzi wa hila na ghilba wa kuuza nyumba za serikali ni ubinafsi na hulka ya baadhi ya viongozi kutaka kujipendelea.

  Karibu wote waliouziwa au kujiuzia nyumba hizo za Serikali, nyumba za wananchi, tayari walikuwa na nyumba kabla. Siku zoe, hamu inakuwa ni jambo jema, endapo binadamu ataweza kuitawala hamu/tamaa yake.

  Wanadamu tusipoitawala hamu yetu, tukaanza kujipendelea, kuwasahau wengine, basi, hilo huwa ndio chimbuko la maovu. Hupelekea kutoelewana baina ya wanandugu, na hata kwa marafiki walioshibana.

  Hupelekea vurugu na machafuko katika jamii. Tunazungumzia uwepo wa upendo, haki na usawa. Dini nyingi zinazungumzia umuhimu wa upendo, haki na usawa katika jamii. Iwe ni Uislamu na Ukristo vivyo hivyo. ”

  Naapa kwa zama . Hakika binadamu wote wamo katika hasara isipokuwa wale walioamini na wakafanya matendo mema. Wakahusiana na haki na wakahusiana na subira” (Koran tukufu, Surat ASWR)

  Biblia nayo inasema; kuwa Kaini alikuwa mtu wa kujipendelea mno, akamwua nduguye. Mfalme Saulo alijipendelea mno, akamdhulumu Daudi. Yuda alijipendelea mno, akalikubali kumsaliti Yesu kwa Vipande thelathini vya fedha. Hatimaye, akamsaliti Yesu.

  Na ufufuko wa Bwana Yesu utukumbushe jukumu letu la kupambana na maovu katika jamii. Utukumbushe jukumu la kusaidia kazi ya kuwakomboa kifikra wanadamu wenzetu. Kama Bwana Yesu alivyomkumbusha Simoni kwa kumwambia; ” Simoni, acha kuvua samaki. E nenda ukawe mvuvi wa watu. Na hilo ndilo Neno la Leo. Pasaka Njema.


  Maggid Mjengwa,
  Dar es Salaam
  0788 111 765
  http.//mjengwablog.com
   
 2. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #2
  Apr 8, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Majjid siamini kama ni mgeni wakushindwa kujua jukwaa gani la kupost japokuwa nimeona kipande kimoja tu kinachoweza kukaa hapa cha Magufuli na uuzaji nyumba.

  Ok, mimi nimependa sana ile aya ya Qurani iliyonakiri kusema kweli ni aya nzito kwa watu wenye kumjua Mungu. Nashukuru kwa message yako ya Easther.
   
 3. Gwalihenzi

  Gwalihenzi JF-Expert Member

  #3
  Apr 8, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 5,117
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Maggid, unamtafuta maneno Magufuli, shauri yako!
   
 4. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #4
  Apr 8, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,781
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  1.Kwa sababu wewe ni MWANDISHI wa HABARI tena ALIYEBOBEA umeandika ARTICLE ya KIDINI kwenye JUKWAA LA KISIASA na IKIWA HAINA MAUDHUI YOYOTE KISIASA!!
  -My TAKE:
  1:Wewe ni miongoni mwa BINADAMU wanao semekana na SEHEMU KUBWA YA DUNIA kuwa na AKILI SANA!

  2-Kwa kuwa leo ni Pasaka nakusamehe na sikutuhumu tuhuma ya UKILAZA kwa ku POST KWENYE JUKWAA WRONG kwani kuna uwezekano uligonga kilaji!
   
 5. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #5
  Apr 8, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  maggid kwa udini
   
 6. m

  matawi JF-Expert Member

  #6
  Apr 8, 2012
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 2,055
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Haya mambo ya biblia /quran yana ukweli si unaona Lema magamba wamemwambia Arusha inatosha sasa njoo uwakomboe watanzania wote
   
 7. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #7
  Apr 8, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  Mkuu usijali baada ya muda utaona Moved!
  Kazi ya Mods kumuvuzisha
   
 8. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #8
  Apr 8, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  Majjid,
  Mbona unataka kumzibia mwenzio riziki? hujui Pombe anavyojikakamua kutaka kuomba ridhaa ya magamba kugombea urais?
   
 9. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #9
  Apr 8, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 730
  Trophy Points: 280
  JF inazidi kupoteza mvuto kwa post zenye muelekeo wa kidini!
   
 10. B

  Bangoo JF-Expert Member

  #10
  Apr 8, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 5,594
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  bg up mr
   
 11. Hassan J. Mosoka

  Hassan J. Mosoka JF-Expert Member

  #11
  Apr 8, 2012
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 647
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Ahsante Mjengwa kwa ujumbe wa Pasaka
   
Loading...