Neno La Leo: Wasaidizi Wa Nahodha Wanapodanganya! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Neno La Leo: Wasaidizi Wa Nahodha Wanapodanganya!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by maggid, Nov 16, 2011.

 1. m

  maggid Verified User

  #1
  Nov 16, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Ndugu zangu,


  Mwandishi mTanzania Shaaban Robert ni mmoja wa wanafalsafa wa kujivunia waliopata kutokea barani Afrika


  Mwandishi huyu mahiri aliweza kuyaona mengi mbele ya wakati wake. Mathalan, kupitia vitabu vyake kama vile Kusadikika na Adili na Nduguze tunaona jinsi Shaaban Robert alivyokuwa mbele ya wakati wake.


  Na kwenye moja ya maandiko yake ya kifalsafa, Shaaban Robert anasema; “ Ujana ni nusu ya uwendawazimu”. Kuna ujumbe mzito kwenye mtazamo huo wa Shaaban Robert.


  Na swali tunalopaswa kujiuliza ni hili; kama ujana ni nusu ya uwendawazimu, je, uzee ni nusu au ukamilisho wa jambo gani katika maisha?


  Naam, katika ulimwengu huu mwenye miliki ya ujana ni kijana. Ujana hauwezi kuwa wa mzee. Lakini, mzee ndiye mwenye uzoefu na werevu wa nini maana ya kuwa kijana. Maana, mzee alishaupitia ujana. Hutokea, kuwa kijana hajui kama anao ujana maana hajatambua kuwa anaishi katika ujana.


  Mzee atakaa na kujiuma vidole akijilaumu kwa kutofanya hili na lile wakati wa ujana wake. Wakti utakuwa umeshamtupa mkono. Hawezi tena kuurejea ujana.


  Mwone nahodha mzee kwenye jahazi kongwe linalokaribia kuzama majini. Nahodha huyu atachukua darubini yake. Kwa kutumia darubini ataangaza majini na kuangalia chombo kingine kilichojaza abiria. Atawaita wasaidizi wake wakiwamo mainjinia wa chombo.


  Atawaambia; ” Oneni jahazi lile. Ni la juzi tu, lakini lenda mbio vile na limesheheni abiria . Kwanini jahazi letu lina abiria wachache ili hali ni la siku nyingi na sie ni wenye uzoefu sana? Halafu, nasikia mwungurumo usio wa kawaida kwenye injini. Je, kuna hitilafu?”


  Yumkini, wasaidizi wa nahodha watampamba nahodha kwa kile wanachodhani nahodha wao anataka kusikia.


  ” S’tie shaka nahodha, mwungurumo huo ni wa kawaida tu, na sie tutafika salama. Abiria hao watakuja kutambua kuwa sie ni bora kuliko wengine wote!”


  La hasha, wasaidizi wa nahodha wanamwongopea nahodha wao. Kumbe, kama jahazi linakimbiwa na abiria swali la kwanza kujiuliza ni ’ kwa nini?’. Yumkini kuna hitilafu. Kinachopaswa kufanywa ni kutafuta njia ya kurekebisha hitilafu na si kuukimbia ukweli wa tatizo lililopo.


  Na ilivyo majini, kila jahazi huwa na panya wake. Jahazi linapokaribia kuzama, basi, panya wake huwa wa kwanza kurukia majini.


  Ni ipi basi hatma ya panya mzee jahazini?


  ” Nawe unajiandaa kurukia majini?” Anauliza nahodha.


  ”Hapana nahodha wangu. Natamani ningekuwa na miliki ya ujana. Mie ni mzee sana kuweza kurukia majini. Nimeamua kubaki jahazini. Tutazama wote!”


  ” Hivi , si wewe uliyesema nahodha us’tie shaka?!”


  Naam, kama ujana ni nusu ya uwendawazimu, uzee ni nini?

  Shaaban Robert hatunaye. Swali hilo ni letu.


  Maggid,

  Iringa.
  Jumatano, Nov 16, 2011
  MJENGWA - Picha, Habari & Matangazo
   
 2. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #2
  Nov 16, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,526
  Likes Received: 5,674
  Trophy Points: 280
  Nafurahi moja ya waliokuwa wanamdaganya nahodha wameanza kurukia majini kabla jahazi halijazama ili baadae waseme "aah sio sisi tuliomshauri vibaya,tulitoka jahazi likiwa sawa kalizamisha mwenyewe!" Teh teh teh pamoja sana mkuu wangu Maggid!
   
 3. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #3
  Nov 16, 2011
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  hongera kaka hii kiboko
   
Loading...