Neno La Leo: Viongozi Wetu Na Ndege Huyu Tulikuliku | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Neno La Leo: Viongozi Wetu Na Ndege Huyu Tulikuliku

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by maggid, Mar 12, 2012.

 1. m

  maggid Verified User

  #1
  Mar 12, 2012
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Ndugu zangu,

  Ni Jumatatu usiku. Siku inaelekea ukingoni. Naandika nikiitafakari siku ya leo. Kwangu haikuja na jipya. Ni yale yale. Moja kubwa ni dhahiri, kuwa Watanzania bado tuna safari ndefu sana kufikia hatua ya kuitwa taifa la kisasa.


  Tuyafanyayo mengi bado ni mambo ya hovyo hovyo, na wenye kuongoza kuyafanya hayo ya hovyo hovyo ni viongozi wetu. Lakini hatuna jinsi, hatua tunayopitia sasa ni lazima tuipitie. Hakuna njia nyingine ya kupita na kutufikisha kwa haraka tunakotaka kwenda. Tusisahau tu , kutunza kumbukumbu. Tufanye hivyo ili Watanzania wa vizazi vijavyo waje wajifunze kutokana na matendo yetu.


  Tulikuliku ni aina ya ndege. Viongozi wetu wanaweza kujifunza kutoka kwa ndege huyu. Tulikuliku ana kanuni inayomwongoza. Mara ile tulikuliku anapotaga mayai, basi, hufanya maamuzi magumu ya kujinyonyoa manyoya yake.

  Kwa pamoja, tulikuliku dume na jike watafanya tendo hilo.

  Kwanini?
  Wanajiwekea wenyewe mazingira ya kushindwa kuruka. Wanafanya hivyo ili waatamie mayai yao hata atakapotokea nyoka mpenda mayai wapambane nae hapo hapo. Kwamba wangebaki na manyoya, huenda wangemwogopa nyoka. Hivyo, wangeruka na kuacha mayai yakiliwa na nyoka.


  Kwa kiongozi kujinyonyoa manyoya ina maana ya kukubali kushuka chini kwa watu. Kuyaelewa matatizo ya watu anaowaongoza. Kuwa tayari kupambana kuyatatua matatizo ya watu akiwa na watu.


  Ilivyo kwa viongozi wetu wengi wa leo, ni kuwa, katikati ya dhiki kubwa ya wanaowaongoza, si tu wamefuga manyoya mengi, bali, hata pale wananchi wanapokabiliwa na adui maradhi, wao, viongozi, wana mbawa za kuwawezesha kuruka juu angani huku wakiwaimbia watu wao nyimbo za kejeli. Na bado watafanya hila ili kuwachonganisha na kuwagawa watu wao walio kwenye dhahma ya umasikini.

  Na kuna mawili ambayo yaliwezekana kutumiwa na yakafanya kazi miaka ya sitini hadi themanini, na mawili hayo hata yanapotumika sasa, hayafanyi kazi tarajiwa. Maana, wakati umebadilika. Ni yepi hayo?

  Naam, ni kwa kiongozi kutumia Uongo na kutishia nguvu za mamlaka. Kiongozi anayetaka kufanikiwa katika zama hizi ni yule aliye tayari na kuachama na mambo ya zama hizo; kuwaongopea watu wako na kutishia nguvu za mamlaka. Badala yake, kuwa tayari kufanya maongezi hata na wale ambao huko nyuma haikuwezekana kukaa nao meza moja.


  Vinginevyo, Watanzania tungali na safari ndefu sana. Njia ina miba mingi, lakini ni lazima tuipite. Hakuna njia nyingine. Na hili ni neno la leo.


  Maggid Mjengwa

  0788 111 765
  Mjengwa Blog::Habari,Picha,Matangazo
   
 2. K

  Keil JF-Expert Member

  #2
  Mar 12, 2012
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hekima iliyocheleweshwa .....
   
 3. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #3
  Mar 12, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  nENO ZURI SANA. Karibu tena Bukoba
   
 4. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #4
  Mar 12, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,268
  Trophy Points: 280
  Za mbayuwayu changanya na za kwako!.....
   
 5. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #5
  Mar 12, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Tulikuliku
   
 6. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #6
  Mar 12, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180

  Nimependa hii part ya nakala yako... Hii hasa ndio inabeba yooote haya....
   
 7. Companero

  Companero Platinum Member

  #7
  Mar 12, 2012
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
 8. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #8
  Mar 12, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Mamiii, ni lazima tupitishwe kwenye ushenzi, tuuone ushenzi na tujifunze kwa ushenzi huo, then tufanye maamuzi sahihi.

  Ukifuga bata then bata akawa Anakunya sebuleni kila siku, inanity za kwamba, bata Hawaii kufuga nyumbani asilani!

  This regime is bata asiye na adabu
   
 9. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #9
  Mar 12, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
 10. m

  maggid Verified User

  #10
  Mar 12, 2012
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Companero,

  Asante sana, lakini hivyo ndivyo nilivyoipokea siku ya leo. Haikuja na jipya, kwa mtazamo wangu. Leo hapa Iringa niliwahi mapema asubuhi kununua magazeti kuona kama mtani wangu Profesa Lipumba amekuja na jipya kutoka Marekani. Hapana, hata Profesa hakuwa na jipya anaposema Tanzania hakuna demokrasia. Huhitaji kwenda Marekani au kuwa na shahada ya Chuo Kikuu kulifahamu hilo! ( Wanyamwezi wana matatizo yao!) na hasa wanapokuwa wamesoma sana.

  Na leo usiku kupitia TBC1 nimeona Profesa ameongea na wanahabari. Nasubiri kusoma magazeti ya kesho. Natumaini Profesa atakuwa amekuja na jipya kwa siku ya kesho.
   
 11. m

  maggid Verified User

  #11
  Mar 12, 2012
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Birigita,

  Asante kwa maoni yako. Lakini, ni vema ukitaka kunitukana, nitukane mimi tani yako. Na si wengine wanaonihusu na wasiohusika na nilichoandika.
   
 12. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #12
  Mar 12, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,177
  Trophy Points: 280
  Hizi habari tushazisikia tangu enzi za "miezi 18 ya kufunga mkanda" (eighties babies what do you know about that?) au tangu enzi za "fagio la chuma".

  Rais Mwinyi katika hotuba yake moja alishatoa mfano kwamba Watanzania inabidi tu "burn our boats" kama alivyofanya Jemadari Tariq Ibn Ziyad alivyokuwa anavamia Iberia baada ya kupita strait of Gibraltar (Gibraltar = Jabal al Tariq) AD 711, ili kusudi tuseme "failure is not an option" it is "win or die".

  Lakini mpaka leo tunaongea yale yale tu.
   
 13. Hassan J. Mosoka

  Hassan J. Mosoka JF-Expert Member

  #13
  Mar 13, 2012
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 647
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  MKuu Mjengwa,
  Well said nothing was new today, hotuba zilezile, maisha yale yale! Hongera sana kwa ujumbe mwanana
   
 14. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #14
  Mar 13, 2012
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Kwani ni lini tulishawahi kuwa na jipya?
   
 15. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #15
  Mar 13, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  mwenyekiti nimeipenda hii reply
   
 16. K

  Keil JF-Expert Member

  #16
  Mar 13, 2012
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mjengwa Bwana, sasa kaka yangu Prof. Lipumba ana uhusiano gani na hao watawala ambao ulikuwa unawasema kwenye Neno la Leo? Au ulitegemea jipya kutoka kwake akiwa kama nani?

  Usipotezee malengo ya hoja yako ... na ndio maana huwa naona maandiko yako wakati mwingine huwa yanauma na kupuliza. Kwa wale wasoma Biblia unaweza kuitwa "vuguvugu" unawafanya watu washindwe kujua umesimamia wapi. Kama una-wananga watalawa, then wanange moja kwa moja, wala huna haja ya kuficha mapungufu ya utawala wa JK na chama chake tawala kwa kuanza kuzunguka mbuyu kwa kumtaja Lipumba ambaye wala si sehemu ya utawala wa huyo ndege.

  According to hiyo para hapo juu, Prof. Lipumba ana nguvu za mamlaka?

  Finally, labda nikuulize, je, wewe ulitegemea nini siku ya jana ambacho kingeifanya Jumatatu iwe tofauti na siku nyingine? Au ulitegemea hotuba ya JK iwe bomba sana na kummwagia sifa ya hekima iliyochelewa? Ninaisubiri kwa shauku kubwa sana Tafsiri yako ya Hotuba ya JK kwa Taifa kupitia kwa Wazee wa Dar!
   
Loading...