Neno La Leo: Ukimwona Rais Wa Nchi Anakasirikia Umbea... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Neno La Leo: Ukimwona Rais Wa Nchi Anakasirikia Umbea...

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by maggid, May 18, 2011.

 1. m

  maggid Verified User

  #1
  May 18, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Ndugu Zangu,


  Pichani ni ' Chifu' wa mtandao wa Tanzanet, Mzee Yussuf Kalala. Nilikutana nae Dar jana. Tuliongea kwa kirefu. Mzee Kalala ana mengi ya kuelimisha, ikiwamo maarifa ya kihistoria. Ameishi Washington DC kwa miaka mingi. Tumefahamiana tangu enzi za mtandao wa Tanzanet ya miaka 1998 na kuendelea. Nakumbuka nilivyoingia Tanzanet kwa mara ya kwanza ni pale Ben Mkapa alipotembelea Sweden mwaka 1998.


  Watanzania tulialikwa nyumbani kwa Balozi Samson Kasekka jioni moja, kwa chakula na vinywaji. Na hapo alikuwepo Mkapa na Waziri wake wa Mambo ya Nje, Jakaya Kikwete.


  Mkapa aliongea machache sana, kisha akaondoka zake na hatukumwona tena, nyuma alimwacha Kikwete akiongea na Watanzania. Na katika machache aliyosema Mkapa nakumbuka alitamka; " Na kule kwenye mtandao wa Tanzanet kuna watu kazi yao ni kusema mambo ya umbea umbea tu!". Kwa kufanya hivyo, Mkapa akawa ameitangaza Tanzanet ambayo hata mimi sikuijua wakati huo.


  Nilipofika nyumbani tu , cha kwanza ni kuitafuta Tanzanet na kujiunga nayo, si kwa sababu wanasema umbea umbea, bali ni kufahamu kuwa wanaosema umbea ni wengi, lakini ukimwona Rais anakasirika hadharani juu ya umbea wa watu fulani, basi ujue, ndani yake kuna yasiyo ya umbea. Ni ya ukweli. Na mwanadamu siku zote awe na kiu ya kuutafuta ukweli.


  Na wanadamu tumejaliwa akili ili tuweze kufikiri. Na kufikiri ndio njia mojawapo ya kuiteka kweli. Kufikiri kunahamisha milima na hata kuiweka kando kuruhusu mwanga upite. Inakuwaje basi mwanadamu anapoacha kufikiri?Na hilo ni Neno La Leo.


  Maggid,
  Dar es Salaam
  Jumatano, Mei 18, 2011

  MJENGWA - Picha, Habari & Matangazo


   
 2. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #2
  May 18, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Picha ipo wapi?
   
 3. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #3
  May 18, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,923
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Mi binafsi sijaelewa hasa una-maanisha nini, malezo yote nimeyasoma lakini sijapata anythng behind the truth. Na hii ndiyo style yako ya uandishi always. Najua JK nchi imemshinda sasa anatafuta wa kufa nae, sasa sijui yy ndo m-mbea!!
  Anyway,nitarudi kusoma comment za wengine labda nitaambulia smthg.
   
 4. Manumbu

  Manumbu JF-Expert Member

  #4
  May 18, 2011
  Joined: Oct 28, 2009
  Messages: 1,751
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  huyo alikuwa Ben akipayuka vya kwake wakati huo na leo tunaweza kumwelewa vizuri sana kwa nini aliwaita wengine wambeya kwa vile walikuwa wanaingilia 'ulaji' fulni fulni. so somo la leo ni nini hasa? tuliyenaye leo ambaye nyinyi mlibaki nae wakati huo mkisogoa nae kapandishia watu umbeya? tafadhari tuelimishe tuchangie kwa sasa ili kweli liwe somo la leo tukiichanganya na hiyo topic ya sweden ya miaka hiyo ya mkapa
   
 5. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #5
  May 18, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,277
  Trophy Points: 280
  Mimi hapa nimetoka kapa, nahata hiyo picha siioni hapa. Maggid uandishi wa namna hii haukubaliki.
   
 6. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #6
  May 18, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,499
  Likes Received: 19,913
  Trophy Points: 280
  hahah wazee imebidi nicheke, soma tena bandiko la maggid na utajua anachokimaanisha na wala content ya bandiko lake halipo kwenye hiyo picha mnayoidai hapa
  ok picha hii hapa
  [​IMG]
   
Loading...