Neno La Leo: Tunaposubiri Kuhesabiwa Na Dhana Ya Kiumbe Mzito.. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Neno La Leo: Tunaposubiri Kuhesabiwa Na Dhana Ya Kiumbe Mzito..

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by maggid, Aug 25, 2012.

 1. m

  maggid Verified User

  #1
  Aug 25, 2012
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Ndugu zangu,  Kwa siku kadhaa nimekuwa nje ya mitandao. Hata magazeti, redio na televisheni zimenipitia kando. Jioni hii wakati nikipitia taarifa mbalimbali nimekutana na hili la hoja ya baadhi ya Waislamu kutaka sensa ya watu na makazi itakayofanyika kesho Jumapili igomewe kwa vile haina kipengele ama dodoso linalotaka kujua dini ya mtu.


  Kabla sijatoa maoni yangu juu ya hilo ningependa niitafsiri dhana ya ‘ Kiumbe mzito’ kama tulivyoambiwa na wahenga wetu. Huenda si wengi kati yenu wasomaji wenye kufahamu maana hasa ya usemi wa Wahenga kuwa ‘ Kiumbe mzito’.


  Ndio, Mwenyezi Mungu ametuumba wanadamu kwa usawa kwenye mambo mengi. Wala hakutaka kubagua; ona unyayo wa mwanadamu. U sawa, iwe kwa tajiri au masikini. Wewe na miye tumepata, ama wenyewe au kusikia mtu akilalamika kuwa soli ya kiatu chake imechakaa, kwamba anakwenda kwa fundi viatu kubadilisha soli. Lakini, wewe au miye hatujapata kumsikia mwanadamu mwenzetu akilalamika kuwa unyayo wake umechakaa, anataka kwenda kwa fundi awekewe unyayo mwingine!


  Ndio, wewe na miye ama tumeshuhudia au kusikia kuwa upepo umeangusha mti, nyumba, ghorofa, gari na hata meli. Lakini, jiulize, je, umepata kumwona mwanadamu mwenzako anayetembea kwa miguu akiangushwa kwa upepo?


  Binafsi hilo la mwanadamu kuangushwa na upepo sijapata kulisikia au kuliona kwa macho yangu. Mwanadamu hata awe mwembamba kiasi gani, haiyumkini akaangushwa kwa upepo. Na ukimwona mwanadamu mwenzako anaanguka barabarani, basi, ama ni mgonjwa, au ni mlevi. Na hilo la mwisho haliwezi kuwa na maana ya mwanadamu huyo kaangushwa na upepo, bali kaangushwa na pombe alizokunywa.


  Naam, kiumbe mzito.
  Na kesho ndio siku yenyewe ya Watanzania kuhesabiwa. Kuna wenzetu hususan kwenye Uislamu wenye kudai kuwa watagoma kuhesabiwa; Kisa? Hakuna dodoso lenye kutaka kujua dini ya mtu. Mimi naamini walioamua suala la dini ya Mtanzania lisiingizwe kwenye sensa walifanya uamuzi wa busara na wenye hekima sana.


  Sisi ni Watanzania. Ni watu wamoja kwa asili. Na tujiulize kwanza; kwa nini tunahitaji kujihesabu. Ndio, sensa ina maana ya kujua idadi yetu kama Watanzania ili iisaidie Serikali katika kupanga mipango ya maendeleo ya nchi yetu. Mipango ya maendeleo ya nchi haibagui dini ya Mwananchi. Kama ni huduma ya maji, basi, maji hayo watakunywa Watanzania; wawe Waislamu, Wakristo, Wahindu au Wapagani. Hivyo hivyo kwa huduma nyingine muhimu za kijamii.


  Bila shaka, Sensa ya watu na makazi ni mpango madhubuti wa Serikali kwa maendeleo ya watu wake na wenye kugharimu mabilioni ya shilingi. Si busara na hekima kwa baadhi ya viongozi wa madhehebu ya dini kushiriki kuhujumu mpango huu wa Serikali kwa manufaa ya wananchi wakiwamo waumini wa dini mbali mbali na hata wasio waumini. Na kubwa zaidi hapa ni ukweli huu; kuwa nchi yetu haina dini.


  Naam, kiumbe mzito, hata kama Sensa ingeingiza kipengele cha dini, basi, wangetokea wachache wa kuhoji; iweje leo watu wakaulizwa dini zao, ama ni njama za kutaka kuwabagua na kuwakandamiza zaidi kimaendeleo Watanzania wa dini fulani au ni mbinu ya kutaka kudhibiti kuongezeka kwa idadi ya waumini wa dini fulani. Ndio, kuna ambao wangepambana kutaka kipengele cha dini kiondolewe na hata kutishia kugomea sensa.


  Naam, kiumbe mzito, na mgumu pia!


  Shime Watanzania na hususan ndugu zangu Waislamu, kesho ikifika na tuwe tayari kuhesabiwa kwa maendeleo ya nchi yetu. Kwa maendeleo yetu.
  Mungu Ibariki Afrika, Mungu Ibariki Tanzania.


  Maggid Mjengwa,
  Iringa.
  0788 111 765
  Mjengwa Blog::Habari,Picha,Matangazo
   
 2. MAVUNO

  MAVUNO JF-Expert Member

  #2
  Aug 25, 2012
  Joined: May 29, 2011
  Messages: 334
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Jitokeze wewe bana, sisi tutakuwa masjid
   
 3. Freema Agyeman

  Freema Agyeman JF-Expert Member

  #3
  Aug 25, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 3,282
  Likes Received: 1,432
  Trophy Points: 280
  Umesikia ya Wahdzabe kukataa kuhesabiwa hadi wapewe nyama ya nyani na gongo?

  Kwa vile hairuhusiwi kuua nyani, viongozi wamekubaliana kuwapa nyama ya pundamilia na gongo ili wahesabiwe. Wahadzabe ni viumbe gani?
   
 4. B

  Bangoo JF-Expert Member

  #4
  Aug 25, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 5,594
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Jk ana tabu mpaka amalize utawala wake!!
   
 5. Songoro

  Songoro JF-Expert Member

  #5
  Aug 26, 2012
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 4,136
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0
  Majid umeandika vizuri hongera,Waislam wanataka kujua mnapouliza dini za watu shuleni,vyuoni,mahakamani kazini(za serikali) mna agenda gani za siri mpaka huko iwe sawa ila kwenye sensa iwe haram? Tatizo hili swali hamlijibu mnakimbilia kusema maendeleo hayaangalii dini mbona huko tulipotaja mnauliza dini?
   
 6. Davie S.M

  Davie S.M JF-Expert Member

  #6
  Aug 26, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 720
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Si unajua kwamba huko kuna viapo,ni vile kupata taarifa sahihi pasi ubaguzi/upendeleo wowote kwa mfumo wa social services, na Hii Sensa ikumbukwe ni IDADI tu na madodoso mengine.na Serikali hawahitaj kujua dini sababu Maendeleo itakayotoa hayatolenga Udini yatalenga kila mwananchi.ikifanya ivo Kuna DINI nyiingi Tanzania zitataka kutambulika wakati Serikali Haina Tija nazo,
  Waislam waondoe dhana yao kwamba wao ndio DINI bora Kabisaa wajikite zaidi kwenye Imani yao ambao itawajenga ata wakaiona Pepo.

  Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
   
Loading...