Neno La Leo: Simba Mzee Anapokaribia Kufa.... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Neno La Leo: Simba Mzee Anapokaribia Kufa....

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by maggid, Mar 30, 2011.

 1. m

  maggid Verified User

  #1
  Mar 30, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Ndugu Zangu,


  ” HAYO malumbano ni ya kwao, sisi hatuyajui, wala hatutaki kuyajua. Tunashughulika na kutekeleza Ilani tu… maneno maneno kama hayo hayatuhusu”. Anasema John Chiligati, Katibu Mwenezi wa CCM.( NIPASHE, Jumapili, Machi 27, 2011)


  Simba anapozeeka na kukaribia kufa huanza kupoteza uwezo wa kuona, kunusa na hata kusikia. Lakini, kuna moja ambalo simba ana hakika nalo, kuwa ameacha simba watoto. Kizazi cha simba kitaendelea.


  Chiligati anasema hayajui yanayotokea ndani ya UVCCM na malumbano yanayoendelea. Hapa kuna mawili; kama ni kweli hayajui ni tatizo, na kama anayajua na kuamua kutingisha mabega na kujifanya hayaoni wala kuyasikia ni tatizo kubwa zaidi. Kwa vile, Umoja wa Vijana wa Chama ni moja ya viungo muhimu kwenye mwili wa chama.


  Maana, katika maisha haya ya kisiasa, vijana ndio nguzo na uhai wa chama chochote kiwacho. Inakuwaje basi, chama kinachozeeka kinapozungukwa na ’vijana wazee’? Uhai wa chama hicho utakuwa hatarini. Na hilo ni Neno La Leo. ( Hii ni sehemu ya makala yangu, RAIA MWEMA, leo Jumatano)  Maggid
  Iringa
  Jumatano, Machi 30, 2011
  MJENGWA - Picha, Habari & Matangazo
   
 2. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #2
  Mar 30, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  kazi ipo mpaka 2015
   
 3. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #3
  Mar 30, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  neno la leo
   
 4. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #4
  Mar 30, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  Mh.majid habari za miezi? Umeitenga Jf au mpaka siku za uchaguzi? Tunahitaji michango yako kama ilivokuwa kabla na baada ya oct.2010. Pia mkuu, simba ni nani ktk vita hii ya uvccm?chilligati?au ni msemo tu? Unajua kama mzee uyu akikusikia ataogopa maneno yako. Ccm kuna simba wakati mwindaji cdm anaingia mpaka pangoni na kuwangoa meno watoto wa simba? Cdm imemg'oa meno mtoto wa simba na ukoo wake wote. Kufikia 2015, uyu simba badala ya kuwinda na kupata mawindo ya nyama atakuwa anakula majani na kukorogewa uji,simba ni mkali lakini hana meno tena!
   
Loading...