Neno La Leo: RC Makonda Na Makolongulu..!

maggid

JF-Expert Member
Dec 3, 2006
1,084
1,246
-Haki Yako Ya Kurusha Mikono Inaishia Inapoanzia Pua Ya Mwenzako...

Ndugu zangu,

Inahusu haki. Hata mkiwa wawili chumbani, aayesinzia kwenye muda wa kulala ana haki ya kutaka utulivu.

Kama mwenzako kalala, wewe mwenye hamu ya kusikiliza muziki kwa sauti unapaswa kiungwana ukasikilizie nje ya chumba.

Na kama walio kwenye vyumba vya jirani muda huo wa kujipunzisha nao wako kwenye usingizi au kuutafuta usingizi, mwenye hamu ya kusikiliza muziki anapaswa kiungwana atoke nje kabisa ya nyumba. Aende akatafute sehemu ya kusikiliza muziki wake kwa sauti bila kuwabughuzi wanadamu wenzake, walio katika muda ambao ni haki kwao kuwa na utulivu.

Naam, haki yako ya kurusha mikono inaishia inapoanzia pua ya mwenzio.

Ukiacha kumbi za starehe na bar zenye kupiga muziki kwa sauti kubwa maeneo yenye kuishi wananchi ikiwamo watoto na wagonjwa, moja ya kero za Jiji la Dar es Salaam ni kelele za magari yenye kupita mitaani yakifanya promosheni ya bidhaa zao kwa kutangaza na kucheza muziki kwa sauti kubwa inayoumiza ngoma za masikio. Kwanini wasitumie redio na tv kutangaza. Uharibifu wa mazingira si kukata miti ovyo tu, bali ni pamoja na kupiga kelele ovyo.

Hata wavuvi wa Lindi kule Nangulukulu wakitia nanga pwani hustaarabu wa kutopiga kelele huwajia.

Sikiliza kibao hiki, lakini kama aliye jirani nawe kajipumzisha katika muda anaostahili kujipunzisha, basi, usiucheze kwa sauti.

Naam, haya hapa ni Makolongulu, kumbuka, haki yako ya kucheza na kurusha mikono inaishia kwenye pua ya mwenzako!

Sikiliza..

Maggid.
 
Mtoa mada huu wimbo wa Mbaraka hujautendea haki kabisa. Ulipaswa uuache uende mpaka pale unaposema ".. wewe uliona wapi jogoo la shamba likawika mjini .."
 
Back
Top Bottom