Na Maggid Mjengwa.
KUNA wakati, katika mwaka huu, vyombo vya habari vya dunia vilimwonyesha Rais Hamid Karzai wa Afghanstan akitoa machozi hadharani. Ni pale alipotamka kwa uchungu akielezea hali ya nchi hiyo kukosa amani; Watoto wangu watakwenda kuishi uhamishoni kwenye nchi za kigeni Akaanza kububujikwa machozi.
Rais Karzai alizungumza na kutoa machozi kutokana na kuona hali halisi ya nchi yake. Kwamba kuendelea kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe na kukosekana kwa amani kutapelekea hata watoto wake mwenyewe ( Rais) kukimbilia uhamishoni. Jambo hilo lilimuuma sana. Tuna cha kujifunza.
Kufuatia Uchaguzi Mkuu wetu uliopita na matokeo yake, sauti za Watanzania kutaka uwepo wa Katiba Mpya zimeongezeka zaidi; mijini na hata vijijini.
Matokeo ya uchaguzi wa mwaka huu yamedhihirisha jambo moja kuu ; Watanzania wanataka mabadiliko. Hii si ajenda ya chama cha siasa, ni ajenda ya Watanzania kwa ujumla wao. Vyama vya siasa vina wajibu wa kusaidia kufanikisha adhma hii.
Kwa Chama tawala, kuruhusu kuanzishwa kwa mchakato wa kupata Katiba Mpya si tendo la kuwafanyia hisani´wapinzani wa kisiasa, bali, ni wajibu wa kisiasa kwa maslahi ya nchi na kuna maslahi ya kisiasa hata kwa Chama tawala.
Idadi ya Watanzania wanaonyesha kuchoka na hali iliyopo inaongezeka. Wanataka uwepo wa misingi imara zaidi ya demokrasia. Wanataka haki zaidi za kidemokrasia na hivyo kuweza kupiga hatua zaidi za maendeleo ya mtu mmoja mmoja, kikundi cha watu na nchi yao kwa ujumla.
Ni dhahiri, kilio cha kutaka Katiba Mpya kinazidi kusikika. Hata kabla ya Uchaguzi Mkuu, tulimsikia Jaji Mkuu Augustino Ramadhani akitamka; kuwa Katiba ni Nyaraka inayoishi ( A living document ) Kwamba inaweza kubadilika ili kukidhi mahitaji ya wakati husika. Na juzi hapa tumemsikia Jaji Manento pia, naye amezungumzia Katiba Mpya, kwamba wakati umefika. Na hilo ni Neno La Leo.
( Hii ni sehemu ya makala yangu ya Raia Mwema niliyotuma wiki hii)
Maggid,
Iringa.
Novemba 23, 2010
mjengwa