Neno La Leo: Rais Wa Nchi Anapotoa Machozi Hadharani!


maggid

Verified User
Joined
Dec 3, 2006
Messages
1,084
Likes
396
Points
180

maggid

Verified User
Joined Dec 3, 2006
1,084 396 180
Na Maggid Mjengwa.


KUNA wakati, katika mwaka huu, vyombo vya habari vya dunia vilimwonyesha Rais Hamid Karzai wa Afghanstan akitoa machozi hadharani. Ni pale alipotamka kwa uchungu akielezea hali ya nchi hiyo kukosa amani; “ Watoto wangu watakwenda kuishi uhamishoni kwenye nchi za kigeni…” Akaanza kububujikwa machozi.


Rais Karzai alizungumza na kutoa machozi kutokana na kuona hali halisi ya nchi yake. Kwamba kuendelea kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe na kukosekana kwa amani kutapelekea hata watoto wake mwenyewe ( Rais) kukimbilia uhamishoni. Jambo hilo lilimuuma sana. Tuna cha kujifunza.
Kufuatia Uchaguzi Mkuu wetu uliopita na matokeo yake, sauti za Watanzania kutaka uwepo wa Katiba Mpya zimeongezeka zaidi; mijini na hata vijijini.
Matokeo ya uchaguzi wa mwaka huu yamedhihirisha jambo moja kuu ; Watanzania wanataka mabadiliko. Hii si ajenda ya chama cha siasa, ni ajenda ya Watanzania kwa ujumla wao. Vyama vya siasa vina wajibu wa kusaidia kufanikisha adhma hii.


Kwa Chama tawala, kuruhusu kuanzishwa kwa mchakato wa kupata Katiba Mpya si tendo la kuwafanyia ’hisani´wapinzani wa kisiasa, bali, ni wajibu wa kisiasa kwa maslahi ya nchi na kuna maslahi ya kisiasa hata kwa Chama tawala.
Idadi ya Watanzania wanaonyesha kuchoka na hali iliyopo inaongezeka. Wanataka uwepo wa misingi imara zaidi ya demokrasia. Wanataka haki zaidi za kidemokrasia na hivyo kuweza kupiga hatua zaidi za maendeleo ya mtu mmoja mmoja, kikundi cha watu na nchi yao kwa ujumla.


Ni dhahiri, kilio cha kutaka Katiba Mpya kinazidi kusikika. Hata kabla ya Uchaguzi Mkuu, tulimsikia Jaji Mkuu Augustino Ramadhani akitamka; kuwa Katiba ni Nyaraka inayoishi ( A living document ) Kwamba inaweza kubadilika ili kukidhi mahitaji ya wakati husika. Na juzi hapa tumemsikia Jaji Manento pia, naye amezungumzia Katiba Mpya, kwamba wakati umefika. Na hilo ni Neno La Leo.


( Hii ni sehemu ya makala yangu ya Raia Mwema niliyotuma wiki hii)Maggid,


Iringa.
Novemba 23, 2010


mjengwa
 

Nicky82

JF-Expert Member
Joined
Mar 14, 2009
Messages
939
Likes
1
Points
35

Nicky82

JF-Expert Member
Joined Mar 14, 2009
939 1 35
Well said Majjid.
Endelea kutumia kalamu yako kwa kusambaza habari hizi zenye tija kwa future ya nchi yetu. Maana hakika hatuwezi kuwa na katiba ya kidkteta inayobariki hata wizi wakati wa uchaguzi. Eti mtu akishatangazwa na tume hata ile aliyoichagua yeye hakuna wa kutengua maamuzi, huu ni ubakaji wa demokrasia.
 

JoJiPoJi

JF-Expert Member
Joined
Aug 8, 2009
Messages
2,645
Likes
1,918
Points
280

JoJiPoJi

JF-Expert Member
Joined Aug 8, 2009
2,645 1,918 280
Maggid naona ulikuwa unaogopa uchaguzi ila kwa sasa umerudi sehemu sahihi, hongera sana kwa ujumbe mzuri kwa watawala wa tanzania na afrika kwa ujumla
 

Mo-TOWN

JF-Expert Member
Joined
Oct 11, 2010
Messages
1,717
Likes
216
Points
160

Mo-TOWN

JF-Expert Member
Joined Oct 11, 2010
1,717 216 160
It is happening in TZ only. This is the time to overhaul the constitution and remove all nonsense and undemocratic clauses.
 

satellite

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2010
Messages
613
Likes
21
Points
35

satellite

JF-Expert Member
Joined Nov 18, 2010
613 21 35
Inamua sana pale unaibiwa hata mkeo then sheria inasema huyu kashamua tena hivyo huna haki ya kudai,kudadeki mi ntaua mtu hapo sitaelewa kama hiyo sheria inanibana wala nini,hv huyo aliyetunga hii sheria ya uchaguzi rais akishatangazwa huwezi kupiga zipo kichwani zinafanya kazi kweli au alikua amelewa au alikua amewekewa mtutu wa bunduki matakoni?mwenye akili timamu hawezi fanya upuuzi kama huo
 
Joined
Nov 2, 2010
Messages
83
Likes
1
Points
0

wikama

Member
Joined Nov 2, 2010
83 1 0
hii ni nzuri kama Kikwete ana akili atalifanyia kazi hili ili kuwatendea haki watanzania walio na hamu ya kutaka kujua hatima ya maisha yao, nchi hii ni yetu sote lakini wanaofaidi ni wachache utasikia Rostam, Lowasa, Chenge, na wengine kwani ni wao tu na wao wana utajiri ni kutoka kwenye mfuko wa serikali na wanaendelea kunyanyasa. tunataka mabadiliko tumechoka. pia katiba ibadilishwe kwa kupata maoni ya wananchi kama walivyofanya kuingia kwenye vyama vingi.
 

Nungunungu

JF-Expert Member
Joined
Feb 13, 2007
Messages
312
Likes
0
Points
0

Nungunungu

JF-Expert Member
Joined Feb 13, 2007
312 0 0
Mjengwa aliyasema hayo hata kabla ya Uchaguzi

"Nasi kama taifa, tuanze sasa kuangalia uwezekano wa kuanzisha mchakato wa kuandika Katiba mpya. Zawadi kubwa kwetu Watanzania tukaposherehekea miaka hamsini ya uhuru wetu iwe ni kwa viongozi wetu kutuanzishia mchakato huo. Na huo ndio utakuwa urithi muhimu na wa maana kubwa tutakaoviachia vizazi vijavyo....."

"Zawadi nono mnayoweza kutupa ni Katiba mpya"

Zawadi nono mnayoweza kutupa ni Katiba mpya

Tatizo la Chadema mamboleo hamsomi ila kinachoishabikia Chadema. Aibu!
 

kiraia

JF Gold Member
Joined
Nov 20, 2007
Messages
1,626
Likes
308
Points
180

kiraia

JF Gold Member
Joined Nov 20, 2007
1,626 308 180
Kaka Maggid nini kimekutokea au kuna mahali hao Jamaa wanaopinga katiba Mpya wamekubania? Sikutegemea kama ungerudi kundini kutetea haki za watanzania, karibu na hongera kwa makala nzuri nitaisoma vizuri kesho kwenye Raia mwema kama ulivyoahidi.
 

Konakali

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2009
Messages
1,506
Likes
71
Points
145

Konakali

JF-Expert Member
Joined Dec 15, 2009
1,506 71 145
Ni kwa sababu Nyerere alikwishatambua mapungufu ya katiba yetu, na akasema kuwa tunapaswa kumuomba Mungu sana tusije tukampata raisi kichaa...! Maana raisi tunayemchagua sisi wananchi atuongoze kwa muda fulani, lakini kwa mujibu wa katiba anakuwa na mamlaka kwenye nchi kuliko hata mamlaka ya baba nyumbani...!
 

Forum statistics

Threads 1,204,087
Members 457,130
Posts 28,140,823