Neno La Leo: Pravda Na Izvestia- Ukweli Na Habari! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Neno La Leo: Pravda Na Izvestia- Ukweli Na Habari!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by maggid, May 3, 2012.

 1. m

  maggid Verified User

  #1
  May 3, 2012
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Ndugu zangu,

  Leo ni Siku ya Uhuru wa Habari duniani. Ni siku inayotuhusu sote.


  Enzi za Ukomunisti kwenye Soviet Union kulikuwa na magazeti mawili makubwa; Pravda na Izvestia, ikiwa na maana ya Ukweli na Habari.


  Na Urusi kulikuwa na utani mitaani; kwamba kwenye Pravda hakukuwa na ukweli wowote ulioandikwa, na kwenye Izvestia hakukuwa na habari!


  Na kwa kiasi kikubwa watu wa mitaani hawakutania. Huo ndio ulikuwa ukweli wenyewe. Chama cha Kikomunisti kiliendesha zaidi propaganda. Na tafsiri sahihi ya propaganda ni uongo. Na propaganda maana yake haswa ni uongo unaorudiwa rudiwa sana hadi pale jamii inapoamini kuwa ni ukweli. Kule Soviet Union, kitengo cha propaganda kwenye Chama Cha Kikomunisti kilikuwa na kazi moja kubwa; kusambaza uongo.


  Na anayeajiriwa kufanya kazi hapo lazima moja ya sifa zake ziwe ni umahiri wa kusema uongo. Kwamba hata kama kinachoonekana na kila mmoja kuwa ni jiwe, mtu wa propaganda anaweza kusema hilo si jiwe, ni mchanga uliolundikana na kufanya kichuguu. Na atarudia rudia kusema hilo mpaka pale wengine mtakapoanza kuamini kuwa mnaliliona mbele yenu si jiwe ni ' mchanga uliolundikana'!


  Na ukweli una sifa moja kubwa, kuwa hata ukifichwa chini ya uvungu wa kitanda kwa miaka hamsini ( Nusu karne) , iko siku, utatoka na kutembea hadharani wenyewe. Hautasubiri kuvalishwa viatu.


  Yes, get up stand up!


  You can fool some people sometimes. But you can't fool all the people all the time- Bob Marley.


  ( Pichani nikiwa na wapambanaji; John Bwire na Kyaruzi, Sinza Kijiweni, enzi hizo nikiandikia Rai)


  Maggid Mjengwa,
  Msamvu, Moro
  0788 111 765
  Mjengwa Blog::Habari,Picha,Matangazo

   
 2. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #2
  May 3, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Shukrani. Kumbe Kyaruzi yule aliyekuwa Habari na baadaye kwende TSN naye ni mpiganaji au alikuwa mpiganaji?
   
 3. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #3
  May 3, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Mapendekezo ya kamati ya hesabu za serikali za mitaa(LART) yameanza kutekelezwa kwa watuhumiwa kukamatwa katika halmashauri ya wilaya ya Kishapu.Naendelea kufuatilia kwa kina zaidi ili niwalete update ni akina nani,Kwasasa nipo Polisi kujua ni vitengo vipi.Muda si mrefu nitawajuza
   
Loading...