Neno La Leo; Pavumapo Palile, Si Kazi Kudamirika! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Neno La Leo; Pavumapo Palile, Si Kazi Kudamirika!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by maggid, Jul 29, 2011.

 1. m

  maggid Verified User

  #1
  Jul 29, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Ndugu zangu,


  Kuna tuliopata bahati ya kuyakumbuka tuliosimuliwa zamani. Ni mambo yenye elimu kubwa inayofaa maishani.


  Naam, palipata kutokea nchi kwenye bahari ya giza. Nchi hiyo ilikuwa ikitawaliwa na mfalme maarufu sana. Aliitwa Mfalme Ihsani. Mfalme alikuwa mtu mwema. Alikaa vema na raia wake. Alikuwa ni mwingi wa hekima na busara.


  Mara zote, Mfalme alikaa akitafakari namna ya kuwapatia raia wake mambo mema yenye kuwafaa. Akatafuta wataalam wa kuisukuma nchi mbele kimaendeleo. Akawaita waalimu, akajenga mashule watu wasome; mijini na vijijini.Naam. Mfalme alifahamu, kuwa maendeleo hayawezi kupatikana bila elimu.


  Nchi ikawa na raia wenye maradhi mengi. Mfalme akatambua, kuwa nchi haiwezi kujengwa na wagonjwa. Ndio, duniani hakuna shamba la mgonjwa. Mfalme akatia jitihada za kusomesha matabibu. Kisha akajenga vituo vya tiba. Maradhi yakaanza kutoweka. Raia wakawa wenye wingi wa siha.


  Nuru ikamulika katika nchi ile. Maendeleo yakaanza kuonekana. Sifa zikatapakaa, na mfalme akasifiwa kwa jitihada , hekima na busara zake katika uongozi. Lakini, Mfalme Ihsani hakutosheka na mafanikio hayo. Akatia jitihada zaidi. Akaumiza kichwa kufikiri shida za watu wake.


  Akabaini, kuwa raia wake walipata tabu sana kufika shuleni na kwenye vituo vya tiba. Mfalme akaanzisha mpango wa ujenzi wa barabara, mijini na vijijini. Raia wakapata ajira na ujira pia katika kufanya kazi ya ujenzi wa barabara.


  Watu wa dunia wakasikia sifa za nchi ya Mfalme Ihsani. Wakatamani kuishi katika nchi hiyo. Wengi wakahama nchi zao kuhamia nchi ya Mfalme Ihsani. Watu hao walikuja wakiwa na vipaji mbalimbali vya kazi za ufundi na mengineyo. Wengine wakafanya kazi za biashara kwa kufungua maduka. Majengo zaidi yakahitajika na mahitaji mengine ya kihuduma kwa raia. Watu wa nchi ya Mfalme Ihsani wakaanza kupata maisha bora.


  Aaa! Fitina ikaanza kuingia. Ni fitina zilizosababishwa na watu wenyewe wa nchi ya Mfalme Ihsani. Chuki ikaingia, hivyo basi mifarakano na makundi. Njia ya maendeleo ikawa imewekwa vizingiti vya mawe makubwa. Naam, nyota mbaya ikawa imeanguka katika nchi ile kwenye bahari ya giza.


  Kuna waliongiwa shauku ya kukamata mbingu kwa mkono wakitarajia makubwa kwa njia haramu. Kadri siku zilivyokwenda, basi, chuki, choyo, husuda na fitina vilitamalaki. Na kubwa zaidi kukawapo na ubaguzi wa kimakundi. Fujo na zogo la kijamii likatawala. Nchi ikaanza kuangamia.


  Na nchi yetu Tanzania, kama ilivyo kwa nchi ya Mfalme Ihsani, nayo imeanza kuingiwa na sumu ya ubaguzi wa kisiasa , kidini na hata kikabila. Na yote hayo yanasababishwa na chuki, choyo, husuda na fitina. Yoye hayo ni matendo ya kifisadi. Ni uoza wa kimaadili- A moral decay- ni rushwa.


  Pavumapo Palile, Si Kazi Kudamirika! Na hilo ni Neno La Leo.


  Maggid


  Sweden, Ijumaa, Julai 29, 2011
  MJENGWA - Picha, Habari & Matangazo
   
 2. Rufiji

  Rufiji JF-Expert Member

  #2
  Jul 29, 2011
  Joined: Jun 18, 2006
  Messages: 1,710
  Likes Received: 161
  Trophy Points: 160
  Maggid,

  Tafadhali acha kufananisha kunguru na meza. Tanzania haifanani na nchi ya mfalme Ihsani uliyotaja hapo juu, kwani mfame Ihsani wetu hajatufanyia kitu chochote zaidi ya kutuletea giza. Tukirudi kwenye article yako, nashindwa kuelewa ni vigezo ulivyotumia kusema ya kuwa ubaguzi wa kisiasa umeletwa na chuki za dini, kikabila. Hii ni moja kati ya kauli ya kitoto niliyowahi kusikia katika maisha yangu! Ubaguzi wa siasa unaozungumzia, kama upo, basi utakuwa ni matokeo ya watu kukandamizwa kwa muda mrefu na watawala.

  Mwandishi yeyote makini angejiuliza ni nini kilichopekea , watu toka kila kona ya Tanzania na wa dini mbali mbali, kumshangilia kwa nguvu Kikwete alipogombea kwa mara ya kwanza? Kama watu hawa ni wadini na wakabila, mbona hawakumpinga mwaka 2005? Maggid, waandishi kama nyie ndio mnaorudisha taifa letu nyuma, kwa kutoa majibu au maoni mepesi kwenye ishu muhimu zinazogusa mstakabali wa taifa letu.
   
 3. Sooth

  Sooth JF-Expert Member

  #3
  Jul 29, 2011
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 3,773
  Likes Received: 4,496
  Trophy Points: 280
  ..Look who talking!
   
 4. Mkuu wa chuo

  Mkuu wa chuo JF-Expert Member

  #4
  Jul 29, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,255
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  kwani ni nani muasisi wa kubaguana kwa makundi, kama unataka jibu, hebu angalia ule mtandao wa uliomwingiza madarakani mkwerè, hata ndani ya magamba kwenyewe kuna kubaguana kwa makundi. Kila mmoja ana kundi lake!
   
 5. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #5
  Jul 29, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  hii afadhari ya mfalme Ihsani maana rais wetu ndio basi kabisa hajui hatamatatizo ya nchi yake bali anachojua ni natural things amabavyo hawezi kuvirekebisha kama kuleta mvua hajui nchi zilizoendelea hawategemei mvua inyeshe isinyeshe wao ni mdundo tu ukipungukiwa ufahamu nitatizo kubwa sana afadhari na mfalme Ihsani alikuwa namawazo ya kufikiria nini afanye na kwa wakati gani.
   
 6. SILENT ACtOR

  SILENT ACtOR JF-Expert Member

  #6
  Jul 29, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 618
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 45
  Ihsan story does not correlate with the case of tz. Miaka yote uliyokaa ktk uandishi unashindwa hata kuchagua mfano bora wa kufundishia hadhira yako? Shame on you Maggid! Bora ungetumia mfano wa mfalme ****.
   
 7. Mentor

  Mentor JF-Expert Member

  #7
  Jul 29, 2011
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 18,714
  Likes Received: 8,266
  Trophy Points: 280
  What happened to mraba wa Maggid...those days you used to write things I loved to read!
  Sijui kwa kweli...
   
 8. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #8
  Jul 29, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,768
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  yaani wewe ndiye maggid watu walikuwa wanajaribu kukulinganisha na mzee mwanakijiji?
  aisee kauwezo kako kumbe ni kadogo hivyo?
  nafikiri huna haja ya kujadiliwa wala kulinganishwa na great thinkers
   
 9. Wayne

  Wayne JF-Expert Member

  #9
  Jul 29, 2011
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 663
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Yeah, tupo pamoja mkulu
   
Loading...