Neno La Leo: Nyamongo Ni Huzuni Yetu, Ni Aibu Yetu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Neno La Leo: Nyamongo Ni Huzuni Yetu, Ni Aibu Yetu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by maggid, May 26, 2011.

 1. m

  maggid Verified User

  #1
  May 26, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Ndugu zangu,


  PICHA ya jeneza lililotelekezwa barabarani imeongea zaidi ya maneno milioni moja. Kwa Watanzania, imetutia simanzi, imetutoa machozi. Ndani ya jeneza hilo pichani kuna mwili wa marehemu Emmanuel Magige iliyotelekezwa kijijini Nyakunguru, Tarime. Emmanuel Magige hakuwa jambazi. Ni Mtanzania mwenzetu mwanakijiji wa kawaida. Aliyetelekezwa si Magige tu, kuna maiti nyingine tatu.


  Mauaji ya Nyamongo yaliyofanywa na polisi wetu ni huzuni kubwa kwetu, ni aibu yetu pia, kama taifa. Maana, wauaji hawakutoka nje ya mipaka yetu, na bado wamo ndani ya mipaka yetu.Kupunguza aibu hii ni kwa wote waliohusika kuchukuliwa hatua za kisheria.  Maana, mauaji ya Nyamonngo yanatukumbusha Arusha, yanatukumbusha Mbarali. Yanatutia hofu mpya pia. Hatujui kesho yatafanyika wapi.


  Jeneza la Emmanuel Magige lililotelekezwa barabarani ni kielelezo cha mahali tulipofikia. Kuna chuki inajengeka. Na katika tofauti zetu hizi za kiitikadi tusifike mahali tukashindwa kuongea kama Watanzania. Tusifike mahali tukachochea machafuko makubwa ya kijamii. Wanasiasa wana jukumu la kutanguliza busara katika kila maamuzi wayafanyao.


  Na tuyalaani vikali mauaji ya Nyamongo. Tusipoyalaani nasi tutalaaniwa. Na Mungu huyu anatupenda Watanzania, kuna tunachoonyeshwa. Na tuzisome kwa makini alama hizi za nyakati. Na Miungu yetu, mizimu ya mababu zetu, inatupenda pia. Walikolala mababu zetu, nao wanaturajia tulaani kitendo hiki, maana, hata katika mila na desturi zetu, Waafrika hatutelekezi maiti zetu. Tunazizika.


  Ndio, kwa jadi yetu, Waafrika tunahesabu wafu wetu, tunawatambua kwa majina, tunawaombea kwa imani zetu. Ndio, tunawazika wafu wetu. Kwa heshima zote.

  Kwa desturi, Watanzania hatupendi kuwa katika hali ya kudharauliwa na kutothaminiwa kwa utu wetu tukiwa hai. Na kamwe, tusikubali Watanzania wenzetu wasithaminiwe wakiwa katika hali ya umauti. Na hilo ni Neno la Leo.


  Maggid
  Iringa,
  Alhamisi, Mei 26, 2011
  MJENGWA - Picha, Habari & Matangazo


   
 2. tanga kwetu

  tanga kwetu JF-Expert Member

  #2
  May 26, 2011
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 2,163
  Likes Received: 1,122
  Trophy Points: 280
  Kwa mwenye upeo mfupi wa fikra, anaweza kuona hili suala kama dogo, hata wanaobeza huu msiba wa Tarime nina imani hawajapata wasaa wa kutafakari. Najaribu kujiuliza, ndugu yangu apigwe risasi wakati anawakimbia Polisi dhalimu, then wamuite jambazi, then wanibembeleze kumzika nami nikakataa, nikaamua nimuhifadhi mortuary hadi uchunguzi wa kisheria na kitabibu ukamilike-vikakamilika.

  Then wauwaji wa ndugu yangu waje kupora maiti ya ndugu yangu mortuary na kisha mimi mfiwa nipigwe virungu na kuswekwa lupango, then waitelekeze maiti ya ndugu yangu huyo barabarani/vichakani? Naomba uchukue nafasi yangu, naomba ubebe huzuni, ghadhabu na hasira zangu juu ya hawa wauwaji, naomba uvae viatu vyangu.

  Nipe sababu 3 tu, kwa nini nisi-revenge juu ya damu ya ndugu yangu huyu? Ndugu yangu alijumuika na wanakijiji wenzake kwenda kudai haki za kijiji chao mbele ya 'wawekezaji' wanaolindwa na dola instead wanaambiwa majambazi?

  Nipe sababu 3 tu, kwa nini nisi-revenge juu ya damu ya ndugu yangu huyu? Ni hadi lini 'wawekezaji' watatetewa na dola in expense of our lives? Enyi tulio mbali na Tarime, Mbalali na arusha mjini, tuacheni kubeza yaliyowapata hawa watanganyika wenzetu?

  Sie tunatofauti gani ya uthamani kuliko wa Tarime, Mbarari na Arusha mjini hata tujione salama sana? Una uhakika gani na usalama wako dhidi ya risasi/mauaji ya dola tena pale unapodai haki yako ambayo haitekelezwi?

  Uwoga wetu ndio nguvu yao.
   
 3. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #3
  May 26, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,266
  Trophy Points: 280
  Yangekuwa majeneza ya waislamu ungepata majibu yao kesho baada ya swala ya ijumaa kwa takbir na maandamano ya nguvu kupinga dhulma.
   
 4. mfereji maringo

  mfereji maringo JF-Expert Member

  #4
  May 26, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 1,003
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  "wal kiswaswa haku" ktk uislam kulipa kisasi ni haki, kwahiyo pale wangeandamana kuwafata wauwaji hadi risasi ya mwisho ingesikika
   
 5. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #5
  May 26, 2011
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,458
  Likes Received: 1,331
  Trophy Points: 280
  Hii ni aibu sana kwa taifa hili maskini, hadi leo bado serikali yetu haijachukua hatua angalau za kutufanya tuamini ipo kwa ajili ya wananchi licha haipo hivyo
   
 6. Shinto

  Shinto JF-Expert Member

  #6
  May 26, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 1,781
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Maggid
  Nilikuwa nakuheshimu sana ndugu yangu.
  Nilifuatilia kwa makini makala zako za Mamwindi na Kleruu.

  Nillikuwa nakuona mojawapo ya uncorrupted minds katika kada ya uandishi habari.
  Ila kwa makala zako za karibuni hususani hii, nimeondoa kila joho nililokuvika!

  Wakati siungi mkono hata kidogo mauji ya raia wasio na hatia popote pale duniani, nashangazwa na wewe kuchukua scene moja kwenye movie yote ikawa ndio issue kwako.

  Habari yako ni one-sided, hukutaka kutuambia mazingira yaliyopelekea hilo jeneza kuachwa barabarani, na wala hukutuambia role ya uchochezi ya wana MAGWANDA wakiongozwa na LISSU.

  Ki msingi makala yako ni shallow sana, unaimba nyimbo zile zile ziliziojaa humu JF za MAGWANDA!
   
 7. s

  sawabho JF-Expert Member

  #7
  May 26, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,504
  Likes Received: 946
  Trophy Points: 280
  Nakuunga mkono, mwenzako akinyolewa wewe tia maji. Yanayotokea yaliyotokea Tarime ni mfululizo wa matukio amabyo hakun mwenye uhakika yatatokewa tena wapi na lini.
   
 8. Wa Ndima

  Wa Ndima JF-Expert Member

  #8
  May 26, 2011
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 1,512
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Ningependa Waislamu waandamane kupinga jambo hili kesho baada ya swala ya ijumaa na inshaallah Mwenzezi Mungu atawaafu!
   
 9. Kinyungu

  Kinyungu JF-Expert Member

  #9
  May 26, 2011
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 4,380
  Likes Received: 3,339
  Trophy Points: 280
  Kaka Majig Nina hasira acha tu.
   
 10. Fred Katulanda

  Fred Katulanda Verified User

  #10
  May 26, 2011
  Joined: Apr 1, 2011
  Messages: 229
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Jeneza likiwa limefunikwa na majani baada ya kukaa saa kadhaa huku likipigwa na jua
  100_0034.JPG
   
 11. Mosachaoghoko

  Mosachaoghoko Senior Member

  #11
  May 26, 2011
  Joined: Apr 19, 2011
  Messages: 137
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  We must payback on this hata kama ni kwa gharama gani ipo siku
   
 12. Tangawizi

  Tangawizi JF-Expert Member

  #12
  May 26, 2011
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 2,835
  Likes Received: 927
  Trophy Points: 280
  Hivi polisi nchini Tanzania imeundwa na watu wasio makini, wenye uwezo mdogo wa kutumia akili zao kujua athari ya kutumia vibaya dhamana yao waliopewa?
  Yote anayosema Maggid yana ukweli mtupu. Tulipo sasa polisi imejitwika jukumu la kuhakikisha hakuna sauti nyingine tofauti na ile wanayoitaka wao ikisikika. Kwa Tanzania ya leo ilivyo, kama hawatabadili mbinu za kiutendaji, wajiandae kumwaga damu za watu wengi zaidi maana mabadiliko ndiyo hayo yameanza kuchukua sura yake, wapende wasipende.
  Nafikiri, imefika mahala sasa warudi kwenye drawing board na kujitafiti vizuri kama wanachofanya ni kitu sahihi
   
 13. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #13
  May 26, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  mKUU LEO UMWAMUA UWE MKWELI! TANZANIA KWANZA!
   
 14. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #14
  May 26, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,224
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  umesema mengi mazuri yanayofaa kwa wakati huu, umesahau moja muhimu: tukumbushane watanzania tukumbuke kutii amri za mamlaka zetu, tuache kuvamia mali za watu, tujifunze kutafuta rzki kwa njia halali+ la sivyo akina magige watakuwa wengi hata kabla jogoo hajawika.
   
 15. Sooth

  Sooth JF-Expert Member

  #15
  May 26, 2011
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 3,773
  Likes Received: 4,494
  Trophy Points: 280
  Taasisi zetu haziko huru. Polisi hawawezi kufanya kazi zao kwa weledi kama wanaingiliwa na wanasiasa ktk maamuzi ya kazi zao. Ni rahisi kulaumu polisi kwa tukio la nyamongo, lakini ukitafakari kwa undani utagundua kuwa polisi hawawezi kufanya walichofanya (kutelekeza majeneza barabarani) bila kupata maagizo toka kwa wanasiasa. Naamini uamuzi wa kufuta kibali cha kufanya maziko ya pamoja, haukuwa wa askari yeyote (hata IGP asingeweza kutoa uamuzi huo).
   
 16. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #16
  May 26, 2011
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,502
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Majjid,

  Hilo wala usiwe na wasiwasi. Nina imani kuwa kama siyo mwaka 2016 basi ni mwaka 2021, kuna watu watapanda kizimbani na kuhukumiwa kunyongwa kwa haya maovu wayafanyayo.

  Mkuu wa Polisi wa Tarime nina imani anaweka kumbukumbu ya amri zote anazopewa kutoka huko majuu maana vinginevyo, ni yeye pekee atakuja kuhukumiwa kunyongwa.

  Waziri wa mambo ya ndani na Mkuu wa Jeshi la Polisi, hawa nao ni lazima siku moja wapande kizimbani. Haiwezekani watu wanakufa ovyo ovyo mara kwa mara na wao wanatoa majibu mepesimepesi.......

  Kuna watu hapa naona wanafurahia sana hayo mauwaji, sawa tu acha waendelee kufurahi na ninashukuru watu hawawajibu. Ila siku hao Mabwana zao watapanda kizimbani na kuhumiwa na umma, ndiyo watakuja kulia na kusaga meno.

  YANA MWISHO HAYA. Mungu Ibariki Tanzania.
   
 17. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #17
  May 26, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  mkuu hawanaga akili hawa jamaa..IGP ndo linaongea ka bwabwa hivi yaani ananichefua huyu mzee mpaka basi...
   
 18. A

  ADAMSON Senior Member

  #18
  May 26, 2011
  Joined: May 23, 2011
  Messages: 126
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mungu awape pumziko la milele marehemu wote waliopoteza maisha yao kule nyamongo,lakini Kisasi ni juu Ya Mungu tuwe na subira kwani saa ya ukombozi imewadia
   
Loading...