Neno La Leo: Ng'ombe Kipofu Na Ng'ombe Aliyevunjika Mguu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Neno La Leo: Ng'ombe Kipofu Na Ng'ombe Aliyevunjika Mguu!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by maggid, Oct 13, 2010.

 1. m

  maggid Verified User

  #1
  Oct 13, 2010
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Ndugu zangu,

  Wahehe wana msemo; Isenga imbofu na isenga indenyeefu.

  Kwamba ng'ombe kipofu ni sawa tu na ng'ombe aliyevunjika mguu, wote watakufa njaa. Ng'ombe kipofu hawezi kuyaona majani, na yule aliyevunjika mguu naye hawezi kujikokota kwenda kutafuta nyasi za kula.

  Tunavyoenenda kama jamii wakati mwingine ni sawa na ng'ombe kipofu na yule aliyevunjika mguu. Unaweza kuliona hilo nyumbani kwako, katika ukoo wako na hata mahala pako pa kazi.

  Leo kuna wanaotafuta visingizio vya kuingia vitani. Kuna wanaodai wanapigana kuwatetea wanyonge walio gizani. Walio gizani nao wameanza kuona katika giza hilo hilo, maana wamekuwa gizani kwa muda mrefu.

  Wameshtuka. Wanahoji mantiki ya vita vinavyopiganwa kwa niaba yao. Na walioamua kuingia vitani nao wanaonekana kutojiandaa vema na vita hivyo, wanaelekea kushindwa, maana wanapigana vita vya kinafiki. Na kamwe usiingie kwenye vita kama hujajiandaa.

  Mwingine atasema; vita vingine havina budi kupiganwa hata kama hujajiandaa kupigana na kushinda. Hapana, huendi vitani ili mradi tu unakwenda vitani , kama vile unakwenda harusini. Vita si lelemama.
  Katika dunia hii inasemwa; chagua vita vyako. Haina maana uchague vita kama unachagua mashati ya mitumba Kariakoo. Ina maana kubwa. Pima kwanza, soma alama za nyakati. Chagua vita inayoshindika, iliyo ya muhimu kupiganwa na unayokuwa na hakika ya kuwa umejiandaa vema kulipa gharama ya ushindi. Kwamba unachokipigania si cha kinafiki.

  Angalia kwanza kwenye kabati lako, kabla hujaanza kutangaza kwa watu, kuwa kabati la jirani yako lina mzoga unaonuka, huenda nawe unao, umeanza kutoa harufu, lakini unahisi tu harufu ya mzoga wa jirani yako!

  Wengi wetu tumekutana na hali ya kuwaona jogoo wawili wakipambana. Kawaida ya mpambano wa majogoo wawili ni kuvutia watazamaji. Na kila mtazamaji huwa na hulka ya kuchagua jogoo wake wa kumshangilia; kama ni jogoo mweusi na mwekundu, basi, kutakuwa na mashabiki wa jogoo mweusi na wale wa mwekundu. Yahitaji ujasiri kuamua kuwa katikati, kutochagua jogoo wa kumshabikia.

  Na hutokea, kwa yule ambaye jogoo wake ameshindwa pambano, basi, atatoka mahali hapo kwa masikitiko, akiwa na unyonge, kisa? Jogoo wake kashindwa! Ni hulka ya mwanadamu. Yahitaji ujasiri kuamua kuwa katikati, kutochagua upande. Kutochagua jogoo wa kumshabikia. Wapo wanadamu wenye ujasiri huo. Pambano linapoendelea au linapomalizika, basi, huweza kutoa tathmini isiyoegemea upande mmoja.

  Ndio, tunapaswa pia kutumia bongo zetu katika kutoa hukumu, na si kuongozwa na mapenzi ya moyoni tu. Hivyo ndivyo wafanyavyo mahakimu na majaji wanapoamua mashauri mahakamani. Usiishie tu kumlaani jogoo mwekundu anayeonekana kuwa na maumbile makubwa kwa kumtwanga jogoo wako mweusi mwenye maumbile madogo. Ukiumiza kichwa, unaweza kubaini , kuwa jogoo mwekundu alikuwa na sababu na haki za kumtwanga jogoo wako mweusi. Unatakiwa kuwa na ujasiri wa kuyaangalia mapungufu ya jogoo wako mweusi. Si wengi wenye kutaka kuifanya kazi hii ya kuumiza vichwa, kutafakari mapungufu yao na yale ya wanaowashabikia.

  Naam. Maisha ni mapambano, kuna kushinda na kushindwa. Ushindi una gharama. Mwanadamu jiandae na gharama ya ushindi. Ushindi waweza kuwa ghali mno. Unaweza kupambana ukashinda, lakini gharama ya ushindi yaweza kuwa jamaa na marafiki wa wote uliowashinda watageuka kuwa maadui zako, yawezekana
  watakuwa maadui kwako kwa muda mrefu tu. Watakukasirikia, watafanya yote nawe upate maumivu.

  Hivyo, mwanadamu usifikiri tu gharama ya kushindwa, fikiri pia gharama ya ushindi. Na wakati mwingine, ni gharama inayostahili kulipwa. Franklin Roosevelt alikuwa Rais wa zamani wa Marekani. Alifahamu faida na hasara za kuwa na maadui. Waliompinga katika sera zake za kiuchumi aliwaita " Watiifu wa Kiuchumi" Na akasema; wamejiunga kwa pamoja kunichukia na nakaribisha chuki zao kwangu!

  Kama unapigana vita ya muhimu, kama vita hivyo vyaweza vikawa vya kushinda (winnable). Na kwamba umejiandaa kulipa gharama ya chuki ya muda mrefu ya utakaowashinda, basi, ingia vitani, na kama la, tafuta suluhu au rudisha majeshi nyuma kimpangilio ( tactical retreat).

  Swali ni hili; utafikiaje uamuzi wa ama kuingia vitani au la?

  Miaka mingi iliyopita alitokea Mfalme wa Epilus aliyeitwa Pyrrhic. Mfalme huyu aliamua kuingia vitani kulikabili jeshi kubwa na lenye nguvu nyingi, ni jeshi la Warumi. Lakini kabla ya Mfalme kuingia baharini na vikosi vyake kuitafuta Italia ya Warumi, msaidizi wake wa karibu, Cineas, aliomba mazungumzo ya faragha na Mfalme. Alitaka kumwuliza maswali na kumshauri.

  Cineas alimtamkia Mfalme; " E bwana Mfalme, Warumi wanasadikika kuwa na jeshi kubwa , lenye nguvu na lenye mashujaa wengi. Ndio maana wameteka nchi nyingi. Je, Mungu akitusaidia, tukaja kuwashinda Warumi,
  tutafanya nini na ushindi wetu? Mfalme akajibu: " Mbona hilo ni swali jepesi sana. Mara ile tukiwashinda Warumi, hakutatokea jeshi kutoka mji wowote wa Italia litakaloweza kupambana nasi."

  Cineas alitulia kidogo, kisha akamwuliza Mfalme: " Tukishaikamata Italia ya Warumi, kipi kitafuatia?"
  Mfalme akajibu: Sicily ni kisiwa chenye hazina za thamani kubwa, itakuwa rahisi sana kukiteka kisiwa hicho."
  Cineas aliendelea kuuliza: " Bwana Mfalme, unaongea juu ya mambo ya kusadikika, lakini una maana kukitwaa kisiwa cha Sicily kutakuwa na maana ya kukoma kwa vita?" Mfalme akajibu: "Hapo tutakuwa tumeikaribia Afrika. Na tukishaikamata Afrika ni nani hapa duniani atathubutu kutukabili kivita?" "Hakuna" Alijibu Cineas, kisha akauliza; " Na baada ya hapo tutafanya nini?"

  Mpaka hapo Mfalme hakujua Cineas alikuwa anampeleka wapi kwa lojiki ya kifikra. Mfalme akajibu:
  "Baada ya hapo, tutapumzika, tutakula raha. Tutakula na kunywa. Tutabaki tukichekeshana na kucheka, siku nzima."

  Kama ni hivyo, alisema Cineas; " Ni kitu gani kinachotuzuia kufanya hayo yote sasa bila kwenda vitani?
  Mfalme hakuielewa mantiki ya Cineas. Akakaidi ushauri. Akavipeleka vikosi vyake kupambana na Warumi. Baada ya vita ngumu, jeshi la mfalme liliwashinda Warumi. Hata hivyo, lilipata hasara kubwa ya kupoteza watu na kuwa na majeruhi wengi. Jeshi lake likadhohofika sana. Likajaribu kuitwaa Sparta, likashindwa vibaya sana. Mfalme aliwindwa na hatimaye akakakamatwa kama kuku na kuawa kwa kupigwa mawe kwenye mitaa ya Argos.

  Isenga imbofu na isenga indenyeefu. Ng'ombe kipofu ni sawa tu na ng'ombe aliyevunjika mguu.

  Na hilo ndilo ‘Neno Leo.'

  Maggid,
  Iringa.
   
 2. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #2
  Oct 13, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Unajua hata uandike page 1000, the problem is "the agenda you are trying to drive". Worse enough kila wakati mtu anapokuwa tofauti na hiyo agenda basi he's some loon or else a dumb.
   
 3. I

  Interested Observer JF-Expert Member

  #3
  Oct 13, 2010
  Joined: Mar 27, 2006
  Messages: 1,402
  Likes Received: 434
  Trophy Points: 180
  At least you tried to be neutral
   
 4. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #4
  Oct 13, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Umeandika nini in summary?? kijani hahahaha?
   
 5. The Good

  The Good Senior Member

  #5
  Oct 13, 2010
  Joined: May 26, 2010
  Messages: 152
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Maggid una ujasiri wa pekee

  1. Huoni haya kutetea unachokiamini hata kama utawaudhi wengi. Mada zako humu zinachukiwa na wengi sana lakini huonekani kuyumba.
  2. Wengi humu wanaficha identities zao. Wewe unaiweka hadharani na huonyeshi woga wowote kueleza hisia zako.

  Keep it up
   
 6. Baba Mtu

  Baba Mtu JF-Expert Member

  #6
  Oct 13, 2010
  Joined: Aug 28, 2008
  Messages: 881
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Soma tena ili uelewe alichokiandika. Soma kwa kutaka kuelewa na usisome kwa jazba.
  Alichokiandika kinaeleweka vizuri tu.
   
 7. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #7
  Oct 13, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Si ujasiri kulazimisha watu wakubaliane na wewe unavyofikiria.............Ukiona wachangiaji wana mlengo tofauti kesho yake unaibuka na thread " aah mgombea kaongea we acha tu"
   
 8. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #8
  Oct 13, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 419,846
  Trophy Points: 280
  tatizo langu na maggid ni lilelile kuwa uhusiani na ucahguzi huu na mada yake ni finyu.

  Tunakwenda kwenye uchaguzi kwa matakwa ya kikatiba na wala siyo hiari. Hivyo, siyo sahihi kusema ya kuwa tuna hiari ya kushiriki katika uchaguzi au la!!!!!!!!1

  Vile vile, adui ambaye ni CCM sasa hivi amedhoofika sana kutokana na kuukumbatia ufisadi na kutokuwa tayari kubadili hulka nzima ya uendeshaji nchi ili ioane na mahitaji ya jamii ya karne ya ishirni na moja. Kuichagua CCM ni kukubali hakuna matatizo ya kiuchumi wala ya kijamii kusema hivyo ni kuidanganya nafsi yako tu na wala siyo vinginevyo. Matatizo yapo na yametuthibiti hivyo ni vyema tukayatafutia ufumbuzi wa kubadilisha katiba na muundo mzima wa uwajibikaji serikalini. CCM yasema hakuna haja ya mabadiliko kwa sababu mambo nishwari................Ni mwendawazimu tu ndiye atakubaliana na upupu huu

  Hizi ni sababu tosha za kwenda vitani na kumwondoa adui CCM ambaye anatumia adui watatu ambao ni umasikini, ujinga na maradhi kama silaha za kushinda chaguzi nchi hii.

  Hoja zako ndugu yangu Maggid ndizo mkoloni alimwambia Nyerere alipokuwa anadai uhuru na CCM imezinakili vivyo hivyo. Kuwa watanganyika hawakuwa tayari kujitawala na hawako tayari.............kabisa kujitawala lakini tuliwathibitishia ya kuwa hawakuwa wa kweli.

  CCM yadai Chadema haipo tayari kutawala lakini wapigakura ambao ndiyo waajiri wa tawala zote wataishangaza CCM hapo Oktoba 31
   
 9. m

  mwita ke mwita JF-Expert Member

  #9
  Oct 13, 2010
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 5,501
  Likes Received: 1,226
  Trophy Points: 280
  hii habari mbona niliwahi kuisoma siku nyingi sana kwenye gazeti fulani kama sio rai basi raia mwema , mbona mzee mzima maggid umeirudia humu :smow:
   
 10. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #10
  Oct 13, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Kasemaje??
   
 11. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #11
  Oct 13, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Mimi pamoja na elimu yangu nimeisoma na kusoma na kusoma na bado sijamuelewa. Mwenye elimu inayopita yangu maana hapa tunazidiana anisaidie kuifahamu. Na ikiwezekana yeye Maggid afanye hivyo nisije potoshwa. Asante.
   
 12. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #12
  Oct 13, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Majjid,
  nikivua japo haka kauelewa (kashule) kangu nakuelewa sana kwa kuwa nakuwa maamuma,
  lakini nikitumia haka kauelewa (kashule) kangu sikuelewi vyema kwa kuwa nakuwa siyo maamuma,

  hebu saidia kuweka wazi hasa kwakutumia lugha isiyo na matongotongo, maana huo siyo
  wakati wa vitendawili na nahau..........

  Heri ya Dr SLaa asokuwa kipofu wala kilema tena haanguki hovyo kuonesha
  afya mgogoro MPe KuRa
   
 13. S

  So Perfect Member

  #13
  Oct 13, 2010
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kama kuna watu wenye ujasiri wa kusimama kwenye ukweli bila ya kuwa na unafiki basi mjengwa wewe unaweza kuongoza humu JF. wengi humu ni wanafiki na wenye chuki zisizo na msingi! keep it up man!
   
 14. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #14
  Oct 13, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  mwisho wako wa kufikiri ndiyo mwanzo wa mwingine kufikiri
   
 15. Alnadaby

  Alnadaby JF-Expert Member

  #15
  Oct 13, 2010
  Joined: Sep 28, 2006
  Messages: 507
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Nimesoma na nimepata maudhui ya maana.Endelea na kuandika na ambao hawaelewi watakuuliza!
   
 16. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #16
  Oct 13, 2010
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,795
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145

  ...Pole. Angalau basi ngoja watu wakusifie. sio ujisifie mwenyewe. Kaaz Kwei Kwei.
   
 17. J

  JokaKuu Platinum Member

  #17
  Oct 13, 2010
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,805
  Likes Received: 5,108
  Trophy Points: 280
  ..ppl need to understand kwamba umati ulioko hapa jamii forums unalilia mabadiliko.

  ..Mjengwa hana haja ya kuja hapa na kuanza kukatisha watu tamaa, badala yake awaeleze wananchi what needs to be done kufikia mabadiliko wanayoyataka.

  ..so far tumeshuhudia utitiri wa makala toka kwa Mjengwa zikimpiga vijembe Dr.Slaa. hakuna makala yoyote ile ya kukosoa UOZO wa miaka 33 ya uongozi wa CCM.

  ..inawezekana Mjengwa ameridhika na hali yake ya maisha. lakini je ameridhika na jinsi wa-Tanzania wenzake kule vijijini wanavyoishi?
   
 18. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #18
  Oct 13, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  I vowed not to reply to Maggid's posts but let me ask rather than replying him

  is there a way you can improve you presentation skills? tumasoma habari nyingi sana ndefu lakini hatuchoki, ya kwako inakosa kitu fulani, its like you are struggling even to understand yourself

  Au basi unaweza ukawa unatoa summary ya hizo barua zako?
   
 19. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #19
  Oct 13, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  mmmhhhhhhh kweli mie simuelewi. Sasa nimemuuliza hajibu. Nikiandika vibaya anatishia kujinyonga. Mi nadhani naomba nimuazime kamba akajinyonge kisha akishamaliza kujinyonga anirudishie kamba yangu.
   
 20. 911

  911 Platinum Member

  #20
  Oct 13, 2010
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 761
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 60
  Sure mazee,ni Raia Mwema la tarehe 24/2/2010.
   
Loading...