Neno La Leo: Nchi Yetu Haina Dini, Na Koo Zetu Pia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Neno La Leo: Nchi Yetu Haina Dini, Na Koo Zetu Pia

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by maggid, Jan 27, 2011.

 1. m

  maggid Verified User

  #1
  Jan 27, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  [FONT=&quot]Ndugu Zangu, [/FONT]
  [FONT=&quot]Ni juzi tu nimepigiwa simu na msomaji wangu (RAIA MWEMA) akiwa kijiji cha Mwambata, Masasi. Amejitambulisha kwa jina la Edward Hassan. Alichotaka kuongea ni juu ya suala la Dowans. Suala hilo linagusa maisha yake. [/FONT]
  [FONT=&quot]
  [/FONT]
  [FONT=&quot]
  [/FONT]
  [FONT=&quot]Nikamdadisi juu ya mchanganyiko wa Edward na Hassan katika jina lake. Akaniambia; kuwa huko maeneo ya kusini ni kawaida sana. Utamkuta mtu anaitwa Dominick Rashid, John Ramadhan na mengineyo. Ni majina yanayotokana na dini za kimapokeo toka kwa Waarabu na Wazungu. Ni kweli, maana, Watanzania sisi tuna majina ya asili ya koo zetu. Majina yasiyotokana na dini za kimapokeo. Mengi ni majina yenye maana fulani.[/FONT]
  [FONT=&quot]
  [/FONT]
  [FONT=&quot]Ndio, Watanzania tumechanganyika kiasi hata kwenye koo zetu tunatofautiana katika imani za kimapokeo; Ukristo na Uislamu. Ni kawaida kabisa katika ukoo mmoja kuwakuta Waislamu na Wakristo. Kinachowaunganisha wanaukoo hawa ni mila zao za jadi ikiwamo matambiko yao. Na leo hii, katika nchi yetu, kuna familia zenye wanafamilia wa imani tofauti za kimapokeo; Uislamu na Ukristo. Ni kawaida kumkuta mama Mkristo na baba Muislamu au kinyume chake. Ni kawaida pia kuwakuta watoto wa familia moja wenye kufuata imani tofauti.[/FONT]
  [FONT=&quot]
  [/FONT]
  [FONT=&quot]Swali linakuja; hivi wenye kusambaza mahubiri haya ya chuki za kidini wanafahamu kuwa watachochea hata vita vya kikoo? Maana, koo zetu nazo zina tofauti za kidini, hususan dini hizi tulizozipokea toka kwa Wazungu na Waarabu. [/FONT]
  [FONT=&quot]
  [/FONT]
  [FONT=&quot]
  [/FONT]
  [FONT=&quot]Ndugu zangu, [/FONT]
  [FONT=&quot]Kuna kila dalili, kuwa sasa baadhi ya viongozi wa kidini na wanasiasa, kwa maslahi yao, wanafanya juhudi za kutugawa Watanzania kwa misingi ya kidini. Tusikubali kugawanywa na tukafikia kuchinjana. Hii ni nchi yetu, na kuna wanasiasa wanaotaka nchi yetu isitawalike. Nchi kutotawalika ina maana ya nchi kuingia katika hali ya vurugu ( State of Anarchy). Hivi, wenye kuombea hili wanaelewa hilo lina maana gani? Watanzania, Wazalendo wa nchi hii, tuna kila sababu ya kuihami nchi yetu dhidi ya chuki hizi za kidini na kisiasa. [/FONT]


  Mimi sasa naamini, kuwa Afrika mvunja nchi si mwananchi, bali ni mwanasiasa na hata kiongozi wa kidini. Ni kwa kutanguliza mbele maslahi binafsi na ya kundi dogo badala ya yale ya kitaifa. Masikini nchi yetu, Watanzania hawana udini ila kuna wachache, walio tayari kutumia mtaji wa udini kutimiza malengo yao. Inasikitisha sana, kuwa baadhi ya wanasiasa, hata kwa kutumia udini, wameamua kutupitisha Watanzania katika njia isiyo salama. Ili mradi, malengo yao yatimie.


  Watanzania tukubali sasa, kuwa nchi yetu imepatwa na bahati mbaya ya baadhi ya Watanzania wenzetu kuanza kupandikiza mbegu za chuki miongoni mwetu. Hili ni jambo la hatari sana.  Taratibu tumeanza kuizoea misamiati ya sisi na wao. Mathalan, sisi Wakristo na wao Waislamu. Sisi Wachagga na wao Wazaramo. Tunasahau, kuwa katika nchi yetu hii hakuna Sisi na Wao, kuna SISI tu.Tutakapokumbwa na maafa ya kitaifa watakaoathirika ni SISI, hakutakuwa na WAO.
  Na hili ni Neno La Leo. ( Hii ni sehemu ya makala yangu ya Raia Mwema, juma hili)

  Maggid
  Dar es Salaam
  Januari 27, 2010
  http://mjengwa.blogspot.com
   
 2. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #2
  Jan 27, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 896
  Trophy Points: 280
  Pumba!!

  Wewe na wana - CCM wenzako munaendeleza kujenga hisia za kipuuzi. hisia hatari za kidini katika akili za Watanzania kwa kuendelea kuandika makala za kishenzi-shenzi kama hizi.

  Naomba Mungu raia Mwema wasichapishe makala haya.

  Tumechoka na upuuzi wenu.
   
 3. G

  Gurti JF-Expert Member

  #3
  Jan 27, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 211
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Majid acha unafiki ni mwanasiasa gani aliasisi udini Tanzania na ambaye anauendeleza hadi leo kwa maslahi yake. Anaitwa Kikwete. Wewe mbona humtaji? Acha unafiki ndugu yangu, udini utatuangamiza wote. :msela::msela:
   
 4. G

  George Jinasa JF-Expert Member

  #4
  Feb 6, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 393
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Ndugu zangu matusi na jazba hayajengi wala hayawezi kuficha ukweli wala uongo. Hoja ya Bwana Maggid ni kwamba baadhi ya wanasiasa na viongozi wa dini wanataka kutupeleka katika udini. Hakutaja jina la kiongozi wa dini wala siasa. Mchangiaji mwingine anaibuka na kujibu kwa jazba na kisha kusema kiongozi huyo ni Kikwete. Sasa sijui hapa anapinga kuwepo udini au anakubali? Nini kinatufanya kushindwa kuvumilia hoja zinazopingana nasi. Wewe una macho gani ya kuweza kuona kila mtaa wa nchi. Kuona kila kanisa, msikiti na ofisi ya chama cha siasa? Kama mtu mzima anaibuka na kusema kuna udini mhoji atoe maelezo zaidi badala ya kumkatiza kwa vitisho na kejeri.

  Viongozi wa siasa na dini sio malaika wasiweze kutenda dhambi ya udini. Wananchi wanahaki ya kukosoa na kutahadharisha juu ya hili kama wanaona dalili. Kipindi cha Uchaguzi Mkuu dalili za udini zilikuwepo japo tafsiri ya udini tunaweza kutofautiana. Baadhi ya viongozi wa dini kutoa ilani ya uchaguzi mitizamo ya baadhi yetu nikiwemo mimi ni udini.Wapo wengi wenye mtizamo kama huu na tofauti yake. Kama kila mwaka wa uchaguzi kila dini watakuwa na ilani yao ya uchaguzi ni miaka michache ijayo tutakuwa tunachaguana kwa misingi ya kidini au kuzingatia maslahi ya kidini. Maana, kiongozi wa dini fulani anapotoa ilani yake ya uchaguzi anazingatia maslahi ya dini yake pamoja na mambo mengine. Maslahi ya wakristo sio lazima yawe sawa na ya waislamu. Hivi kiongozi wa kiislamu akisema chagua kiongozi mcha mungu ni lazima iwe sawa na kiongozi wa wakristo akisema hivyo?

  Tukienda mbele zaidi viongozi wa kikoo na kikabila nao wakianza kuandaa ilani zao za uchaguzi itakuwaje?

  Mimi naona kuna haja tukakaa na kujadiliana na kukubaliana mipaka ya wanasiasa na mipaka ya viongozi wa dini. Hilo litawezekana kama tukisikilizana na kuvumiliana. Kila mtu anahaki ya kutoa hoja anayoona inafaa.
   
Loading...