Neno La Leo: Na Wabunge Wetu Wengine Nao Ni Wezi, Hakyamungu!

maggid

JF-Expert Member
Dec 3, 2006
1,084
1,246
Ndugu zangu,

Waziri Muhongo ameusema ukweli wake kule Dodoma. Nami nimefuatilia sinema hii ya Dodoma, kila inavyoendelea ndivyo ninavyozidi kuchoka. Ama hakika, tunakokwenda siko, tuna lazima ya kujipanga upya.

Namsifu Waziri Muhongo kwa ujasiri wake. Amutusaidia sana kuyajua yale ambayo yangetuchukua muda mrefu kuyajua. Kwa kusimama kwenye ukweli Waziri Muhungo ameitendea haki nchi yetu tuliyozaliwa.

Na tulipofikia hapa ni ukweli tu ndio utakaotusaidia kutupa ahueni ya hali mbaya tuliyonayo kama taifa. Huu si wakati wa kutanguliza siasa za vyama bali kuitanguliza Nchi yetu tuliyozaliwa na tunayoipenda. Kutanguliza uzalendo.

Leo tunabaki vinywa wazi kusikia kuwa hata wachungaji, na wengine wamejiingiza Bungeni, kuwa nao wanawaibia Watanzania wenzao. Kwamba nao hawatosheki. Wanaiba huku wakitaja neno la Mungu. Leo hata wale wanaojinadi kuwa ni watetezi wa wanyonge wameanza kutiliwa mashaka. Uwezo wao wa kiuchumi unahusianishwa na ' madudu' kama haya ya Tanesco. Na kuna hata wenye ' kuwafuturisha' wenzao wenye uwezo kwa fedha walizowaibia wananchi wanyonge. Hawa hawana cha swaumu bali wanashinda na njaa kwa dhambi ya wizi wao.

Tuna lazima sasa ya kuamka na kuwabana wezi wetu. Mwizi ni mwizi tu, hata kama ni mheshimiwa Mbunge.Na ukweli ndio unaohitajika sasa. Na si nusu ukweli, bali ukweli mzima hata kama utatugharimu maisha yetu.

Nimepata kusimulia kisa cha kijana aliyehangaika sana kuusaka ukweli. Katika pitapita zake akaliona duka. Kibao kimeandikwa dukani ; " Hapa tunauza ukweli".

Dukani hapo ukweli unauzwa kwa kilo. Bei ya robo kilo ya ukweli imeandikwa, vivyo hivyo, bei ya nusu kilo ya ukweli. Lakini, mwenye duka hakuandika bei ya ukweli mzima, kwa maana ya kilo nzima ya ukweli.


Kijana yule akauliza; " Mie nataka ukweli kilo nzima, mbona hujaandika bei?"

" Alaa, unataka kilo nzima ya ukweli?" Aliuliza mwenye duka.
" Naam" Akajibu kijana yule.
" Basi, zunguka uje ndani nikuambie bei yake".

Alipoingia ndani dukani, kijana yule akaambiwa;

" Kijana, hatukuandika bei, maana, gharama ya ukweli mzima ni uhai wako. Je, uko tayari?"

Kijana yule akatimua mbio. Nyuma aliacha vumbi. Hakuwa tayari kulipa gharama ya ukweli mzima.


Katika Uislamu inasemwa; sema ukweli, hata kama unauma na kwamba unaweza kupelekea umauti wako.

Hakika, maandiko ya kwenye vitabu vya dini zetu hizi yana ya kutufundisha.

Na hilo ni Neno langu la Leo.


Maggid Mjengwa,
Sweden.
Mjengwa Blog::Habari,Picha,Matangazo

 
  • Thanks
Reactions: UKI
...


Katika Uislamu inasemwa; sema ukweli, hata kama unauma na kwamba unaweza kupelekea umauti wako.


Hakika, maandiko ya kwenye vitabu vya dini zetu hizi yana ya kutufundisha.


...


Maneno mazuri sana hapo kwenye
red. Lakini je tunaishi kadiri ya mafundisho na maongozi ya dini zetu? Mbona ni unafiki tu umetujaa huku tukijidai wenye dini? Kwa kuwa inaonekana dini zimeshindwa kubadili tabia na hulka zetu kuna haja sasa ya kutafuta njia mbadala.
 
mama rwakatare kweli,kuna mtu tulikuwa tunabishana kuwa rais kumpa mama rwakatare nafasi kuna kitu si hivihivi akabisha mengi sana yataibuka.
 
maggid unaweza kutusaidia ukiwa kama mwandishi ukapanga interview na Mchungaji Lwakatare? maana nimeogopa sana kama sasa watu wanahubiri wasichoamini je nchi hii inakwenda wapi?
 
Last edited by a moderator:

Maneno mazuri sana hapo kwenye
red. Lakini je tunaishi kadiri ya mafundisho na maongozi ya dini zetu? Mbona ni unafiki tu umetujaa huku tukijidai wenye dini? Kwa kuwa inaonekana dini zimeshindwa kubadili tabia na hulka zetu kuna haja sasa ya kutafuta njia mbadala.

mbadala wa ukweli....ukweli ukishindwa kutubadilisha nini kitatubadilisha?
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom