Neno La Leo: Mwana Wa Gavana Anapotenda Kosa...

maggid

JF-Expert Member
Dec 3, 2006
1,084
1,246
Na Maggid Mjengwa,


KUNA kisa cha mwana wa gavana katika Misri ya Kale. Mwana yule alitembea akijivunia cheo cha baba yake. Akajawa kiburi kufikia siku moja kumdhalilisha mwalimu wa shule mtaani huku watu wazima na watoto wengine wakiangalia.
Ndio, mwana yule alimchapa bakora ya matakoni mwalimu yule, hadharani. Mwalimu alifedheheshwa sana, maana hata kosa lake hakulijua. Mwalimu yule akafunga safari ndefu kwenda kuarifu jambo lile kwa mfalme wa nchi . Huko akapokelewa, akaeleza yaliyomsibu.
Mfalme akaamuru mwana yule wa gavana aletwe haraka kujibu shauri akimbatana na baba yake, gavana. Baada ya kusikiliza shauri lile, mtawala yule akajiridhisha kuwa mwana yule wa gavana alifanya kosa. Akamwamuru mwalimu yule achukue bakora na kumchapa mwana yule wa gavana bakora mbili. Bakora za matakoni.
Mwalimu aliinua bakora akaanza; moja, ikaja ya pili. Akatamka; “ Mfalme wangu, nimemaliza”. Mfalme akatamka; “ Bado, chukua tena bakora mchape gavana bakora tatu za matakoni”.
“ Ewe Mfalme wangu, gavana hajanitendea kosa lolote, ni mwanawe”. Alitamka mwalimu yule.
Mfalme akamwambia; “ Nimekwambia mchape gavana bakora tatu kwa kuwa bila ya yeye mwanawe asingetenda kosa hilo!”. Na hilo ni Neno La Leo.


Maggid, Iringa


mjengwa
 
Najiuliza mengi. Kisa kilichoelezwa hapo juu nadhani hakina tatizo per se. Pia kina mafunzo mazuri kwa anayyetaka kujifunza. Tatizo langu ni kwamba sijaona uhusiano wa jukwaa hili la Siasa na kisa hiki. Hata hivyo Mjengwa kama ndiye nnayemfahamu katika gazeti la Raia Mwema, napata kigugumizi kwa kuwa uandishi nnaouona hapa ni wa aina ya Mjengwa (Kusimulia kisa kabla ya Uchambuzi), tofauti tu ni kuwa sikutgemea thread hii hapa. Nadhani wadau watanisahihisha nilipokosea au kunifafanulia ambapo siijaelewa maana huenda kuna falsafa ama fumbo ambalo sijalielewa hapa, adios.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom