Neno La Leo: Mwadhama Kardinali Pengo, Nina Nyongeza Ya Neno

...hivi Askofu Mkuu Kilaini aliongea lini na Mwenyezi Mungu akamwambia JK ni chaguo la Mungu kama siyo utapeli kwa kumdhihaki Mwenyezi Mungu.................

Mkuu sahihisho kidogo la kiitifaki. Kilaini si Askofu Mkuu ni Askofu Msaidizi.
 
Majid,

mbona kama umeshachakachuliwa? jambo ulilobandika hapa halina mantiki inayorandana na hali alisi. watanzania tumeudhika kudhulumiwa, hatuhitaji busara za kinafiki za pengo. alikuwa wapi wakati wote? kwa nini anaidhinisha dhuluma? ningemuelewa kwamba ni mpenda haki kama angekiri kwamba dhuluma imefanyika na kwamba siyo vizuri na kwamba anajitolea kutafuta maridhiano kwa lengo la kuweka misingi imara kwamba dhuluma hizi hazitatokea tena 2015.

Sasa unasema ni maneno ya busara kuenzi amani hivyo tunyamaze kimya halafu 2015 tutafanya nini? tutanyamaza pia ili kuenzi amani, na ndiyo maana kila ccm wakiambiwa wasidhulumu hoja yao ni ile ile ya pengo, amani na utulivu, tusiruhusu wamwaga damu.

Maggid rudi Rai kama unataka Raia mwema iendelee kununuliwa. Usiwaharibie wenzio biashara tafadhali.
 
Hila, dhuluma na uzandiki siku zote haviwezi kudumisha amani. Hizi ngonjera za amani ilitakiwa tuzielekeze katika kujenga "miundo mbinu" ya kuzuia hila, dhuluma na uzandiki unaofanywa na watawala dhidi ya watawaliwa. Wale walioko madarakani ni lazima wajue wajibu wao na wajue kuwa wanawajibika kwa nani?

Unapokaa kimya wakati dhuluma, hila na uzandiki vinatamalaki, unaiangamiza jamii. Hakuna mahali duniani ambapo amani imetamalaki katika lindi na maovu kama inavyoendelea hapa nchini kwetu. Wale wanaobaka haki za watu wengine ndio wanaofanikiwa na jamii nzima tunalazimishwa tuwainamie! Ni kweli inatakiwa tuangalie njia zetu tunazotumia, lakini mwizi lazima aambiwe kuwa wizi ni kitu kibaya.

Hizi kauli tunazozisikia baada ya uchaguzi zinaashiria kuwa watu wote hawa wanajua uovu uliofanyika ila wanaogopa matokeo ya uovu huo! Sasa ni kitu gani kitakachowaambia waovu kuacha uovu? Hivi tunaamini kuwa Tanzania itaongozwa kwa hila na dhuluma?

Mwalimu Nyerere alifanikiwa kwa kutenda haki! Amani inamomonyolewa na viongozi wanafiki wanaoendekeza utawala wa hila na fitna. Tuwe makini!
 
Magid mimi huwa nakuheshimu sana kwa sababu kuu mbili.

1. Gazeti la Raia Mwema ambamo unaandika makala zako.
2. Nakuchukulia kama mwandishi mahiri.

Lakini sasa naomba niwe wazi kuwa kwa kipindi hiki cha uchaguzi, umeonesha kuwa hufai hata kidogo.

Huwezi kuficha hisia zako za kichama kama alivyo Masako na wengine wasiojua wanachokifanya kama vile Gondwe. Ujue kuwa makala unazoandika hazisomwi na wanaccm tu, wewe ni mwandishi wa habari kwa watz wote sio ccm pekee.

Unapoandika makala tafadhari vaa uandishi na siyo uchama, upo hapo kuwahabarisha watz wote siyo ccm pekee. Unanikera kuliko mbu wanaoeneza malaria.
 
Hivi kumbe kila kiumbe anaweza andikia RAIA MWEMA akijitahidi eeh! I am stunned.
duh!!!!!!! ulidhani wanaoandika RAIA MWEMA ni malaika????
ungejua wanaandika kile ambacho wajinga mnataka na kupenda kukisoma!!!
poleni sana wasomi ambao akili zenu zinaendeshwa na vyombo vya habari.ENDELEENI KUKANA KILE MNACHOKISHUHUDIA KWA MACHO NA MUAMINI KIILE KINACHANDIKWA NA lula ndali mwanzela
 
mwadhama,utamkapo juu ya busara na hekima wanaoshiba inawagusa sana. Tatizo ni kwamba ccm itaonaje busara ili wote angalau wapate sehemu ya keki hii ya Taifa. CCM imekumbatia mafisadi, wanyonge na watoto wao waliyoifundisha adabu ccm wameona kura zao hazikutosha kuwaondoa mafisadi. Je unategemea nini baadaye?
 
maggid umerudi tena nilidhani wameshakupa ujumbe wa nyumba kumi kumi kijijini kwenu..Sasa ndio nini umetuletea hapa soma mwenyewe na tafakari mwenyewe. Kampeni zimeisha bana kila mtu ataongea analotaka lakini watanzania wenyewe ndio wenye maamuzi acha kutufanya kama hatuna akili na maarifa..... whoever kasema so what??? pim...wweee!! Sipendi hii mtu mimi.
 
[/QUOTE]
Kama huamini CCM imepandikiza chuki ya udini na ukabila, hebu jaribu kufanya analysis ya ushindi wa CCM kwa majimbo, utagundua kuwa CCM imepata ushabiki mkumbwa sehemu za mamwinyi na hii ni matokeo ya strategy za Kikwete na CCM kwa kutumia neno udini.

KWA MAANA HIYO ZILE SEHEMU WALIZOSHINDA CHADEMA ZINAUSHABIKI MKUBWA WA KULA KITI MOYO SIO????
 
Kardinali Pengo anatambua kasoro tele katika uchaguzi tulioumaliza. Ninakiri hajakemea kwa nguvu kasoro hizo.
Lakini pia kardinali anatambua kwamba hii mamlaka itabakia madarakani hadi 2015, pamoja na kasoro zote na malalamiko yote. Hii ndio hali halisi.
Tugange yajayo. Tujipe moyo na kufanya mikakati kutokea sasa ya kuhakikisha 2015 mambo yanakwenda sawasawa.
 
Jamani najua hapa Maggid kajijengea maadui wengi pamoja na mimi. Lakini kwa hili naomba nimtetee kidogo. Maana nilivyoelewa yeye kawakilisha kama ripota yale ambayo Pengo kasema. Kwa maana nyingine leo hakuleta makala bali kaja kama ripota.
Sasa basi ebu mijadala yote ielekezwe kwa Pengo na si Maggid ingawa huko nyuma Maggid alitukosea.
Pengo kama viongozi wengine wengi wa dini ni viongozi wanaotushangaza watanzania hasa wanapokaa kimya bila kukemea uovu wa watawala. Mimi ningemshauri kwa kuwa yeye na viongozi wengine wa dini waliamua kufunga mdomo wakati wa kampeni Kikwete alipowataka wakae kimya, basi na akae kimya milele na atuachie ligi sisi na Kikwete regime. Kuingilia ligi hii kwa namna yoyote ile ni kuingilia ligi isiyomhusu maana alishachagua his own side. Akae kimya milele na viongozi wengine wa dini pia ambao hawakuona haja ya kuzungumza wakati ule wakae kimya pia milele. Tunakinaishwa na kelele zao
 
Kardinali Pengo anatambua kasoro tele katika uchaguzi tulioumaliza. Ninakiri hajakemea kwa nguvu kasoro hizo.
Lakini pia kardinali anatambua kwamba hii mamlaka itabakia madarakani hadi 2015, pamoja na kasoro zote na malalamiko yote. Hii ndio hali halisi.
Tugange yajayo. Tujipe moyo na kufanya mikakati kutokea sasa ya kuhakikisha 2015 mambo yanakwenda sawasawa.
Mimi nasema hatambui. Siamini kama ni huyu Pengo nileyesikia anamwambia Kikwete uso kwa uso kwamba Serikali isijaribu kulichangulia kanisa kitu cha kusema, na sasa hawezi kusema. Nasema hatambui.
 
maggid ninayemjua mimi ni yule aliyeolewa na kibibi kizee cha kizungu. maskini sasa ona kimemrisisha mawazo ya kizee, fikra za kizee sasa amekuwa kama mzee ilhali ni kijana.we maggid sisi hatuitaji mahubiri yako hapa sisi tunachohitaji ni njia za kuikomboa nchi na rasilimali zetu na sio utumbo huu.
 
Maggid Mjengwa!

Kwanza kabisa napenda kupiga hodi JF.
Sina uhakika kama neno AMANI linatamkwa baada ya kuchanganua na kujiridhisha na chembechembe zake. Hatuhitaji kwenda shule ili tuweze kutambua kuwa nchi yetu haina amani au la. Kwanini ujenge nyumba yenye mageti saba? kwa nini mbwa? kwa nini mlinzi? kwa nini security guard? kwa nini oysterbay? Kwa nini mlo mmoja? Kwa nini nyumba mbovu sawa na shimo analolala fisi?. Kimsingi nchi yetu haina amani. "Mwenye gari hana uhakika na gari yake mahala popote atakapo paki, ukipata ajali barabarani huokolewi badala yake ama wakumalizie au wachukue chochote wanachoona inafaa". Je, hii ni amani? Vijana hawana kazi na wamekata tamaa ndiyo maana tunatumia gharama kubwa kujilinda badala ya kuwekeza na kuzalisha. Ukiambiwa kitu usikichukue kama kilivyo, nawe fikiri pia. Nadhani Pengo anakosa maana halisi ya neno Amani. Viongozi wadini wasidanganye watu; maisha yakiwa magumu hiyo siyo amani hata siku moja. Kama wanadhani ni utani wasubiri muda si mrefu hata waumini watawakosa makanisani na misikitini. Please, be extra aggressive rather than passive. Hata ukiogopa kufa leo, siku yako itafika tu. Tudai haki zetu na siyo kuleta maneno ya faraja yasiyokuwa na tija.


 
Mbona amani inahubiriwa na wale tu wenye maisha yanayofanana na ya ikilu?mbona sie wenye zile ajira za kufungua vizibo hatuioni hiyo amani?Si ndio hawa hawa mwaka 2005 walisema JK ni chaguo la Mungu?au tumesahau.kwa niaba ya wafungua vizibo naomba niseme hatudanganyiki!
 
Duu! nilidhani watawala wangekukumbuka kwa juhudi zako which hata wewe unajui zina walakini, likely unatwanga maji kwenye kinu,look at you dont be that much kipofu,wapi na wapi amani at the cost of your constitutional right, hebu kuweni na ujasiri wa kuwa fair than kukosoe upande dhaifu pekee.
 
maggid mjengwa!

kwanza kabisa napenda kupiga hodi jf.
Sina uhakika kama neno amani linatamkwa baada ya kuchanganua na kujiridhisha na chembechembe zake. Hatuhitaji kwenda shule ili tuweze kutambua kuwa nchi yetu haina amani au la. Kwanini ujenge nyumba yenye mageti saba? Kwa nini mbwa? Kwa nini mlinzi? Kwa nini security guard? Kwa nini oysterbay? Kwa nini mlo mmoja? Kwa nini nyumba mbovu sawa na shimo analolala fisi?. Kimsingi nchi yetu haina amani. "mwenye gari hana uhakika na gari yake mahala popote atakapo paki, ukipata ajali barabarani huokolewi badala yake ama wakumalizie au wachukue chochote wanachoona inafaa". Je, hii ni amani? Vijana hawana kazi na wamekata tamaa ndiyo maana tunatumia gharama kubwa kujilinda badala ya kuwekeza na kuzalisha. Ukiambiwa kitu usikichukue kama kilivyo, nawe fikiri pia. Nadhani pengo anakosa maana halisi ya neno amani. Viongozi wadini wasidanganye watu; maisha yakiwa magumu hiyo siyo amani hata siku moja. Kama wanadhani ni utani wasubiri muda si mrefu hata waumini watawakosa makanisani na misikitini. Please, be extra aggressive rather than passive. Hata ukiogopa kufa leo, siku yako itafika tu. Tudai haki zetu na siyo kuleta maneno ya faraja yasiyokuwa na tija.



uliyoyasema nakuunga mkono na miguu yote! Ila naomba ufafanuzi kidogo, jee, unashauri tufanyeje ili tuipate hiyo amani, jee, tutumie nguvu au mazungumzo? Maana ukichunguza nchi zote zilizoingia ktk machafuko mwisho wake watu wanaamua kukaa chini na kuzungumza ni vipi amani ipatikane!!! Sasa sijui wewe unatushauri vipi?
 
Maggid katika hili huna nyongeza. Kadinali Pengo ameongea kwa umahili mkubwa sana huku akitazama mamlaka na katiba tuliyonayoa sasa. Ameenda mbali zaidi kwa kuonya ya kuwa, hata kama mamlaka zilizopo zitaona kuwa wananchi wamekikataa chama tawala kwa njia ya kura basi wakiambie kipishe ili kulinda jambo la msingi ambalo ni amani ya taifa. Na vivyo hivyo kwa vyama vingine vyote. Hayo yote amesihi yafanyike kwa Uhuru na Haki ili amani hiyo isipotee na hatimae itugharimu kuirejesha kama tunavyoshuhudia nchi jirani au nyingine zenye kufanana na hizo. Msome Kadinali VIZURI. Utagundua HEKIMA NA BUSARA ZAKE.
 
Back
Top Bottom