Na Maggid Mjengwa,
" SIO kila mmoja ataridhishwa na matokeo, isipokuwa, jambo la msingi ni kulinda lengo kuu ambalo ni amani ya taifa". Hiyo ni kauli ya Askofu Mkuu Jimbo Kuu la Dar es Slaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo alipozungumza kwenye kipindi cha ujumbe wa Askofu Pengo kilichorushwa na Redio Tumaini na kuripotiwa na gazeti la Mwananchi, Ijumaa, Novemba 5, 2010.
Kwa ye yote mwenye kuitakia mema nchi yetu, basi, atakubali, kuwa, kauli ya Mwadhama Kardinali Pengo ni kauli iliyojaa busara na hekima nyingi. Ni ya kuungwa mkono. Na hapa nina nyongeza ya neno, maana, Kardinali Pengo amenukuliwa pia akitamka; kuwa mataifa mengi ulimwenguni yamejikuta yakitumbukia katika maafa kutokana na kutoridhishwa na matokeo ya uchaguzi. Askofu Pengo akawataka viongozi wa vyama na jamii wasichukue hatua zinazoweza kuliangamiza taifa. Akatamka;
"Mungu atujalie moyo wa kupokea matokeo yalivyo na hata tusiporidhika tujipe moyo ili tusije tumbukia katika maafa ambayo yatachukua muda mrefu kuondoka". ( Mwadhama Kardinali Polycarp Pengo, Mwananchi, Novemba 5, 2010)
Na hapa tena nina nyongeza nyingine ya neno. Hakika, ni busara na hekima, kwa mwanadamu kutambua na kuheshimu mamlaka iliyopo na zaidi, inayotokana na watu. Kutambua na kuheshimu mamlaka inayotokana na sheria, kanuni na taratibu za mahali husika, hivyo basi, mamlaka inayotokana na Katiba ya wakati huo. Na mwanadamu huyo, midhari amefanya mawili hayo, hana lazima ya kufanya jambo la tatu; kuyaenzi mamlaka hayo.
Yawezekana kabisa, kuwa katika kuyapata mamlaka hayo kukawa na mapungufu ya sheria, kanuni na taratibu. Lakini, hayo yasipewe nafasi ya kufanya mchakato wa kisiasa katika jamii ukakwama. Maana, siasa ina maana ya majadiliano endelevu. Ni majadiliano yasiyo koma. Muhimu katika siasa ni kubaki katika meza ya majadiliano.
Na hilo ni Neno La Leo.
Maggid
Iringa, Novemba 9
( Ni Sehemu ya makala yangu ya Raia Mwema ikichapwa kesho Jumatano)