Neno La Leo: Mtoto Anapokosa Titi La Mama Anafanyaje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Neno La Leo: Mtoto Anapokosa Titi La Mama Anafanyaje?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by maggid, Nov 2, 2010.

 1. m

  maggid Verified User

  #1
  Nov 2, 2010
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Ndugu zangu,

  MTOTO anayetegemea maziwa toka titi la mama anafanyaje anapolikosa? Jibu lake; mtoto huyo atahangaika sana, na kama ataliona titi lingine, atalishika alinyonye, hata kama si la mama yake. Na mtu mzima anafanyaje? Nawe una majibu yako.

  Hatimaye Watanzania tumeshiriki tena kwenye zoezi la kuwachagua viongozi wetu. Katika nchi , matokeo ya uchaguzi yana maana pia ya ujumbe au salamu zinazotolewa na walioshiriki uchaguzi huo, yaani wananchi kwenda kwa viongozi. Nionavyo, matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu yamebeba ujumbe mmoja mkubwa, lakini mfupi sana; MABADILIKO.

  Kwamba umma umeanza kwa dhati kabisa kuonyesha unataka mabadiliko. Hamasa ya kisiasa imeongezeka. Kazi ya wanasiasa na hususan vyama vya siasa ni kusaidia kuyaongoza mabadaliko hayo katika njia salama. Na matokeo ya uchaguzi wa mwaka huu, kwa mara nyingine tena, kama kutakuwapo na dhamira ya kisiasa, yanakipa Chama Cha Mapinduzi, jukumu hilo kubwa la kuyaongoza mabadiliko hayo.

  Kama Chama Cha Mapinduzi kina nia ya kupunguza kupotea kwa imani ya umma kwa chama hicho, basi, kutahitajika sio tu kufanyika mabadiliko makubwa ndani ya muundo wa Serikali na uongozi wa Chama Cha Mapinduzi, bali kufanyika kwa mabadiliko makubwa yenye kishindo.

  Kuna watakaopuuza, lakini, kuna ukweli, kuwa tuhuma za ufisadi zimeipaka matope mno CCM. Kwenye macho ya umma, Chama hicho kimechafuliwa na tuhuma hizo za ufisadi. Kuna wana CCM leo wanajiuliza kama wavae sare za chama au la wapitapo mitaani. Maana, kuna Watanzania walioanza kuchukia rangi za chama hicho. Wanazihusisha na ufisadi.

  Na matokeo ya uchaguzi wa mwaka huu yawe ni fundisho kwa chama tawala. Kama CCM inataka kubaki kwenye mioyo ya Watanzania wengi, kuwa na uhalali wa kubaki madarakani, basi, ina lazima ya kujipambanua kwa vitendo kutoka kwenye yote makubwa yenye kuhusiana na ufisadi na maovu mengine. Ibaki kuwa kimbilio la wanyonge. Isifike mahali, Chama kikajikuta katikati ya mgogoro na umma. Hilo laweza kuharakisha mazishi ya chama yasiyo na kisomo. Na hilo ni Neno La Leo.


  ( Neno hilo ni sehemu tu ya makala yangu Raia Mwema, juma hili)


  Maggid,
  Iringa,

  Novemba 3, 2010
   
 2. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #2
  Nov 2, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135

  Trash,Wewe kila siku NENO LA LEO MBONA KICHWA CHAKO KIGUMU KUFIKILIA??
   
 3. J

  Jenifa JF-Expert Member

  #3
  Nov 2, 2010
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 603
  Likes Received: 193
  Trophy Points: 60
  mafisadi mmeponea tundu la sindano mwaka 2015 tutawamalizeni kabisa. maggid na mafisadi wako wote wezi tu hatudanganyiki
   
 4. Deodat

  Deodat JF-Expert Member

  #4
  Nov 2, 2010
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 1,279
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145


  Mjengwa, ndio umegundua leo kuwa watanzania wanataka mabadiliko? kejeli na dhihaka zako kwa wapinzani zinaanza kutoweka eeh? sikutofautishi na wale wasanii wa bongo fleva walikuwa kwenye majukwaa ya JK tena wamedhulumiwa malipo yao jana wanampigia simu SUGU eti "hongera kaka! umetuwakilisha!". Maggid, Nguvu ya umma ni kubwa kuliko fedha za mafisadi, na HILO NDILO NENO LANGU LA LEO
  .
   
 5. Kivumah

  Kivumah JF-Expert Member

  #5
  Nov 2, 2010
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 2,413
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  who is this Majjid??
   
 6. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #6
  Nov 2, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Asante kwa kugundua hilo.
   
 7. B

  Binti Sayuni JF-Expert Member

  #7
  Nov 2, 2010
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 357
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Hivi ni neno la leo au kesho?
   
 8. Pakawa

  Pakawa JF-Expert Member

  #8
  Nov 2, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,737
  Likes Received: 3,170
  Trophy Points: 280
  maggid (lower case)......Acha kuupaka upinzani mafuta kwa mgongo wa chupa fi...wewe!! Ulikuwa wapi kuyaandika haya siku zote? By the way hatusomi kijarida chako maana umejawa na unafiki kupita maelezo. Wewe ni mwongo. Uchaguzi umeisha watanzania wameamua lakini CCM imewaamulia wewe tutakutana mitaani maisha yanaendelea. Mwaka 2015 utakuwa kwenu kijijini maana maisha ya mjini yatakuwa yamekushinda kwa ugumu wa maisha. Na hivo umezoea kuhamahama kama mbayuwayu sitoshangaa kama utakuwa kisarawe umepanga nyumba ya vyumba viwili utaliona joto ya jiwe halafu urudi hapa utuambie CCM mchuzi na urojo
   
 9. Emma Lukosi

  Emma Lukosi Verified User

  #9
  Nov 2, 2010
  Joined: Jul 22, 2009
  Messages: 932
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  CHAMBIO la MAFISADI!!!!
   
 10. The Dreamer

  The Dreamer JF-Expert Member

  #10
  Nov 2, 2010
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ahsante Paukwa Pakawa kwenye hiyo red coloured
   
 11. WABUSH

  WABUSH JF-Expert Member

  #11
  Nov 2, 2010
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 285
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  HUyo ndio mjengwa jamani! I am always trying hard to understanding his postulations
   
 12. m

  maggid Verified User

  #12
  Nov 2, 2010
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Wabush,
  Heri yako unayejaribu kufanya bidii ya kuelewa ninachowasilisha. Ni shida yao, wale wasiofanya kazi hiyo.
   
 13. K

  Keil JF-Expert Member

  #13
  Nov 3, 2010
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mimi ninasubiri tathimini ya mwandishi makini kwamba CUF itashinda viti 20 bara, 8 vikiwa kwenye ngome ya CUF ambayo ni mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma na kwamba wangeshinda udiwani na kufanikiwa kuunda/kuongoza halmashauri 2.
   
 14. Rufiji

  Rufiji JF-Expert Member

  #14
  Nov 3, 2010
  Joined: Jun 18, 2006
  Messages: 1,710
  Likes Received: 161
  Trophy Points: 160
  Nadhani wakati umefika wa kukuhukumu kutokana na maneno yako mwenyewe uliyowahi kuropoka hapa. Mimi neno langu la leo ni ...

  Chama chenye makada wengi wenye kuielewa itikadi, malengo na shabaha ya chama, huwa hakimtegemei mtu mmoja katika kuwepo kwake. Hakimtegemei mtu mmoja katika kufanikisha ushindi wa chama. Hakimtegemei mtu mmoja katika kuhamasisha wanachama au umma. Chama hicho hujiamini. (Maggid)
   
 15. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #15
  Nov 3, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,435
  Likes Received: 19,787
  Trophy Points: 280
  .:llama:
   
 16. K

  Keil JF-Expert Member

  #16
  Nov 3, 2010
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mkuu Rufiji,

  Huu ndio wakati wa kumkumbusha yale "mawazo/fikira huru" zake ambazo zote zilikuwa zinaelekezwa kuiponda CHADEMA na Dr. Slaa. Sasa naona amekuja na mpya ya kujisafisha baada ya kuona kwamba alichokuwa anaandika hakikuwa na mantiki na ndipo wengine tunaendelea kujiuliza hivi alikuwa anaandika maneno hayo kwa malengo yepi au nini kiini cha msukumo wa maandishi hayo?
   
 17. Rufiji

  Rufiji JF-Expert Member

  #17
  Nov 3, 2010
  Joined: Jun 18, 2006
  Messages: 1,710
  Likes Received: 161
  Trophy Points: 160
  Coach Parcells,

  Tafadhali ondoa message yako hapo juu, that's unacceptable and below the belt. Let us learn to disagree without insulting each other.
   
 18. Rufiji

  Rufiji JF-Expert Member

  #18
  Nov 3, 2010
  Joined: Jun 18, 2006
  Messages: 1,710
  Likes Received: 161
  Trophy Points: 160
  Coach Parcel,

  Once again I am arguing you to remove the above message. Even though I disagree with many things that Maggid has postulated, I vehemently defend him on this one. It is reprehensible to attack one's family member; in summary family members are off- limit! Frankly speaking, it is message like yours ,Coach Parcel, that are destroying JF's reputation! Plz let's maintain the level civility that has been around for years now. By the way, I have already informed the moderator and I hope he will act swiftly.
   
 19. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #19
  Nov 3, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  sielewi kwanini Raia Mwema bado wanampa nafasi huyu dogo
   
 20. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #20
  Nov 3, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,179
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  Safi.

  Leo naona sisikii miluzi ya mbwa.
   
Loading...