Neno La Leo: Msijiulize, Nani Atakuwa Rais 2015, Jiulizeni, Mtampataje?

Unafikiri CCM wapo tayari kuanzisha mchakato wa kubadili katiba? Na swala la kuunda Tume huru ya uchaguzi hawa CCM wapo tayari?


Fidel,

Kwa tunavyoenenda, Katiba mpya haina maana ya CCM kuwafanyia favour wapinzani. Ina maslahi hata kwa CCM yenyewe. Iko siku nitalifafanua hili kwa mifano.
 
Fidel,

Kwa tunavyoenenda, Katiba mpya haina maana ya CCM kuwafanyia favour wapinzani. Ina maslahi hata kwa CCM yenyewe. Iko siku nitalifafanua hili kwa mifano.

Maggid,

Nakubaliana na wewe kwamba ili tupate mabadilliko ya kweli, basi katiba yetu inabidi ifanyiwe marekebisho makubwa. Ni muhimu kutambua ya kuwa katiba yetu ilitengenezwa kipindi ambapo chama kilikuwa kimeshika hatamu na kwa maana hiyo basi haiko compactible na mfumo wa vyama vingi. Nakubaliana na Fidel80 kuwa CCM hawako tayari kuruhusu mabadiliko ya katiba kwani wanajua kwa kufanya hivyo watakuwa wamehalalisha kushindwa kwao. Cha kusikitisha ni kuwa CCM wanafikiri ya kuwa watakuwa madarakani milele, ndio maana wanapinga kitendo chochote cha kutaka mabadiliko ya katiba. Watu hawa ni wagumu sana wa kusoma alama za nyakati, lakini ipo siku katiba hii wanayojivunia leo itatumiwa kuwaazibu wenyewe; wamuulize Kaunda nini kilimpata pale Chiluba aliposhindwa.

Ili tupate Katiba mpya ni lazima serikali ipate pressure toka kwa wananchi. Mimi naamini kabisa kama nyinyi waandishi mkiungana na wadau mbali mbali kama wanavyuo na wanasiasa mkaielimisha jamii umuhimu wa katiba mpya, ili jambo linawezekana kabisa. Aiingi akilini kwa mtu kumtegemea Jaji Lewi Makame ambaye alikuwa apointed na Rais, and he is serving at the president discretion, to rule against JK. Ni lazima katiba itakayokifanya hiki chombo NEC kuwa huru kabisa! Na viongozi wa hiki chombo wapewe life time appointments, hii itawafanya wawe huru katika maamuzi bila ya kuhofia ni chama gani kitakuwa madarakani.
 
Wazalendo:

Nyerere alipoulizwa kuhusu mambo ya Ujamaa na siasa zake alisema anatembea na vitabu viwili tu: Biblia na Azimio la Arusha. Kwa maoni yangu baba wa taifa alitakiwa atembelee na katiba. Sisi tuliopata bahati ya kusoma siasa tukiwa mashuleni tulikuwa tunajua muundo wa chama na miiko ya viongozi kwa kusomeshwa katiba ya chama lakini sio ya nchi. Hivyo kwa miaka mingi katiba ya nchi sio sehemu ya maisha ya mtanzania.

Tutatoa mifano ya wamarekani na katiba yao. Lakini kitu cha kukumbukwa ni kuwa Mmarekani hata akiwa mpuuzi au mwizi anajua angalau kwa kiasi fulani haki zake za kikatiba.

Inafika miaka 50 sasa toka madaraka ya ndani yapatikane, lakini ni watanzania wachache wenye kujua haki zao za kikatiba. Hivyo basi viwili muhimu vya kufanya. Kitu cha kwanza ni kuwa na mabadiliko ya kikatiba. Na kitu cha pili ni kuwafanya watanzania wajenge utamaduni wa kufuata na kuelewa haki zao za kikatiba. Hii ni kwa sababu tusipojenga utamaduni huo, hakuna atakayeheshimu katiba yenyewe. Kutoheshimu katiba ni kitu cha kawaida sana katika nchi za kiAfrika.

Kwa mfano katiba ya Liberia ni copy ya katiba ya Marekani. Lakini kwa sababu wale waMarekani weusi waliorudi Afrika walihamua kuendelea maslahi yao kuliko maslahi ya wazawa matokeo yake tuliyaona.

Na hili katiba ieleweke na kujengewa utamaduni ni lazima iwe simple hata kwa mtoto wa darasa la tatu aweze kujifunza. Tatizo la katiba ya sasa imeandikwa hili isomwe na mwanasheria na sio mwananchi wa kawaida.
 
Back
Top Bottom