Neno La Leo: Msijiulize, Nani Atakuwa Rais 2015, Jiulizeni, Mtampataje?

maggid

JF-Expert Member
Dec 3, 2006
1,084
1,246
Ndugu zangu,

KATIKA kuadhimisha miaka kumi ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi, CCM na miaka 20 ya Azimio la Arusha, Mwalimu Julius Nyerere alikubali kufanya mahojiano ya kipekee na ya aina yake na Mhariri wa gazeti la Uhuru. Huo ulikuwa ni mwaka 1987.

Katika mahojiano yale Mwalimu, akiwa Mwenyekiti wa CCM hakusita kutamka bayana, kuwa Chama alichokuwa akikiongoza kilikuwa na kasoro na mapungufu mengi.

Mwalimu aliona dalili za kupungua kwa moyo wa kujitolea. Aliona dalili za kupungua kwa maadili ya uongozi. Mwalimu aliona dalili za mioyo ya kimamluki ilivyoanza kuingia na kuenea ndani ya CCM na nchi yetu. Mwalimu alifikia kumtamkia mhariri yule wa gazeti; " Tumewapa uongozi watu wasiofaa. Nadhani wengi ndani ya Chama tumeanza kuutambua ubovu huu. Hatua ya kwanza kutibu maradhi ni kuyatambua." Alitamka Mwalimu.

Ndio, Mwalimu aliona mbali, hii leo viongozi wanaofanya matendo maovu na ya kimamluki ndani ya vyama vya siasa na nchi kwa ujumla ndio wale aliowatabiri Mwalimu miaka 23 iliyopita.
Ni dhahiri, kuwa demokrasia yetu bado ni changa mno. Huu ni wakati wa kuwa makini katika kujenga misingi imara ya demokrasia yetu.Makala yangu ( Raia Mwema) juma la jana ilizungumzia amani. Nilirejea kauli ya ya Mwadhama Kardinali Polycarp Pengo juu ya suala hilo. ( Mwananchi, Novemba 5, 2010)

Mwadhama Kardinali Pengo alizungumzia umuhimu wa uwepo wa amani. Katika makala yangu hayo nilikwenda mbele zaidi. Nilibainisha, kuwa pasipo haki hakuna amani. Na swali ni je, haki inapatikana vipi?

Hivyo, nikaongeza kuandika, kuwa swali tusilopaswa kujisumbua kujiuliza ni juu ya nani atakuwa Rais wetu mwaka 2015, bali, tujisumbue kwa kujiuliza; Je, Rais wetu wa 2015 tutampata kwa katiba ipi, na kwa mfumo gani wa uchaguzi? Sote, wakiwamo viongozi wa dini, tuna lazima ya kuyatafuta majibu ya maswali haya.

Kwa mfano, wenzetu kule Marekani katiba yao ina zaidi ya miaka mia mbili. Kubadili kipengele tu katika katiba ya Marekani inaweza kuwa ni mchakato wa miaka kumi. Hakuna hata Rais wa Marekani anayeweza kuichezea Katiba ya Marekani kwa maslahi yake, anaweza kuishia gerezani anayejaribu kufanya hivyo. Wamarekani wale hata wakimweka ‘mwendawazimu' Ikulu wanajua namna ya kumdhibiti kikatiba.Ni tofauti na sisi. Mwanafalsafa Charles Montesque aliyeasisi nadharia ya mihimili mitatu ya dola alikuwa na maana pia ya kumpunguzia Rais nguvu nyingi. Wakati huo huo alitaka kuongeza nguvu kwa Bunge na Mahakama. Katika nchi zetu hizi, unapozungumzia kuliongezea nguvu Bunge na Mahakama, ina maana pia ya kutoa tafsiri ya kuipunguzia nguvu Serikali na kwa maana hiyo kumpunguzia nguvu Rais.

Hilo la mwisho ndilo hufanya nchi zetu hizi siku zote zibaki zikipiga makitaimu, ziko pale pale. Na hapo ndipo kilipo kiini cha matatizo mengi ya nchi zetu za Kiafrika. Afrika kujenga hoja za kumpunguzia nguvu za kimamlaka ‘Bwana Mkubwa' maana mara nyingi Afrika Marais ni wanaume, yaweza kuwa ni kujitafutia balaa.

Kama tuna dhamira za kweli za kuviandalia vizazi vijavyo mazingira mazuri ya kuishi, kuifurahia na kujivunia nchi yao, basi, tuna lazima ya kuandaa mazingira ya kuwapo kwa Mkutano wa Kitaifa wa Katiba. Mkutano utakaojumuisha viongozi wa makundi yote ya jamii hii. Hapo yaandaliwe mazingira ya kuandikwa kwa Katiba mpya itakayokuwa na maslahi kwa Watanzania walio wengi, na kwa miaka mingi ijayo.

Nitakuwa mtu wa mwisho kuamini, kuwa tiba ya maradhi yetu tuliyoyatambua, ikiwamo ufisadi uliotamalaki, ni kuendelea kuumiza vichwa kufikiri jina la nani atakayekuwa rais 2015. Huko ni sawa na kuendelea kutwanga maji kwenye kinu.Rai yangu; Watanzania msijiulize, nani atakuwa Rais 2015, Jiulizeni, Rais tunayemtaka 2015 tutampata kwa Katiba ipi, na kwa mfumo gani wa Uchaguzi?
Na hilo ni Neno la Leo.

Maggid,

Iringa,
Jumapili, Novemba 14, 2010
mjengwa
 
Ndahani

Platinum Member
Jun 3, 2008
18,114
8,994
Maggid,
Hata kama mbio za urithi wa urais hazionekani waziwazi, kwa maadili ya sasa na siasa zetu za mizengwe zilivyo, nyuma ya pazia kutakuwa na mashindano makubwa. Time will tell all that.
 
maggid

JF-Expert Member
Dec 3, 2006
1,084
1,246
Ndahani,
Ahsante sana.
Hoja yangu ya msingi ni KATIBA.
 
HISIA KALI

JF-Expert Member
Oct 26, 2010
694
108
Suala la Katiba na utaratibu mzima wa uchaguzi ni kitu muhimu sana. Mimi niko tayari kupiga kura ya mapendekezo ya katiba mpya kuliko kupiga kura ya kumchagua rais mwaka 2015. Najua rais mwisho wake ni miaka mitano ila katiba ni kitabu ambacho kitaweke misingi ya mambo mengi kwa faida ya Taifa la leo na siku za mbele.
 
Hisia Kali,
Unachosema ni cha msingi sana. Kura ya Mapendekezo ya Katiba Mpya itakuwa na maana kubwa kwa mamilioni ya Watanzania kuliko ' maagizo' haya ya chaguzi zetu za sasa. Mathalan, Hatuna Tume Huru ya Uchaguzi, na bado kuna vyama vinaingia kwenye chaguzi vikiwa na ndoto ya kutwaa madaraka ya nchi. Huko ni sawa na sisi Simba tukubali kwenda kucheza mechi na Yanga uwanja wa Kaunda Jangwani. Kisha Yanga watwaambie watani zao; kuwa refa wa pambano wameshamwandaa. Kama hapo kuna Simba mwenzetu atakayetarajia tutoke Jangwani na ushindi, basi, huyo ni Simba kichaa!
 
TIMING

JF-Expert Member
Apr 12, 2008
22,951
8,843
Kwa upeo wa "wenye nchi kwa sasa"... KATIBA ITABAKI HIYO HIYO, Unless tuwapeleke warsha na shule kuenya ili waelewe nini maana ya katiba
 
Nyambala

JF-Expert Member
Oct 10, 2007
4,465
1,165
Ndahani,
Ahsante sana.
Hoja yangu ya msingi ni KATIBA.

Katika vitu vilivyoniacha mdomo wazi kuhusu katiba yetu ni pale JK alipokuwa akisubiri matokeo ya uchaguzi lakinni at the same time anahudhuria kuapishwa uraisi kwa Dr. Shein (ambaye sijui hata kama alijiuzulu umakamu) akiwa kama raisi wa JMT. Hili suala mpaka sasa silielewi elewi kabisa!
 
MwanaHaki

R I P
Oct 17, 2006
2,401
704
Ndugu zangu,

KATIKA kuadhimisha miaka kumi ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi, CCM na miaka 20 ya Azimio la Arusha, Mwalimu Julius Nyerere alikubali kufanya mahojiano ya kipekee na ya aina yake na Mhariri wa gazeti la Uhuru. Huo ulikuwa ni mwaka 1987.

Katika mahojiano yale Mwalimu, akiwa Mwenyekiti wa CCM hakusita kutamka bayana, kuwa Chama alichokuwa akikiongoza kilikuwa na kasoro na mapungufu mengi.

Mwalimu aliona dalili za kupungua kwa moyo wa kujitolea. Aliona dalili za kupungua kwa maadili ya uongozi. Mwalimu aliona dalili za mioyo ya kimamluki ilivyoanza kuingia na kuenea ndani ya CCM na nchi yetu. Mwalimu alifikia kumtamkia mhariri yule wa gazeti; “ Tumewapa uongozi watu wasiofaa. Nadhani wengi ndani ya Chama tumeanza kuutambua ubovu huu. Hatua ya kwanza kutibu maradhi ni kuyatambua.” Alitamka Mwalimu.

Ndio, Mwalimu aliona mbali, hii leo viongozi wanaofanya matendo maovu na ya kimamluki ndani ya vyama vya siasa na nchi kwa ujumla ndio wale aliowatabiri Mwalimu miaka 23 iliyopita.
Ni dhahiri, kuwa demokrasia yetu bado ni changa mno. Huu ni wakati wa kuwa makini katika kujenga misingi imara ya demokrasia yetu.Makala yangu ( Raia Mwema) juma la jana ilizungumzia amani. Nilirejea kauli ya ya Mwadhama Kardinali Polycarp Pengo juu ya suala hilo. ( Mwananchi, Novemba 5, 2010)

Mwadhama Kardinali Pengo alizungumzia umuhimu wa uwepo wa amani. Katika makala yangu hayo nilikwenda mbele zaidi. Nilibainisha, kuwa pasipo haki hakuna amani. Na swali ni je, haki inapatikana vipi?

Hivyo, nikaongeza kuandika, kuwa swali tusilopaswa kujisumbua kujiuliza ni juu ya nani atakuwa Rais wetu mwaka 2015, bali, tujisumbue kwa kujiuliza; Je, Rais wetu wa 2015 tutampata kwa katiba ipi, na kwa mfumo gani wa uchaguzi? Sote, wakiwamo viongozi wa dini, tuna lazima ya kuyatafuta majibu ya maswali haya.

Kwa mfano, wenzetu kule Marekani katiba yao ina zaidi ya miaka mia mbili. Kubadili kipengele tu katika katiba ya Marekani inaweza kuwa ni mchakato wa miaka kumi. Hakuna hata Rais wa Marekani anayeweza kuichezea Katiba ya Marekani kwa maslahi yake, anaweza kuishia gerezani anayejaribu kufanya hivyo. Wamarekani wale hata wakimweka ‘mwendawazimu’ Ikulu wanajua namna ya kumdhibiti kikatiba.Ni tofauti na sisi. Mwanafalsafa Charles Montesque aliyeasisi nadharia ya mihimili mitatu ya dola alikuwa na maana pia ya kumpunguzia Rais nguvu nyingi. Wakati huo huo alitaka kuongeza nguvu kwa Bunge na Mahakama. Katika nchi zetu hizi, unapozungumzia kuliongezea nguvu Bunge na Mahakama, ina maana pia ya kutoa tafsiri ya kuipunguzia nguvu Serikali na kwa maana hiyo kumpunguzia nguvu Rais.

Hilo la mwisho ndilo hufanya nchi zetu hizi siku zote zibaki zikipiga makitaimu, ziko pale pale. Na hapo ndipo kilipo kiini cha matatizo mengi ya nchi zetu za Kiafrika. Afrika kujenga hoja za kumpunguzia nguvu za kimamlaka ‘Bwana Mkubwa’ maana mara nyingi Afrika Marais ni wanaume, yaweza kuwa ni kujitafutia balaa.

Kama tuna dhamira za kweli za kuviandalia vizazi vijavyo mazingira mazuri ya kuishi, kuifurahia na kujivunia nchi yao, basi, tuna lazima ya kuandaa mazingira ya kuwapo kwa Mkutano wa Kitaifa wa Katiba. Mkutano utakaojumuisha viongozi wa makundi yote ya jamii hii. Hapo yaandaliwe mazingira ya kuandikwa kwa Katiba mpya itakayokuwa na maslahi kwa Watanzania walio wengi, na kwa miaka mingi ijayo.

Nitakuwa mtu wa mwisho kuamini, kuwa tiba ya maradhi yetu tuliyoyatambua, ikiwamo ufisadi uliotamalaki, ni kuendelea kuumiza vichwa kufikiri jina la nani atakayekuwa rais 2015. Huko ni sawa na kuendelea kutwanga maji kwenye kinu.Rai yangu; Watanzania msijiulize, nani atakuwa Rais 2015, Jiulizeni, Rais tunayemtaka 2015 tutampata kwa Katiba ipi, na kwa mfumo gani wa Uchaguzi?
Na hilo ni Neno la Leo.

Maggid,

Iringa,
Jumapili, Novemba 14, 2010
mjengwa

Tayari amepatikana, na hatoki kwenye kundi la Chama Cha Mafisadi! Wala sio Dk. Slaa!
 
Dr Matola PhD

JF-Expert Member
Oct 18, 2010
49,287
67,659
Ndahani,
Ahsante sana.
Hoja yangu ya msingi ni KATIBA.

HIVI WAKATI UNATUMIWA NA CCM, HAUKUJUWA KAMA KUNAITAJIKA KATIBA MPYA?:nono: MAANDIKO MATAKATIFU YANASEMA HIVI: HERI UWE MOTO AU BARIDI, KULIKO KUWA VUGUVUGU MAANA NITAKUTAPIGA. SHAME ON YOU, MMESHATUMIWA KAMA MIPIRA, WENZENU MISSION ACCOMPLISH WAKO CHAKO NI CHAKO SAA HIZI WANAKULA MIMBUZI CHOMA, WEWE MTOTO WA KIUME UNAKUJA KUTUBANIA PUWA NA HOJA ZA KIZANDIKI! MNAFKI MKUBWA WEWE.:rip::rip::rip:
 
njiwa

JF-Expert Member
Apr 16, 2009
12,042
4,961

mkuuu vipi..? mbona umetoka nje ya hoja na kushambulia mtoa mada
 
ZeMarcopolo

JF-Expert Member
May 11, 2008
14,011
7,195
HIVI WAKATI UNATUMIWA NA CCM, HAUKUJUWA KAMA KUNAITAJIKA KATIBA MPYA?:nono: MAANDIKO MATAKATIFU YANASEMA HIVI: HERI UWE MOTO AU BARIDI, KULIKO KUWA VUGUVUGU MAANA NITAKUTAPIGA. SHAME ON YOU, MMESHATUMIWA KAMA MIPIRA, WENZENU MISSION ACCOMPLISH WAKO CHAKO NI CHAKO SAA HIZI WANAKULA MIMBUZI CHOMA, WEWE MTOTO WA KIUME UNAKUJA KUTUBANIA PUWA NA HOJA ZA KIZANDIKI! MNAFKI MKUBWA WEWE.:rip::rip::rip:

ni mgeni, unastahili kuonywa.
 
Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
14,818
29,267
HIVI WAKATI UNATUMIWA NA CCM, HAUKUJUWA KAMA KUNAITAJIKA KATIBA MPYA?:nono: MAANDIKO MATAKATIFU YANASEMA HIVI: HERI UWE MOTO AU BARIDI, KULIKO KUWA VUGUVUGU MAANA NITAKUTAPIGA. SHAME ON YOU, MMESHATUMIWA KAMA MIPIRA, WENZENU MISSION ACCOMPLISH WAKO CHAKO NI CHAKO SAA HIZI WANAKULA MIMBUZI CHOMA, WEWE MTOTO WA KIUME UNAKUJA KUTUBANIA PUWA NA HOJA ZA KIZANDIKI! MNAFKI MKUBWA WEWE.:rip::rip::rip:

Siku itakapotokea kukawa na tangazo kutoka kwa mungu kuhusu watu kwenda peponi ninahakika wapo baadhi yetu watapinga.!!! ndiyo demokrasi anyway.
Tulishakuwa na mjadala hapa kuhusu mada kama hii, nami nilikuwa upande wa kile nilichokiita ''level field''. Anachosema maggid kina mantiki, kama si kukosa level field huenda leo matokeo tunayoaminishwa kuwa ya kweli yangekuwa tofauti. Labda tutumie akili zetu ndogo kufikiria kuwa unapoliwa mahindi yako shambani na ngedere halafu mwendesha mashitaka akawa nguruwe na hakimu akiwa nyani unategemea nini.
Tufikirie Msajili wa vyama anateuliwa na rais, mwenyekiti wa tume rais, viongozi wa vyombo vya usalama- Rais,na hawa wote wanawajibika kwa rais na wala hawathibitishwi na mtu au chombo chochote kile, sijui wanawezaje kwenda kinyume na maagizo ya bosi wao. Uaminifu huo upo kwingine lakini si Africa.
Kama ungeniuliza baada ya uchaguzi vyama na taasisi pamoja na sisi sote tufanye nini, jibu langu ni kuwa na KATIBA mpya tuliyoiandaa wenyewe kwa kuzingatia hali na matakwa yetu na si ile tuliyoiazima kwa mwingereza tukabadilisha majina na vipengele kadhaa. Katiba yetu kama sheria mama ina utata sana na ndiyo maana kila siku kunazuka maswali, ndiyo maana kila siku watu wanaweza kuwa na nchi yao n.k.

Kama hatutabadilika na kutengeneza kitu kitakachotuwajibisha sote kama wana wa taifa hili tutabaki kulalama kwasababu madaraka na uongozi wote wa nchi upo kwa mtu mmoja. Leo scandal za richmond n.k kama ni India, Marekani au Uk zingemalizwa na bunge. Mfano mzuri ni wakati waziri mkuu amejiuzulu, hakuwajibishwa na rais ambaye ni rafiki yake, bali umma kwa kupitia bunge. Kama Jaji mkuu, mkuu wa polisi, msajili wa vyama, tume ya uchaguzi vingekuwa vinawajibika sehemu nyingine leo tungewauliza madudu ya uchaguzi yalikuwaje. Lakini kwa vile wanawajibika kwa rais ambaye ni mwenyekiti wa CCM nani atawahoji au kuwauliza.

Fikiria, tume ya uchaguzi ilikaa kimya wakati wanafunzi wanazuiwa kupiga kura kwa kuchelewesha kufungua vyuo, leo tukiwauliza Tume kwanini wapiga kura walikuwa 47% Tume inasema haijui labda ufanyike utafiti! Si kwamba haijui bali inaogopa kutamka maneno yatakayomuudhi mzee.
Kama hatutabadilika na kudai katiba ambayo ni mkataba wa wananchi na serikali yao, wataendelea kuchaguana kwa kulindana kama tulivyoona dodoma. Kundi lenye nguvu ya fedha litaendelea kutuchagulia viongozi ili kulinda maslahi yao.
Tufikirie anachosema maggid hata kama hatukubaliani basi tusikubaliane kwa hoja zenye mantiki.
 
Derimto

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
1,307
303
Hisia Kali,
Unachosema ni cha msingi sana. Kura ya Mapendekezo ya Katiba Mpya itakuwa na maana kubwa kwa mamilioni ya Watanzania kuliko ' maagizo' haya ya chaguzi zetu za sasa. Mathalan, Hatuna Tume Huru ya Uchaguzi, na bado kuna vyama vinaingia kwenye chaguzi vikiwa na ndoto ya kutwaa madaraka ya nchi. Huko ni sawa na sisi Simba tukubali kwenda kucheza mechi na Yanga uwanja wa Kaunda Jangwani. Kisha Yanga watwaambie watani zao; kuwa refa wa pambano wameshamwandaa. Kama hapo kuna Simba mwenzetu atakayetarajia tutoke Jangwani na ushindi, basi, huyo ni Simba kichaa!

Bwana Majid kama vitu watanzani huwa tumelogwa ni kutokuona mbali jaribu kuangalia historia ya nchi kuaanzia sisi wenyewe,waajemi,wajeruman na mpaka Mwingereza halafu jaribu kutafuta wao wanaendeshaje nchi zao hasa Uingereza yenyewe ambapo wao walitutawala mwishoni tuchukua mambo mengi kwao lakini mengine yakaachwa kwa mfano wao wana Malkia Elizabeth ambaye ana last say na ndiye anaweza kupangua kitu chochote kama PM. Ataharibu mambo na vyombo vya ulinzi na usalama vanaheshimu haki za raia na mali zao na mambo yanaenda vizuri.

Tukirudi hapa kwetu ndiyo unakutana na mfano wako hapo juu lakini siyo kwamba tunashindwa kufanya mabadiliko kama baadhi ya tume zikaundwa na wabunge kutoka vyama mbalimbali maana ndiyo wawakilishi wa wananchi na wakafanya kazi kama ilivyofanyika kwenye Richmond na kwingine ila tatizo kubwa ni matokeo yake yatakuwaje na hapo ndipo utakapoona jinsi watu wanavyoogoa vivuli vyao kama ilivyotokea ya Richmond.

Kwa kifupi bado tuna sanaa nyingi sana na hatuwezi kutoka hapa kwa kuyatazama mambo kwa upana zaid na wabunge waelewe kuwa wametumwa na wananchi na siyo chama hivyo wananchi wanaweza kuchagua mbuge wa chama chochote kwa ajili ya kuangalia uwezo wake wa kutetea masilahi ya Taifa kama tulivyoona baadhi ya majimbo mwaka huu mfano Mramba amepeleka maendeleo jimboni kwao kwa nguvu sana lakini wananchi wake pia wameona alikuwa analipeleka wapi Taifa wakafanya maamuzi magumu
 
Dr Matola PhD

JF-Expert Member
Oct 18, 2010
49,287
67,659
ni mgeni, unastahili kuonywa.

NAKUBALI MIMI NI MGENI, LAKINI WEWE NI MWENYEJI UNAEHITAJI KUELIMISHWA, NIKO TAYARI KUMPONGEZA MALARIA SUGU MAANA, YEYE AMEJIPAMBANUWA KWAMBA YEYE NA CCM DAMDAM, LAKINI SI WANAFKI WATU WA CATEGORY YA MAGGID MJENGWA, HUYU YEYE NA MICHUZI, BLOGU ZAO NDIO ZILIKUWA TARUMBETA ZA PROPAGANDA ZA CCM. HAYA WENYE MALENGO YAO WAMESHAYATIMIZA, HALAFU MNAFKI HUYO HUYO TENA, ANAKUJA HAPA KUBANA PUWA ETI KUNAITAJIKA KATIBA MPYA! SHAME ON MAGGID. SASA NIMEAMINI KAULI YA JENERALI, SIO WOTE NI WAANDISHI INGAWA WANATUMIA KALAMU, LUGHA RAISI NI KWAMBA HAWA NI MAKUWADI, NA KALAMU NDIO MTAJI WAO. HUYU MAGGID SASA HIVI NIMESHAMWINGIZA KWENYE ORODHA YA KINA MANYERERE JACKTON, DEODATUS BALILE NA MZEE YUSUF HALIMOJA. WAKO WENGI HAO NI KWA UCHACHE TU.:rip:
 
Henge

JF-Expert Member
May 14, 2009
6,933
1,509
Katiba kweli nitatizo kuna mambo mengi sana ambayo katiba inafaa iyajibu!
Ukiangalia suala la MUUNGANO katiba inakinzana na katiba ya zanzibar, mfano raisi wa zanzibar akitoka kimataifa atajulikana kama nani??? Ninachojua kipindi cha Nyuma raisi wa zanzibar alikuwa ni makamu wa kwanza wa raisi wa Jamhuli ya muungano wa TZ. na kama akitoka kimataifa anajulikana kama makamu wa kwanza wa raisi wa TZ, kwa sasa sielewi inakuwaje!?
Mi nadhani katiba wa tz inamatatizo mengi sana!
 
FuturePresident

JF-Expert Member
Nov 9, 2010
321
53
Wapo watu walishalioona hili kwa muda mrefu sanaaaa......mwanzo kabisa wa kuanzishwa kwa vyama vingi, na walipigakelele kwa sana...lakini hatacjui waliishia wapi?? Lakini wakati Dr Slaa anajinadi alisema wazi kuwa kama angechaguliwa 2015 tungefanya uchaguzi kwa katiba Mpya...sasa ndiyo hivyo teenaa...yaleyale nini nikanyike sasa maana hawa jammmaaa wameshika kwenye mpinni wao kwao....ndiyo sehemu muhimu sana sana yakuzidi na kuzidi kutawala na sio kuongoza....Nini kifanyike? Nani afanye? Wapi pakuanzia? Nani wa kuanzisha?..........:cool:
 
Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
4,525
1,521
Unafikiri CCM wapo tayari kuanzisha mchakato wa kubadili katiba? Na swala la kuunda Tume huru ya uchaguzi hawa CCM wapo tayari?

Fidel,

Nadhani hapa suala wala lisiwe kuwataka CCM, bali ni kuwalazimisha. Nitatoa mfano. Siku ile ya tarehe mbili, nilipigiwa simu na kuelezwa tatizo la kura za Urais, nikatoa ushauri huu
Pettition at High court to: a. stop NEC from declaring the winner of presidency of URT.b. suspend announcing and counting all presidential vote count. c. demand all ballots announced should be reounted by independent body. This should be 1st thing in the morning tomorrow.
Pamoja na kuwa Kikatiba na Sheria ya uchaguzi vinasema akishatangazwa Rais hakuna kubadili matokeo, lengo la kujibu kwa aliyepiga simu ilikuwa ni kuwaambia wafikishe mahakamani kesi kusimamisha mchakato kama ulivyokuwa unaendelea. Sasa hata kama tungesema kisheria na kikatiba hatuwezi kufanya hivyo, lakini ile nia na hata kufikisha kesi mahakamani, iwe ni premise kwa ajili ya kuleta kesi ya kikatiba.

Tayari tumeshaona jinsi mahakama kama mhimili ilivyovurunda mambo. Kwenye kesi ya Mtikila ilidai haina uwezo wa kupinga kitu kwa kutumia katiba (or something like that) wakasema ni jambo ala kurudishwa bungeni, kwenye kesi ya Costa Mahalu, wametoa hukumu kudai kuna kasoro kikatiba.

Then you have to ask yourself what do we need to do to correct this?

Hivyo suala si kuisubiri CCM ifanye hilo, balki ni sisi Watanzania na vyama vya Upinzani kuanza huo msukumo wa kudai mabadiliko kwa manufaa ya Taifa na si kufanya vitu ili kuinufaisha CCM.
 
0 Reactions
Reply
Top Bottom