Neno La Leo: " Kwenye Maji Bwelele, Mpumbavu Hushinda Na Kiu..!"

maggid

Verified Member
Dec 3, 2006
1,084
1,500
Ndugu zangu,

Nimepata kuandika, kuwa NCHI yetu imo mwanzoni kabisa mwa vita vya kweli kweli vya kupambana na panya ( Mafisadi) waliokuwa wakiitafuna hazina yetu.

Fikiri, mwandishi wetu mahiri wa riwaya za upepelezi angelikuwa hai leo. Bila shaka, angemwona Willy Gamba katika Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa, na kwa maelekezo ya Mkuu wake wa operesheni anavyofichua ' Njama' za kuliangamiza taifa.

Kisha, Willy Gamba angemwona Jemedari Mkuu, Rais wa Nchi, anavyochukua mwenyewe jukumu la kuongoza ' Kikosi Cha Kisasi' kupambana na waliotujeruhi kama taifa, kuhakikisha nao wanakiona cha mtema kuni.

Nchi yetu iko sasa kwenye hatari ya kukumbwa na laana ya rasilimali. ( Resource Curse). Mabepari wanazinyemelea rasilimali zetu, tena kwa hila. Tumeanza sasa kugombanishwa http://www.africablogging.org/fires-around-mineral-rich-gr…/kwa urithi tulioachiwa na wahenga wetu. Ni rasilimali zetu; gesi, mafuta, madini na wanyamapori wetu. Kwa mfano, tumeshaambiwa na imethibitishwa, kuwa tuna hazina ya gesi bwelele.

Kuacha rasilimali zetu ziwafaidishe matajiri na watu wetu wabaki kuambulia makombo si ujinga, bali ni upumbavu anaouzungumzia Msanii Bob Marley, kwamba kwenye maji bwelele ni mpumbavu ndiye anayeshinda na kiu.

Ona kwenye eneo la nishati. Tuna ugomvi mkubwa. Makampuni ya kigeni yanakuja na yanashindana hata kwa hila ya kutugombanisha.

Tunakusanyaje kodi kutoka kwenye makampuni hayo?

Tunataka sasa viongozi wazalendo wa kweli watakaosimama kidete kutetea yale yaliyo na maslahi kwa wengi. Na wala wasijifanye watetezi wa wanyonge ili hali nao wanatanguliza tamaa ya kujikwapulia vitalu kwa kisingizio cha uwekezaji.

Kumbe, wanataka kuhodhi ili nao waje kuongeza mitaji yao. Kwamba nao ni mabepari wenye kujali mitaji yao. Katika dunia hii hakuna tofauti ya unyonyaji.

Kwa Mtanzania kunyonywa na Mzungu au Mtanzania mwenzake matokeo ni yale yale. Kunyonywa ni kunyoywa tu, haijalishi ni mrija mweupe au mweusi.

Ndugu zangu,

Tujiadhari pia na wakubwa kutuwekea viongozi wanaowataka wao ili wawatumikie. Kutuwekea vibaraka wao. Wamefanya hivyo huko nyuma. Sasa iwe Kikomo.

Ona ilivyokuwa kwa Tanesco; Ilianza na Baffour Beatty, Net Group Solutions, IPTL, Mechmar, Agreko, Songas, Richmond, Dowans na hata wakaja Symbion. Ni kama mbio za panya zenye kuishia ukutani. Kwamba hatusongi mbele.

Na hakika, Bob Marley hakukosea alipoimba wimbo huu: Rat Race, mbio za panya.
http://www.youtube.com/watch?v=dCE3Ge4bCLk

"Political violence fill ya city, ye-ah!
Don't involve Rasta in your say say;
Rasta don't work for no C.I.A.
Rat race, rat race, rat race! Rat race, I'm sayin':
When you think is peace and safety:
A sudden destruction.
Collective security for surety, ye-ah!

Don't forget your history;
Know your destiny:
In the abundance of water,
The fool is thirsty.
Rat race, rat race, rat race!"- Bob Marley

Maggid .
 

Attachments

 • File size
  45.8 KB
  Views
  31

samurai

JF-Expert Member
Oct 16, 2010
7,547
2,000
Problem creator want to solve the problems..

Ni CCM ikiungwa mkono na wafuasi wake kuwaleta mabepari chini ya Benjamini Mkapa kama Rais wa awamu ya nne, bila shaka alikuwa akitimiza ilani ya CCM ndio maana hakuna mwanaCCM aliyepingana na hilo na hapa Mkapa alipigiwa makofi na kuitwa shujaa..

Mabepari aka wawekezaji walipingwa sana mpaka kupelekea kuwaita wasaliti wapingaji, mikataba mpaka ya 100yrs ilisainiwa hapa na wafuasi walewale wa CCM na viongozi wao walipiga makofi na kuwaona wengine wale waliopinga wasaliti..

Nionacho mimi ni usanii wa CCM unaendelea baada ya kushindwa kuwatoa watanzania kwenye umasikini kwa 55yrs sasa inatafutwa sababu itakayokuwa wimbo kwa kuvunja mikataba ya hovyo wakiosaini kihalali na hao mabepari na kuwaweka as watanzania pagumu..
 

papason

JF-Expert Member
Sep 14, 2010
3,504
2,000
dawa ni kuindoa ccm madarakan na 'kuwa restisha ini pisi' viongozi wake wote kwa usalama wa vizazi vijavyo!
 

Getang'wan

JF-Expert Member
Apr 9, 2015
1,936
2,000
CCM ndyo wametufikisha hapa tulipo alifu wanakaa kulalamika na kuitana ma jemedari uchwara
Lakini tunashindwa wapi kuwang'oa hawa? Nadhani wananchi tujitathmini pia sisi kwamba tunayo share kubwa katika haya yanayotokea. Tuliona na tunaona wakifanya na bado tunawaona mashujaa. Tunapaswa kuchukua hatua? Hatua ipi?
 

sergio 5

JF-Expert Member
May 22, 2017
8,719
2,000
Lakini tunashindwa wapi kuwang'oa hawa? Nadhani wananchi tujitathmini pia sisi kwamba tunayo share kubwa katika haya yanayotokea. Tuliona na tunaona wakifanya na bado tunawaona mashujaa. Tunapaswa kuchukua hatua? Hatua ipi?
Hatu nzuri ya kuiondoa CCM vyama vya upinzani vijijenge vijijini
 

Getang'wan

JF-Expert Member
Apr 9, 2015
1,936
2,000
Hatu nzuri ya kuiondoa CCM vyama vya upinzani vijijenge vijijini
Matumizi ya nguvu ya dola na propaganda chafu ambavyo ndo nguvu ya chama tawala huoni kama ni tishio kubwa sana kwa mstakabali wa ujenzi wa vyama vya upinzani vijijini? Nini kifanyike kukabiliana na hayo?
 

sergio 5

JF-Expert Member
May 22, 2017
8,719
2,000
Matumizi ya nguvu ya dola na propaganda chafu ambavyo ndo nguvu ya chama tawala huoni kama ni tishio kubwa sana kwa mstakabali wa ujenzi wa vyama vya upinzani vijijini? Nini kifanyike kukabiliana na hayo?
Ni kweli ni tishio lakn vyama vijitahdi kutoa elimu hata kidogo kuhakikisha wananchi wanakuwa na elimu juu ya upinzani maana vijiji mtu kuwa mpinzani ni kama kuwa muhalifu
 

Getang'wan

JF-Expert Member
Apr 9, 2015
1,936
2,000
Ni kweli ni tishio lakn vyama vijitahdi kutoa elimu hata kidogo kuhakikisha wananchi wanakuwa na elimu juu ya upinzani maana vijiji mtu kuwa mpinzani ni kama kuwa muhalifu
Nimekupata kiongozi. Elimu ya uraia ni ndogo sana. Lakini ninaamini kuwa siyo ni kwasababu ya udogo wa elimu ya uraia lakini pia nia halisi ya nchi na wananchi kuwa one massive force for development hakuna. Tumekalia siasa za kipumbavu za vyama. Halafu hata wale wanaoona wana favour ya system na chama chao bado ni waathirika wakubwa lakini hawafunguka macho na bongo. Sasa hivi tupo kama vijibwa vya siku moja hadi 3; hatujafunguka macho. Siku ya nne ya kufunguka macho imekaribia. Siku ambayo itakuwa ya muhimu mno kwa mstakabali wa taifa.
 

sergio 5

JF-Expert Member
May 22, 2017
8,719
2,000
Nimekupata kiongozi. Elimu ya uraia ni ndogo sana. Lakini ninaamini kuwa siyo ni kwasababu ya udogo wa elimu ya uraia lakini pia nia halisi ya nchi na wananchi kuwa one massive force for development hakuna. Tumekalia siasa za kipumbavu za vyama. Halafu hata wale wanaoona wana favour ya system na chama chao bado ni waathirika wakubwa lakini hawafunguka macho na bongo. Sasa hivi tupo kama vijibwa vya siku moja hadi 3; hatujafunguka macho. Siku ya nne ya kufunguka macho imekaribia. Siku ambayo itakuwa ya muhimu mno kwa mstakabali wa taifa.
nasisi pia mkuu tutumie Elimu hii ndogo tuliyonayo kusaidia katika hilo
 

Getang'wan

JF-Expert Member
Apr 9, 2015
1,936
2,000
nasisi pia mkuu tutumie Elimu hii ndogo tuliyonayo kusaidia katika hilo
Tupo pamoja kiongozi wangu lakini kuna watu watakushambulia kuwa wewe siyo sehemu yao, siyo mwenzao. Ni hapo tutakapokuwa tumepona huu ugonjwa ndo tutakombolewa. Bahati mbaya sana tutakuwa hatuna raslimali zetu za asili. Utakubaliana nami lakini pia unaweza kunipinga kuwa raslimali zetu ndo zimeyajenga mataifa yanayojinasibu kuwa ni makubwa duniani. Sisi huku waliokwisha kuuona mwanga kwenye tunnel ndo wanatufunga vitambaa vyeusi machoni halafu wanalia kwa sauti kubwa kuwa tumeumizwa. Halafu sisi ndo tuwaonee huruma na kuwaona mashujaa wakati hawatuondolei vitambaa vyeusi machoni.
 

Mdudu halisi

JF-Expert Member
May 7, 2014
2,730
2,000
Hivi mke wa Daudi Mwangosi alipewa rambirambi yake na huyu jamaa? Ni heri ya fisadi kuliko mtu anayedhulumu rambirambi.
 

maggid

Verified Member
Dec 3, 2006
1,084
1,500
Hivi mke wa Daudi Mwangosi alipewa rambirambi yake na huyu jamaa? Ni heri ya fisadi kuliko mtu anayedhulumu rambirambi.
Mdudu Halisi,

Sijawahi kudhulumu rambirambi katika maisha yangu, au kukukusudia kufanya dhuluma nyingine yeyote. Ushahidi wa risiti ya CRDB ya nilichokabidhi kwa mjane huo hapo chini na hivyo, kukanusha vikali tuhuma zako kwangu zisizo na chembe ya ukweli. Kama una lingine lenye ushahidi njoo nalo. Kama huna, ni heri ukae kimya tu. Ni hekima pia.

Nimeshatuhumiwa huko nyuma na nilipata kuandika haya kwenye ukumbi huu
..

.. UKWELI WANGU KUHUSU UTATA RAMBIRAMBI ZA MJANE WA MWANGOSI...

Ndugu zangu,

Cris Lukosi ameandika haya kwenye Jamii Forums jana...

"Nndugu zanguni

Naona kila kukicha makamanda wa chadema wamekuwa wakiendeleza ile singo yao ya rambi rambi dhidi yangu.

Huu wimbo umenikera sana na nadhani sasa ni wakati muafaka kwa Mchungaji Msigwa kujitokeza hapa na kutoa ufafanuzi ziliko hizo hela ambazo mimi nilizifikisha kwake kupitia Maggid Mjengwa

Sio vyema kwa kiongozi wa dini tena mbunge kukaa kimya kwenye suala kama hili.

Watu walitoa kwa moyo, hivyo ni vyema wajue hela zao kama zilifika au zilitumika kwenye mikutano ya pale mwembetogwa

JITAMBUE!"-

Mwingine amechangia...

"JF Senior Expert Member Array

Default Re: Namuomba Mchungaji Msigwa aje hapa kutueleza ziliko rambirambi za Mwangosi nilizompa.

Hapa kuna watu watatu wanaoujua ukweli wa nani ametafuna pesa za rambi rambi. Chris Lukosi, Maggid Mjengwa, au Mchungaji Msigwa. Lukosi anasema amekabidhi pesa kwa Mjengwa, sasa kama Msigwa anakanusha hakupewa pesa, basi pesa aidha zimeliwa na Lukosi au Mjengwa. Tunataka Maggid Mjengwa aje hapa athibitishe kama ni kweli alikabidhiwa pesa na Lukosi? Na yeye jee alizikabidhi kwa Msigwa?
Embu mwenye namba ya simu ya Mjengwa aiweke hapa tafadhali. " ( Chanzo JF)

Ukweli wangu:

Kwa kufuatilia mjadala kwenye mada hii mtandaoni nimeona dhahiri, kuwa wasionitakia mema wameanza hila za kuliingiza na kulichafua jina langu na rekodi yangu ya kujitahidi kuishi na kutenda yalo mema na kwa uadilifu. Na mengine si ya kuyapuuzia, maana kuna wenye kuamini upuuzi pia. Ndio sababu nimeamua kuweka ukweli wangu hapa...

Baada ya kuawa kinyama kwa rafiki na mwanafamilia mwenzetu katika tasnia ya habari, Daud Mwangosi, niliitisha harambee kupitia Mjengwablog ili kumsaidia mjane wa marehemu na watoto wake.

Yafuatayo yawe wazi;
1. Ni kweli kuwa Cris Lukosi kupitia nduguye Augustino Lukosi aliniingizia shilingi milioni moja kwenye akaunti yangu ya MPESA kama mchango wa rambirambi uliokusanywa UK kutoka kwa wanachadema Lukosi akiwa mwenyekiti wao.( Angalia siku, tarehe na muda kwenye kiambatanishi)
2. Kwenye orodha ya wachangiaji niliorodhesha mchango huo kama kutoka kwa Jumuiya ya Watanzania UK. Ni kwa vile kama mratibu, niliweka wazi kuwa suala hili la msiba na rambirambi halihusiani na itikadi za vyama.
3. Cris Lukosi hakukubaliana na utaratibu huo na kunitaka niwakilishe mchango wao kwa Mh. Peter Msigwa, Mbunge wa Iringa Mjini na uwakilishwe kwa mjane wa marehemu Mwangosi kama mchango kutoka kwa WanaChadema UK. Nilifanya kama alivyotaka Lukosi ( Ushahidi ni kiambatanisho hapo chini).

Hitimisho: Ukweli wangu ndio huo. Hakuna hata senti moja ya rambirambi kwa mjane wa marehemu Mwangosi iliyopotea mikononi mwangu. Na chini hapo ni risiti ya CRDB ikionyesha fedha zote zilizochangwa na nilizoziingiza kwenye akaunti ya Itika Mwangosi, mjane wa marehemu Mwangosi. Ushahidi wa majina ya waliochangia na kiasi walichochanga pia upo.

Nimeyaweka haya hadharani kwa nia njema ili kuzuia upotoshaji na hali ya kuchafuana majina kama ningeamua kubaki kimya.

Nawashukuru nyote mnaoendelea kuniamini hata mnaposikia yenye kuzushwa juu yangu.

Wenu Katika Ujenzi wa Nchi Yetu.

Maggid Mjengwa.
Iringa.
 

Attachments

 • File size
  54.8 KB
  Views
  16

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom