Neno La Leo: Kuvua Au Kutokuvua? Ni Swali La Kizushi ! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Neno La Leo: Kuvua Au Kutokuvua? Ni Swali La Kizushi !

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by maggid, Aug 18, 2010.

 1. m

  maggid Verified User

  #1
  Aug 18, 2010
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Na Maggid Mjengwa,

  Jana jioni jamaa mmoja wa Idara ya intelijensia ( Tanzania) aliniuliza swali la ‘ kizushi’ ; “E bwana nataka kuifahamu Jiografia ya hapa, hivi wewe unakaa nyumba ‘A’ au’ B’? ” Aliniuliza. Jamaa huyu amekaa mahali hapo kwa miaka 20. Anafahamu kuwa nakaa nyumba ‘ B’ na kuna siku alinitambia kwa kuniambia alichosikia kwenye mazungumzo yangu ya simu wakati akipita nje ya nyumba ‘ B’ ninayoishi, yalikuwa mazungumzo ya kawaida tu. Iweje leo aniulize swali hili? Nilijiuliza. Kila swali lina tafsiri yake. Usikimbilie kujibu swali kabla hujalitafsiri. Jamaa yangu huyu alitakla kujua kati ya mawili yafuatayo; Mosi, kama nitajibu nakaa nyumba ‘ B’ nitamwambia nani anakaa nyumba ‘ A’. Huenda kuna mtu ameingia nyumba ‘ A’ lakini hajamjua ni nani. Pili; anamfahamu anayekaa nyumba ‘ A’ lakini anataka kujua kama namfahamu jirani yangu huyo. Jibu langu likawa; ” Mimi nakaa nyumba ‘ B’ na bila shaka unafamhamu anayekaa nyumba ‘ A’ , ni fulani. Hilo la mwisho nilimaanisha pia kuwa alimfahamu anayekaa nyumba ‘ B’. Naam. Kuvua au Kutokuvua, ni swali la kizushi. Na hasa kama anayeuliza swali tayari ameshashika mshipi na ndoano yenye chambo! Na hilo ni neno la leo.

  Kwa kazi zaidi za Maggid, tembelea; mjengwa
   
Loading...