Neno La Leo: Kuna Tofauti Ya Mjinga Na Mpumbavu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Neno La Leo: Kuna Tofauti Ya Mjinga Na Mpumbavu!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by maggid, Mar 22, 2011.

 1. m

  maggid Verified User

  #1
  Mar 22, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Ndugu Zangu,


  KUNA tofauti ya mjinga na mpumbavu. Marehemu Mzee Jongo alipata kutamka; ” Kusoma sio kuufuta ujinga, bali ni kuupunguza”. Kila mwanadamu ana ujinga wa jambo moja au mia moja. Kuwa na ujinga wa jambo si kosa, hata Profesa anaweza asijue namna ya kuchochea kuni za kuchomea hindi bichi likachomeka. Kijana wa darasa la saba anaweza kuwa hodari wa jambo hilo kumshinda Profesa.


  Lakini upumbavu ni ile hali ya mwanadamu kufanya jambo isivyotakiwa huku akiwa na uelewa wa namna ya kufanya inavyotakiwa. Huo ndio upumbavu. Na ndio maana binadamu kuitwa mpumbavu ni tusi. Kuitwa mjinga si tusi, kila mmoja ana ujinga wake. Kuwa na ujinga wa jambo fulani ni kutoelewa jambo hilo. Ni nani anayeelewa kila jambo?


  Na mwanadamu unafanyaje unapoamka na kukuta dunia unayoishi ardhi yake imeanza kumegeka na kuchotwa na bahari? Kuna niliyemwuliza swali hilo. Naye akanijibu; ” Huo ndio utakuwa mwisho wa dunia!” Aliyenijibu alikuwa amechoka kufikiri. Nilidhani amgetamka, kuwa angeanza kujifunza kuogelea. Maana, kwa kuogelea majini angeweza kukutana na kisiwa, au nchi kavu.


  Wanadamu tumejaliwa akili ili tuweze kufikiri. Na kufikiri ndio njia mojawapo ya kuiteka kweli. Kufikiri kunahamisha milima na hata kuiweka kando kuruhusu mwanga upite. Inakuwaje basi mwanadamu anapoacha kufikiri? Na hilo ni Neno La Leo.  Maggid
  Iringa,
  Jumanne, Machi 22, 2011
  http://mjengwa.blogspot.com
   
 2. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #2
  Mar 22, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  hamna kitu humu. yale yale tu niliyofundishwa na marehemu bibi.

  ngoja nichek mabandiko mengine.
   
 3. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #3
  Mar 22, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  He! kumbe upo!! Kwani faidika na kampeni za ccm 2010 tayari imeisha..!? Nilikuwa napita tu.
   
 4. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #4
  Mar 22, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  tehe, tehe, tehe! Niptie na mimi twnde wte!
   
 5. Makindi N

  Makindi N JF-Expert Member

  #5
  Mar 22, 2011
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 1,068
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Vp Majjid umeambiwa mjinga/mpumbavu asbuhi hii au?
   
 6. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #6
  Mar 22, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,277
  Trophy Points: 280
  Hata mimi napita tu.
   
 7. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #7
  Mar 22, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Mkuu unaweza kuwa unarekebisha title zako?

  Maana haingii akilini ukisema NENO LA LEO

  NINI MAANA YA NENO LA LEO?
   
 8. m

  maggid Verified User

  #8
  Mar 22, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Kings, asante sana.

  Neno La Leo Ni Neno tu. Neno huru. Nimelitoa leo. Nawe umetoa Neno lako, leo, nalo ni Neno La Leo. Tutafakari Neno, basi!
   
 9. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #9
  Mar 22, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Sasa swtld huo uchokozi.
   
 10. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #10
  Mar 22, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  co uchokoz mkeshaji. Nmependa unavyopta, nkaona c vbya uknptia twnde wte! Sa hapo uchokoz uko wp?
   
 11. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #11
  Mar 22, 2011
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Majjid nasikia CCM wamekulipa mafao yako kwa kuwapigia kampeni vizuri na ninasikia wewe ndiyo uliyehamasisha vijana kinondoni waandamane kuunga mkono hotuba ya rais, sawa fanya vyovyote lakini kumbuka CDM tupo kwa ajili ya kuuwa wadudu wanaoruka na wanaotambaa,maana yangu tunapiga CCM, CUF pamoja na viroboto wengine
   
 12. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #12
  Mar 22, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Ujinga unatibiwa shuleni!

  Upumbavu unatibiwa hospitali ya vichaa!!
   
 13. Buswelu

  Buswelu JF-Expert Member

  #13
  Mar 22, 2011
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 1,989
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Mpumbavu Ni Mpumbavu Tu awe amesoma au hajasoma....same applies kwa Mjinga.
   
 14. wilchuma

  wilchuma JF-Expert Member

  #14
  Dec 24, 2015
  Joined: May 16, 2013
  Messages: 1,090
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  Ahahaha
   
Loading...