Neno La Leo: Kuku Ana Mabawa Na Miguu, Lakini Huteleza! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Neno La Leo: Kuku Ana Mabawa Na Miguu, Lakini Huteleza!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by maggid, Mar 22, 2012.

 1. m

  maggid Verified User

  #1
  Mar 22, 2012
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  [FONT=&amp]Ndugu zangu,[/FONT]

  [FONT=&amp]Ni nani hajawahi kuteleza? Sote tumepata kuteleza. Wengi wetu tumeteleza mara nyingi. Ndio maisha yalivyo. Muhimu kwa aliyeteleza ni pale anapoteleza kukubali kuwa ameteleza, basi.

  Kuku pamoja na kuwa na mabawa na miguu, lakini hutokea akateleza na kuanguka. Nimepata kushuhudia, si mara moja. Bila shaka nawe pia.
  [/FONT]


  [FONT=&amp]Naam, Rais Mstaafu, Mzee wetu Benjamin Mkapa majuzi aliteleza pale alipotamka hadharani kuwa Vicent Nyerere si mwanaukoo wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere. Ile ilikuwa ni kauli ya bahati mbaya ambayo haikupaswa kutolewa na mtu kama Mkapa.[/FONT]

  [FONT=&amp]Mzee Benjamin Mkapa aliteleza.[/FONT]

  [FONT=&amp]Na Vicent Nyerere pia akateleza pale alipomuhusisha Mzee Mkapa na kifo cha Baba wa Taifa. Makosa mawili hayafanyi moja likawa sahihi.[/FONT]

  [FONT=&amp]Na Afrika ukikuta jogoo wawili wanagombana, basi, hapo hapakosi mashabiki. Na kila shabiki aliyesimama kutazama mpambano wa majogoo hao, ujue, kuwa ana jogoo wake anayemshabikia. Na jogoo anayemshabikia akishindwa pambano, shabiki ataondoka akisononeka. Kuna ambao watakosa hata hamu ya chakula siku hiyo. Kisa? Jogoo wake kagalagazwa![/FONT]
  [FONT=&amp]
  Na kama jogoo mmoja ni mnene na mwingine ni mwembamba, ujue, kuwa jogoo mwembamba ana mashabiki wengi. Benjamini Mkapa ni jogoo mnene kwa Vicent Nyerere. Kuna wengi waliofurahia sana kuona jogoo mnene akigalagazwa. Na hasa zaidi kwa kuona kuwa jogoo mwembamba ndiye aliyechokozwa na jogoo mnene. Ndio kisa cha wengi ' kufumbia' macho rafu mbaya iliyochezwa na jogoo mwembamba kwa jogoo mnene. Ni kwa jogoo mnene kuhusishwa na kifo cha Baba wa Taifa.[/FONT]
  [FONT=&amp]
  Lakini, yote haya yanatokana na dhambi ya ubaguzi wa kisiasa. Na tujiulize; hivi, kama Vicent Nyerere angevaa mavazi ya kijani ya chama tawala kuna ambaye angethubutu kumtamkia kauli kama; kuhoji uhalali wake wa kuwa mwanaukoo wa Nyerere?[/FONT]

  [FONT=&amp]Hivi na siye tunaotamka kuwa Nyerere ni Baba wa Taifa tunajipendekeza kwenye ' Ukoo wa Nyerere?'. Kwamba sote ni watoto na wajukuu wa Mwalimu Nyerere.[/FONT]
  [FONT=&amp]
  Naam, kuku ana mabawa na miguu, lakini huteleza. Ni nani asiyeteleza? Na hili ni Neno La leo.[/FONT]

  [FONT=&amp]
  Maggid Mjengwa[/FONT]

  [FONT=&amp]
  Iringa.[/FONT]

  0788 111 765

  Mjengwa Blog::Habari,Picha,Matangazo
   
 2. Hassan J. Mosoka

  Hassan J. Mosoka JF-Expert Member

  #2
  Mar 23, 2012
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 647
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Mchezo wa siasa za majitaka ni mbaya sana huwezi kutarajia mtu kama Mkapa anaweza kufanya personal attack kwa huyu Kijana, but aliyoyafanya Mkapa ilikuwa ni kuonyesha jinsi ambavyo chama kinazama, Kuhusu Vicent kama asingesema kitu uongo wa Mkapa ungekuwa ukweli ingawa amemtupia mzee zigo atakalozunguka nalo kwa mda mrefu sana bila kulipatia usafi wa kkutosha. Wananchi wanataka suluhisho la matatizo yao sio Maigizo wanayofanya hao wanasiasa hapo Arumeru East
   
 3. B

  Bangoo JF-Expert Member

  #3
  Mar 23, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 5,594
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Ben mkapa ni mtu
  jeuri sana, lakini
  kwa hili la kifo cha
  mpendwa we2 ume
  chafuka mno. Utachu
  kiwa na wengi sana
  huna jinsi ya kujisafisha
  . Tunajua pengine
  ushapata shinikizo
  kwa taarifa hii,kwa
  hili 2najua uko ha
  tarini kufa kw presha
  DUNIANI HAKUNA
  SIRI.
   
 4. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #4
  Mar 28, 2012
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,696
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  Si busara waishio kwenye nyumba za vioo kutupa mawe hovyo. Siku wakirudishiwa inakuwa balaa. Ndiyo yaliyompata Mkapa. Kama Vincent Nyerere ameteleza hakuanguka kwa kuwa amepata mashiko.
   
 5. m

  mwanakazi Member

  #5
  Mar 29, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 68
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Hapo penye red! huo ni unafiki, upambe na kujipendekeza. Kauli ya bahati mbaya??!! mbona ajaisahihisha!! au kuifuta? au kuomba radhi? wewe Magid sijui, nani kakwambia kuwa hiyo ilikua ni bahati mbaya?? ndio walivyo hao..wamebaki kutukana na kuropoka tu! wameishiwa....

  ...mimi ni hapo tu! pengine pote fresh!
   
 6. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #6
  Mar 29, 2012
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Maggid aka mwenyekiti kama tunavyokuita kulee kwenye uwanja wetu, Neno la leo linanikumbusha stori ya 'KIFAFA "pileptic seizure disorder" CHA TAJIRI KUITWA KIZUNGUZUNGU (DIZZINESS)'

  Sikubaliani na wewe kuwa Mkapa alitereza, na kama kweli kateleza basi huo tunaita ni MSELE (Kujitelezesha kwa ajili ya fun). Sidhani kama mtu aliyekuwa anapewa taarifa za kiintelijensia kila siku kwa muda wa miaka kumi anaweza ku-justify kuwa hakuwa na mens rea - "guilty mind" katika kutoa matamshi ya uongo jukwaani. Kwa Mkapa nasema vyovyote tutakavyo spin ila KIFAFA kitaendelea kuwa KIFAFA hata kama mgonjwa ni MFALME.
   
 7. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #7
  Mar 29, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Alikuwa anatania
   
 8. M

  Mkandara Verified User

  #8
  Mar 29, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Hata kukata gwala nako ni kuteleza?..ama kweli apendae haoni chongo.
   
 9. Mentor

  Mentor JF-Expert Member

  #9
  Mar 29, 2012
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 18,714
  Likes Received: 8,269
  Trophy Points: 280
  Hakuwa na maana hiyooo....
   
 10. Mwalimu

  Mwalimu JF-Expert Member

  #10
  Mar 29, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,475
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Yale yaleee....

  Ndio maana DC wa Ulanga anasema Askari kuchapa risasi na kuua wananchi kadhaa ni ajali kama waliyopata waimba taarabu!! Yaani hawa jamaa kila wakifungua midomo yao basi ni KICHEFUCHEFU tu...Dah!
   
 11. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #11
  Mar 29, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Usiusemee moyo "lady JADEE" Nina hakika wengi watamfariji Vicent Nyerere kuwa hakukosea , lakini ukweli utabaki pale pale tu kumtuhumu mtu kuwa kaua hakika inakuwa hata mwenyewe linamsuta, na kwa mila za kiafrika hilo hwa linamalizwa na vikao tena vya ndani ya familia kwa upande wa familia sasa sijui hili la nyerere litamalizwa vipi kwa sababu ameliambia taifa kuwa baba yake kauawawa. Hata kama taifa linachukua gharama kibao kwa ajili ya familia ya Marehemu akiwemo Vicent mwenyewe ni kazi bure kwa sababu Baba yao aliuawawa hata ikija madarakani Serikali ya Chama kingine bado doa liko pale pale ha dhambi hiyo haitashia hapo kama ambavyo marehemu mwenyewe alivyokuwa akisema, labda iwe kweli kwamba madai ya Vicent ni ya kweli la sivyo hiyo ni laana kwakwe hatakaa aikwepe.
   
Loading...