Neno La Leo: Kuhofiwa Au Kupendwa, Lipi Jema? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Neno La Leo: Kuhofiwa Au Kupendwa, Lipi Jema?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by maggid, Feb 15, 2011.

 1. m

  maggid Verified User

  #1
  Feb 15, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Ndugu Zangu,

  WaMisri wale hawakuchoshwa tu na Hosni Mubarak. Walichoshwa na mfumo mzima na hususan chama chao tawala. Ndio, tulishuhudia, kuwa jengo la kwanza kutiwa kiberiti na waandamanaji lilikuwa ni jengo la Makao Makuu ya Chama tawala cha nchi hiyo, NDP- National Democratic Party. Kilikuwa chama kikongwe na kilichoshika hatamu za uongozi.

  Kwa WaMisri, NDP kilikuwa ni chama walichokihofia hata katika maisha yao ya kila siku. National Democratic Party kwa maana ya Chama Cha Taifa Cha Demokrasia hakikuwa cha Taifa na wala Demokrasia ndani yake. Kilikuwa chama cha wateule wachache akiwemo mwana wa Hosni Mubarak aitwaye Gamal Mubarak aliyepewa cheo cha Ukatibu Mkuu na aliandaliwa na baba yake kumrithi madaraka ya Urais.

  Ni lipi jema kwa mtawala na chama; kuhofiwa au kupendwa? Mwingine angependa vyote, lakini haiwezekani. Na hilo ni Neno La Leo. Maulid Njema.

  Maggid,

  Iringa,
  Februari 16, 2011
  mjengwa
   
Loading...