Neno La Leo: Kiongozi Wa Nchi Haui Watu Wake, Gaddafi Amewaua, Hana Aibu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Neno La Leo: Kiongozi Wa Nchi Haui Watu Wake, Gaddafi Amewaua, Hana Aibu!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by maggid, Feb 27, 2011.

 1. m

  maggid Verified User

  #1
  Feb 27, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Ndugu Zangu,  KIONGOZI wa nchi haui watu wake, Moummar Gaddafi amewaua. Ndio, mchana wa jua kali, na bado anasimama, anadai ni kiongozi wa WaLibya, Gaddafi hana aibu.


  Anapostahili kusimama Gaddafi sasa si kwenye jengo la Ikulu ya Tripoli, bali Mahakama ya Kimataifa Ya Haki na inayoshughulika na Wahalifu wa Kivita, The Haag.  Baraza la Usalama la Umoja Wa Mataifa jana limepitisha azimio la kumwekea Gaddafi vikwazo vya silaha na kugandisha amali zake. Inasemekana, Gaddafi ana akaunti za mabilioni ya dola za KiMarekani. Kumwekea Gaddafi na familia yake vikwazo ni msaada mkubwa kwa watu wa Libya kwa sasa.


  Kosa kubwa kabisa alilofanya Gaddafi kwa WaLibya ni KUWAKANDAMIZA. Ndio, kuwanyima UHURU. Gaddafi aliwafanya WaLibya kama ng'ombe kwenye zizi. Waliotoa sauti kumpinga aliwakamata na ‘kuwachinja', kimyakimya.  Libya ikawa mali ya Gaddafi na familia yake. Wanaodai haki yao sasa anaowaona kuwa ni majambazi wanaovamia nyumba yake. Kumbe! Jambazi mkubwa kwa WaLibya alikuwa ni Gaddafi na familia yake. WaLibya, kama wenzao wa Tunisia na Misri, wameamka. Hawatalala tena mpaka Gaddafi na familia yake wameondoka madarakani.


  Naam. Gaddafi bado anang'ang'ania madarakani. Ameshindwa kusoma alama za nyakati, kabla na sasa. Ninavyofuatilia yanayoendelea Libya na ulimwengu mzima wa WaArabu, naziona kila dalili, za Gaddafi kutomaliza hata wiki moja kutoka sasa akiwa madarakani.


  Gaddafi anatumia kila mwanya na hila, kujaribu kuurudisha nyuma mshale wa saa ya mabadiliko. Huko ni sawa na kulizuia wimbi la bahari kwa mikono. Hakika, WaLibya hawastahili tena kuongozwa na mtu kama Gaddafi. Ni Gaddafi huyu wa sasa, amewadhalilisha watu wake mbele ya macho ya walimwengu, anaendelea kufanya hivyo.


  Si tumeona Ijumaa jioni , amesimama na kuwaambia WaLibya waendelee kuimba na kucheza! Gaddafi amepoteza mwelekeo na mguso wa hali halisi. Amepitisha viwango vyote vya ulevi wa madaraka, Gaddafi wa sasa anaonekana kama mwehu fulani aliyeshika bunduki na kupita mitaani. Gaddafi anatishia usalama wa WaLibya kwa mamilioni kwa kila siku anayoendelea kuamka akiwa madarakani.


  Tushukuru , kuwa Gaddafi hana silaha za kemikali wala nyuklia, maana, Gaddafi wa sasa, katika dakika za mwisho za kupoteza mamlaka, angeweza kufanya maangamizi makubwa kwa WaLibya na dunia. Kisingizio? Njama za Wazayuni, George Bush ( hata kama hayupo madarakani) na Osama bin Laden! Je, kuna namna nyingine ya kumtambua kama binadamu ni mwendawazimu?


  Kwa sasa Gaddafi ametengwa na dunia na hata baadhi ya marafiki zake. Huenda Gaddafi yuko tayari kufanya lolote lile kwa sasa, maana, hajui ni wapi salama pa kukimbilia. Hata kwa rafiki yake Mugabe kuna wanaojiandaa kufanya kama ya Tunisia na Misri.


  Na kule Saudi Arabia? Haiwezekani. Si ana ugomvi wa siku nyingi na mfalme. Na wala Gaddafi asingepata tabu sana kupata pa kukimbilia, lakini, ugumu anaoupata sasa ni wa kujitakia; kuwaua watu wake. Hata rafiki zake wanapata tabu kumwelewa kwa hilo, maana, wao bado wana chembe za aibu.


  Naam. Kiongozi wa nchi haui watu wake, Gaddafi amewaua, hana aibu. Na hilo ni Neno La Leo.
  Maggid
  Iringa
  Jumapili, Februari 27, 2011
  http://mjengwa.blogspot.com
   
 2. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #2
  Feb 27, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mkuu Maggid,
  Makala ni nzuri na inaeleweka vema, tatizo pale Libya ni kwamba Gaddafi hakuchaguliwa na wananchi hivyo SI KIONGOZI HALALI WA WANANCHI.
   
 3. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #3
  Feb 27, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  kote nakubali, lakini suala la kumfananishsa Osama bin ladena na Wazayuni ni kukebehi dini za watu.
   
 4. m

  maggid Verified User

  #4
  Feb 27, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Jerusalem,
  Asante sana,
  Ni wapi nimemfananisha Osama Bin Laden na Wazayuni? Nahofia umenielewa vibaya.
   
 5. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #5
  Feb 27, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280

  samahani, sikuona kama kuna mkato(,).

  alakini ingetosha tu kusema Bush na Osama.
   
 6. J

  JokaKuu Platinum Member

  #6
  Feb 27, 2011
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,815
  Likes Received: 5,144
  Trophy Points: 280
  Maggid,

  ..umeamua kumsema Kikwete kiujanja-ujanja?

  ..Kikwete naye si amejeruhi na kuua kule Arusha, tena mchana wa jua kali?

  ..how dare you, kumsema vibaya Ghaddafi?

  ..umesahau deni la mafuta aliyotusamehe?

  ..umesahau zawadi ya magari ya fahari aliyowapa Ikulu?

  ..umesahau misikiti aliyojenga Tanzania na Afrika Mashariki?

  ..How dare you, Maggid?!!!
   
 7. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #7
  Feb 27, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,163
  Trophy Points: 280
  Umemsahau Nyerere?
   
 8. Boflo

  Boflo JF-Expert Member

  #8
  Feb 27, 2011
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 4,394
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mbona alivyotoa mabilioni ya fedha kujengewa nyumba wahanga wa mafuriko morogoro hukutaja?? amabapo hata serekali yako imeshindwa!! Mbona misaada lukuki inayotolewa na Gaddafi kwa serekali yetu na Afrika nzima kwa jumla hukutaja? Wewe unayejifanya una uhuru sana, utabaki na njaa mpaka itakuua huku unajitamba kwa kubana pua...:- "oh wajameni mimi nina uhuru tanzania"
  "
   
 9. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #9
  Feb 27, 2011
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Mbona Kikwete aliuwa wale wanachama wa CHADEMA pale Arusha siku chache zilizopita, je tukubaliane kuwa hiyo pia ilimfutia sifa yake ya kuwa kiongozi wa nchi hii - angalu kiongozi wa mabavu kama ilivyo kwa Gadaffi.?
   
 10. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #10
  Feb 27, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,163
  Trophy Points: 280
  Nyerere aliua halaiki ya wa Tanzania ni na asiyejuwa hilo?
   
 11. m

  maggid Verified User

  #11
  Feb 27, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Joka Kuu,

  Mimi nimeyasema yangu, umetoa tafsiri ya nilichosema, nawe umeyasema yako. Na kuna wengine wenye yao. Si ndio maana ya Jukwaa Huru? Na hivi, Kiongozi asilaumiwe kwa vile katujengea misikiti na kutusaidia kuchimba makaburi yetu?

  Nakumbuka sana hotuba ya Mwalimu Nyerere redioni mwaka 1979. Nyerere alisema Ghaddafi amemtumia ujumbe Nyerere aondoe vikosi vyake Uganda ndani ya saa 24. Vinginevyo Ghaddafi angetuma ndege zake za kijeshi na askari kumsaidia ' Joka Kuu!' Nduli Idd Amin.

  Na Nyerere akakaidi, Gaddafi akatuma ndege na askari wake Uganda, wengi wa askari hao walikuwa wazee. Kwenye uwanja wa mapambano walikamatwa mateka kirahisi sana na wapiganaji wetu.

  Vita ilipokwisha, Nyerere na Gaddafi walifikia muafaka. Wazee wale wa Gaddafi wakarudishwa Tripoli. Tangu hapo Gaddafi na Nyerere wakawa marafiki. Na inasemekana, katika moja ya mazungumzo yao, Gaddafi alipata kumwuliza Nyerere amsaidie kwa nini. Nyerere akajibu; "Pale kijijini kwangu Butiama Waislamu wana shida ya msikiti wa kufanyia ibada zao." Gaddafi akatoa msaada wa kujengwa msikiti Butiama. Na kuna wanaodai Nyerere alikuwa mdini!
   
 12. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #12
  Feb 27, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Ya Gadhafi hayana tofauti na Arusha, utofauti ni idadi ya vifo!
   
 13. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #13
  Feb 27, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Ya Gadhafi hayana tofauti na Arusha, utofauti ni idadi ya vifo!
   
 14. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #14
  Feb 27, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,971
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Maggid shukrani Mkuu ujumbe umefika.
  Literally JK hawezi mfikia Gaddafi kwa unyama wa waziwazi ila ndani ya moyo wa JK ameshaua watu wengi kuliko Gaddafi kwa chuki aliyonayo dhidi ya wananchi ambao hawakumchagua, na hususani Wana CDM.

  Kwa hili la Gaddafi anamkaribia kwa karibu Milosovic na dalili zinaonyesha akicheza ataondolewa kwa nguvu na jumuhiya ya kimataifa na kama pia asiposoma vema ramani ingawaje amechelewa nachelea kusema yaliyomkuta Saddam Hussein yanaweza kumpata.

  Gaddafi ameikasirisha jumuhiya ya kimataifa na kuna uwezekana wa kuilazimisha kufanya maamuzi magumu kama ilivyofanyika Iraq. Ukweli uko very clear jeshi limemkataa na alitakiwa ajisalimishe na kuandaa viongozi wa mpito then akawaomba watange kuwa amejiuzulu kama alivyofanya Hosni Mubaraka. Kosa lake alifikiri katika kipindi hiki ubabe na wingi wa silaha unaweza kuzuia wananchi wasidai haki zao haswa pale ukandamizaji unapovuka mstari wa uvumilivu. Hali hii inapofikiwa akili za watu zinakuwa focused kwenye walichodhamiria kukibadilisha na miili inakufa ganzi kwa maumivu na hofu ya kufa hutoweka na ndio maana pamoja na mauaji aliyofanya still raia wanaruka maiti na kusonga mbele kudai haki yao.
   
 15. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #15
  Feb 27, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Kama Gaddafi anastahili kwenda the Hague kwa nini Mubarak asipelekwe.
  Libya wamekufa karibu 1000 au zaidi, Misri walikufa 300 na ushee.

  Hapa ndo unaona unafiki wa Marekani na nduguze....waanze na Mubarak na Ben Ali kwanza.
   
 16. s

  salisalum JF-Expert Member

  #16
  Feb 27, 2011
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 379
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Maggid,

  Za siku nyingi aisee? Umenena ndugu yangu. vijana tayari wako viungani mwa Tripoli leo. Kawapa silaha wananchi wachache waliofaidi kwenye mfumo wake. Kawaita watu wake ni panya na mende! Mtu wa ajabu sana huyu. Nishangaa sana Kikwete kumfanya kuwa rafiki yake.

  Huyu alimsaidia Amini kutuvamia, yeye hasa ndiyo membe na panya yale makubwa! Najisikia hasira sana kwa mtu kama huyu. Kama Tanzania ingekuwa imemepakana na Tanzania ninge-infiltrate kwenda kusaida wananchi wa Libya.
   
 17. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #17
  Feb 27, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 722
  Trophy Points: 280
  kwa jinsi nchi ilivyo sasa jk hana tofauti na gadafi
   
 18. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #18
  Feb 27, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Kiongozi wa nchi hauwi watu wake,hilo halina ubishi ila yaliotokea Linya ni tofauti kabisa,kama maandamano yalikuwa yakuisulubu utawala uliopo madarakani kwa njia za demokrasia ,waandamananji hao wasingepaswa kuchoma moto majumba ya serikali na kuvamia vituo vya polisi na vituo vua kijeshi na kuiba silaha ,hilo ni kosa ,mbona Misri au tuseme Wamisri hawakuteka vituo vya polisi ukiangalia hata polisi walishiriki katika kupambana na Wamisri waandamanaji ,lakini waandamanaji hawakuvamia vituo vya polisi zaidi ya kuchoma moto jumba la chama tawala.
  Gadafi anahaki ya kupigana na watu ambao wamepoteza muelekeo hata kama ni raia zake,kwa mfano yale maandamano ya CDM kule Arusha yalikosa baraka za serikali na ndio pakatokea yaliotokea.Hivyo Gadafi anatumia jeshi kupambana na maharamia ila kama unakumbuka Gadafi kasema yeye sio raisi kama wengi mnavyodhania nchi inawenyewe au Libya ina wenyewe.

  Sasa na nyie fanyeni maandamano afu mvamie vituo vya polisi na kijeshi na kuviteketeza kwa moto tuone.kama mtakubalika.
   
 19. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #19
  Feb 27, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  akili za benard membe. full propaganda. inakuuma sana kwa sababu alijenga misikiti ya misaada?
   
 20. j

  junior2008 JF-Expert Member

  #20
  Feb 27, 2011
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 528
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani unyama wa Gaddafi ni extreme na kwa sasa yuko desperate hakutegemea yamkute haya yanayoendelea na wapinzani wake wamesha control sehemu kubwa ya Libya ikiwemo Zawiyah iliyopo jirani kabisa na Tripoli.
   
Loading...