Neno La Leo: Katiba, Tukichagua Njia Ya Kushindana, Sote Tutashindwa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Neno La Leo: Katiba, Tukichagua Njia Ya Kushindana, Sote Tutashindwa!

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by maggid, Nov 12, 2011.

 1. m

  maggid Verified User

  #1
  Nov 12, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Ndugu Zangu:

  Mwanasiasa Zitto Zuberi Kabwe anaandika;
  ” Kama kuna jambo moja ambalo huunganisha Taifa ni KATIBA ya taifa hilo. Katiba huweka misingi mikuu ya nchi na namna ya kujenga na kuendesha Taifa. Hivyo, Katiba inapaswa kuwa ni matokeo ya mwafaka wa kitaifa kwenye masuala yote ya msingi ya nchi husika.” ( Zitto Kabwe, gazeti Raia Mwema, Nov 9-17, 2011)

  Kwa maandiko hayo ya Zitto Kabwe, Katiba yaweza pia kutafsiriwa kama Mkataba wa Kijamii- Social Contract . Na katiba iwe ni msingi wa utawala bora. Kwamba Katiba ni muafaka pia wa Serikali na Wananchi. Na hapa ndipo falsafa ya Shaaban Robert ya Merikebu na nanga inapokuwa na maana kwetu.


  Madai ya Watanzania kupata Katiba Mpya ni madai muhimu, ya haki na ya kihistoria. Nimepata kuandika, kuwa Watanzania wenye mapenzi na nchi yenu, msikae mkafikiri, kuwa madai ya kupata Katiba Mpya ni kazi nyepesi.

  Ni kazi ngumu sana, hata kama mnaowataka wawasaidie kupata Katiba hiyo ni Waafrika wenzenu na si wakoloni. Ilivyo Afrika, kwanza mtaletewa na walio kwenye mamlaka, ’Katiba Mpya’ iliyofanyiwa marekebisho madogo kwa maana katiba iliyoongezewa viraka. Haitapelekea mkawa na chaguzi salama.

  Kuna kuandamana na hata watu kufa kutakakofuatia. Kuna akina Ocampo wa Mahakama za Kimataifa watakaokuja kuwanyofoa wahusika wa vurugu zitakazopelekea mauaji ya raia. Kisha itakuja Katiba Mpya. Ni njia mbaya na ya kusikitisha, lakini inaepukika, kama kuna utashi wa kisiasa. Ndio, Afrika kudai Katiba Mpya yaweza kuwa ni kazi ngumu kuliko kudai uhuru kutoka kwa mkoloni.


  Nakumbuka, Prince Bagenda, Mwakilishi wa CCM kwenye Kongamano la Katiba pale Chuo Kikuu Mlimani alipata kukaririwa na gazeti la Mwananchi akitamka; ” Msifikiri kila kitu mnapewa tu, lazima mdai”. (Mwananchi Aprili 3, 2011). Ndio, Prince Bagenda alitamka; kuwa hoja ya Katiba haikuwa ya CCM. Kwamba CCM ilikubali kwa kuwa Serikali huongozwa kwa maoni ya wananchi.


  Na Afrika safari ndefu huamuliwa na hatua ya mguu wa kwanza. Ukiianza safari na ’ mguu mbaya’, basi , hiyo haitakuwa safari njema. Ina maana moja kubwa, namna ulivyojipanga na safari yako kuanzia mwanzo. Nilivyofuatilia Kongamano lile la Katiba pale Chuo Kikuu Mlimani, nasikitika kusema, hata wakati ule, tuliianza safari yetu na mguu mbaya.

  Tafsiri yangu juu ya alichokitamka Bagenda ni hii; Katiba ni suala la ’ Sisi na Wao’. Ni mapambano. Hapa kuna tatizo kubwa. Maana, kuna hali ya kutafuta mshindi na mshindwa. Ndio, unatafutwa ushindi na ufahari, le prestige, kama wasemavyo Wafaransa. Ninachokiona, kama tutachagua njia ya kushindana katika kuifanyia marekebisho katiba yetu, basi, hakutakuwa na mshindi. Sote tutashindwa.

  Na hilo ni Neno La Leo.

  Maggid

  Iringa,
  Jumamosi, Novemba 12, 2011
  MJENGWA - Picha, Habari & Matangazo
   
 2. nyabibuye

  nyabibuye Member

  #2
  Nov 12, 2011
  Joined: Oct 28, 2011
  Messages: 85
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  tunakushukuru kwa neno hilo, lakini pia nao wasidhani kilakitu nilazima tukidai tena kwa kupambana wakati kwenye hiyo social contract kila pande inafahamu wajibu wakufanya, wakitaka tushindane tutashindana na tunaamini tutafanikiwa katika mashindano hayo!!!!!!!!!!!!!!!
   
 3. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #3
  Nov 12, 2011
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Katiba ya sasa ni chaka la kuwalinda walioiharibu nchi hii toka uhuru. As long their cronies are still in power, don't expect anything of substance to come out of this biased process. Kupata katiba mpya infront of Kikwete (with his cronies), Mkapa(with his cronies), Mwinyi(with his cronies), Kingunge(with his cronies), Malecela(with his cronies) et al, as members of CCM CC will be a day dream.

  As long as today is the same as yesterday CCM will resist any proper procedure to give Tanzanians their true freedom, freedom of chosing who they want to be their leaders. CCM takes the process as one of the sensitive issue (Issue tete) for their perpetuity to the power, and for this reason don't expect these type of minds set to come up with anything of substance out of this theatric of 'New costitutional which they are now setting its stage using their parliament'. We better count this is a failure abinitio.

  I urge CCM MPs to use this opportunity for the betterment of our country, reject the bill. CCM Mps should know that this process is not going to help them as CCM Mps to maintain their current posts rather they are going to give more power to the CC to decide who can run where and when as long will be their slave. Look the examples of Shibuda et al.

  Fight for the country not CCM's interests (aka cronies). You will come to regret in 2015 by screwing this opportunity. You as individuals you can run for office in a free Tanzania and win any election without help from electoral commission. People are changing, CCM is losing ground you need to learn this in advance. In a free country if you stand by the people you will be elected no matter which party or no party you will be running for.
   
Loading...