Neno La Leo: Katiba Mpya Na Heri Ya Mkwaju | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Neno La Leo: Katiba Mpya Na Heri Ya Mkwaju

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by maggid, Dec 22, 2010.

 1. m

  maggid Verified User

  #1
  Dec 22, 2010
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Na Maggid Mjengwa
  AFRIKA mvua hainyeshi ghafla, utanguliwa na mawingu . Ndio, hakuna mvua isiyo na dalili. Muhimu ni kusoma alama za nyakati.

  Kwa wenyeji wa Pwani wanaelewa tabia za miti hii; mkwaju na mnazi. Upepo mkali ukivumia uliko mkwaju, basi, mti huo huwa na tabia ya kuinama kwa kufuata nguvu ya upepo. Upepo ukipita, mkwaju husimama tena. Mnazi ni tofauti, hushindana na nguvu ya upepo mkali. Upepo ukiwa mkali sana, mnazi utaanguka, hautasimama tena.

  Kauli ya Waziri Mkuu, Mzengo Pinda juu ya Katiba, japo kwa wakati huu, inaitofautisha Serikali na tabia ya mnazi. Waziri Mkuu Pinda aliongea maneno ya hekima sana. Pinda alikubali kuwa hoja ya Katiba ni hoja ya msingi. Kwamba Serikali yetu ni sikivu, na kuwa yeye, kama Waziri Mkuu, atakwenda kumshauri Rais juu ya jambo hilo. Ningemshangaa sana Pinda kama angekurupuka na kutamka, kuwa Katiba iliyopo itabaki kuwa hiyo hiyo, haitarekebishwa. Pinda angekuwa ameonyesha udhaifu mkubwa katika uwezo wa kusoma alama za nyakati.


  Maana, kwa sasa, upepo wa mabadiliko unavuma, si katika nchi yetu tu, hata nje ya mipaka yetu. Nilipata kuandika, kuwa matokeo ya uchaguzi mkuu uliopita yalituma ujumbe mmoja mkuu kutoka kwa wapiga kura; MABADILIKO, kwamba idadi ya Watanzania wenye kiu ya kutaka uwepo wa mabadiliko inaongezeka kila kukicha. Katika hali ya sasa, hali ya wengi kukata tamaa juu ya hali zao za maisha na hata kuwa na hofu ya mustakabali wa nchi yao, ujio wa Katiba Mpya imekuwa ni tumaini jipya kwa Watanzania.

  Jaji Mstaafu Mark Bomani ameweza kuliweka hili la Katiba kwa namna yake; kuwa Katiba mpya itasaidia kuleta nafuu ya maisha ya Watanzania. Kwamba Katiba Mpya ni muhimu kwa sasa na kuwa kuna woga tu katika kuifanyia mabadiliko Katiba yetu. Na hilo ni Neno La Leo.
  ( Hii ni sehemu ya makala yangu ya Raia Mwema, leo Jumatano)

  Maggid
  Bagamoyo,
  Desemba 22, 2010
  mjengwa
   
 2. spencer

  spencer JF-Expert Member

  #2
  Dec 22, 2010
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 2,792
  Likes Received: 1,337
  Trophy Points: 280
  Kumbuka Pinda ni Kiranja, Mtendaji kwa mawaziri.
  Yeye ni kama Manager anayesimamia mabo yaende.

  Nilipata kusoma aina za mamanager
  1:pRODUCTION MANAGERS
  Wao hukomalia kuimarisha uzalishaji, kampuni ipate faida na hawana mchezo katika kazi.
  Kwa maoni yangu Pinda hafanani na Production Managers ingawa hii Jezi iliyofaa kwake
  2:HUMANITY MANAGER
  Mameneja wa aina hii wao huwa ni Ruksa, wanajali sana matatizo ya watu na kuwasamehe. Naomba rususa nikamsalimie bibi anakupa, ni watu wenye huruma na wanaongozwa na hisia zaidi.
  PINDA ni mtu aina hii, Nchi yetu kwa wakati huu si ya kuhitaji mtu aina hii, Inahtaji kiongozi aggrasive/shupavu na mpambanaji kama POWERTILLER-aka POMBE.
  Mtalii akikataa utamuoan MTOTO wa MKULIMA amekaa kimya,hii isiwe kigezo cha mimi na wewe kukaa kimya.
  Katiba ni LAZIMA SIYO OMBI.
   
Loading...