Neno La Leo: 'Joe' Magufuli, ' Harry' Mwakyembe Na Real Madrid!

maggid

JF-Expert Member
Dec 3, 2006
1,084
1,246
Na Maggid Mjengwa,

REAL Madrid ya Hispania ni moja ya timu tajiri sana duniani. Mara nyingi, usajili wa wachezaji wa klabu hiyo huwa ni wa kufuru. Real Madrid ni mkusanyiko wa wachezaji nyota. Na hakika, kocha makini anaelewa, kuwa hakuna jambo gumu kama kufundisha timu yenye mchanganyiko wa wachezaji nyota, tena nyota wa dunia.

Kila mmoja nyota, na uwanjani hivyo hivyo. Kila mmoja anataka kuonyesha umahiri wake. Kazi na mafanikio uwanjani ni ya mmoja mmoja, si kazi ya timu. Ndio maana, Real Madrid, pamoja na kuundwa na nyota wengi wa dunia, bado huwa na kibarua kigumu sana kunyakua ubingwa wa Hispania. Juzi tu, wamenyeshewa mvua Barcelona, 5-0!

Baraza limeshaapishwa. ’Joe’ Magufuli na ’ Harry’ Mwakyembe wameanza mchezo kwa kasi ya kutisha. Kabla ya kusanyiko la Jumatatu la Baraza zima la Mawaziri , wao Jumapili walishaingia Ukumbi wa Karimjee. Mbele ya kamera za wanahabari ’wamemwaga cheche’. Yale yale, kuna tulioanza kuchoshwa na mbinu zile zile wakati mazingira ya mchezo yamebadilika. Ndio maana hatupati ushindi. Mitaani kuna hata wanaokejeli; ”Usanii mtupu!”

Tumemwona John Magufuli akiongea kwa ukali pale ukumbi wa Karimjee. Anasema ndani ya mwezi mmoja hakuna foleni ya magari Dar es Salaam! Hapa Iringa ninakoishi jamaa mmoja aliuliza; ”Hayo magari ya Dar yatakwenda wapi ? Niliiona mantiki katika swali lake hilo. Magufuli akaahidi pia kujenga njia za kupita juu kwa juu. Daraja la Kigamboni, kama NSSF wameshindwa. Tulidhani angeongea na NSSF kwanza kujua wamefikia wapi.Magufuli akasema pia kuwa kunaweza kukawapo na ’ ferry’ ya kupeleka abiria mpaka Tegeta ili kupunguza foleni za barabarani. Ndio hapa tunachoshwa na wanasiasa. Hilo la ’ Ferry ’ ya kwenda Tegeta haliwezi kuwa ’ Ferry’ kwa maana ya Kivuko bali ni usafiri wa meli kwenda Tegeta. Ni suala jingine kabisa, maana, meli hiyo itahitaji kuingia bahari kuu na pale Tegeta kujengwe bandari ndogo ya meli kutia nanga.
Ndio, Magufuli kaongea mengi na kapambwa kweli kwenye vyombo vya habari. Kuna tunaotilia mashaka staili hii ya uongozi. Tuna sababu za msingi. Inatukumbusha hata pale Waziri Magufuli alipotumia maneno mengi kutetea kuuzwa kwa nyumba za Serikali. Ni zoezi alilolisimamia Magufuli mwenyewe katika Utawala wa Awamu ya Tatu wa Rais Mkapa.
Uuzwaji wa nyumba za Serikali kwa maana ya Nyumba za Wananchi, ni moja ya vitendo vya ufisadi mkubwa uliofanyika katika Utawala wa Awamu ya Tatu. Waziri Magufuli aliyesimamia zoezi hilo na ambaye pia ni mmoja wa waliofaidika nalo, ana lazima, kwa namna yake, kuwaomba radhi Watanzania kwa dhuluma ile waliyotendewa ambayo kamwe hawataisahau.
Naam. Na kama mawaziri katika Serikali ya Kikwete watacheza kwa staili ya ’ Kila mtu na kipaji chake’ , basi, nahofia, kuwa wenyewe kwa wenyewe watakwamishana uwanjani. Watanyimana hata pasi. Rais Jakaya Kikwete hahitaji Real Madrid, itamnyima ushindi. Na hilo ni Neno La Leo.

( Hii ni sehemu ya makala yangu ya Raia Mwema iliyochapwa jana Jumatano)Maggid

Iringa
Desemba 2, 2010

http://mjengwa.blogspot.com
 
Mipango katika maisha inahusisha kufanikiwa na kushindwa. Kama tungekuwa tunahofia kushinwa wakati wa kupanga mikakati ya maendeleo basi kusingekuwapo na mipango.

Hatua anazochukua magufuli ni vema zikaungwa mkono angalau kwa kuanzia. sina hakika sana labda mwandishi wa makala hii anafurahishwa sana na mawaziri wakimya kuliko wale aina ya magufuli.
 
So do you mean ni nguvu ya SODA kwa kifupi Magufuli sio mgeni apo so utashangaa nguvu ya soda inayodumu up to infinite
 
Article yako naona ingefaa zaidi kwenye gazeti la RAI kuliko kwenye RAI MWEMA
Na Maggid Mjengwa,

REAL Madrid ya Hispania ni moja ya timu tajiri sana duniani. Mara nyingi, usajili wa wachezaji wa klabu hiyo huwa ni wa kufuru. Real Madrid ni mkusanyiko wa wachezaji nyota. Na hakika, kocha makini anaelewa, kuwa hakuna jambo gumu kama kufundisha timu yenye mchanganyiko wa wachezaji nyota, tena nyota wa dunia.

Kila mmoja nyota, na uwanjani hivyo hivyo. Kila mmoja anataka kuonyesha umahiri wake. Kazi na mafanikio uwanjani ni ya mmoja mmoja, si kazi ya timu. Ndio maana, Real Madrid, pamoja na kuundwa na nyota wengi wa dunia, bado huwa na kibarua kigumu sana kunyakua ubingwa wa Hispania. Juzi tu, wamenyeshewa mvua Barcelona, 5-0!

Baraza limeshaapishwa. ’Joe’ Magufuli na ’ Harry’ Mwakyembe wameanza mchezo kwa kasi ya kutisha. Kabla ya kusanyiko la Jumatatu la Baraza zima la Mawaziri , wao Jumapili walishaingia Ukumbi wa Karimjee. Mbele ya kamera za wanahabari ’wamemwaga cheche’. Yale yale, kuna tulioanza kuchoshwa na mbinu zile zile wakati mazingira ya mchezo yamebadilika. Ndio maana hatupati ushindi. Mitaani kuna hata wanaokejeli; ”Usanii mtupu!”

Tumemwona John Magufuli akiongea kwa ukali pale ukumbi wa Karimjee. Anasema ndani ya mwezi mmoja hakuna foleni ya magari Dar es Salaam! Hapa Iringa ninakoishi jamaa mmoja aliuliza; ”Hayo magari ya Dar yatakwenda wapi ? Niliiona mantiki katika swali lake hilo. Magufuli akaahidi pia kujenga njia za kupita juu kwa juu. Daraja la Kigamboni, kama NSSF wameshindwa. Tulidhani angeongea na NSSF kwanza kujua wamefikia wapi.Magufuli akasema pia kuwa kunaweza kukawapo na ’ ferry’ ya kupeleka abiria mpaka Tegeta ili kupunguza foleni za barabarani. Ndio hapa tunachoshwa na wanasiasa. Hilo la ’ Ferry ’ ya kwenda Tegeta haliwezi kuwa ’ Ferry’ kwa maana ya Kivuko bali ni usafiri wa meli kwenda Tegeta. Ni suala jingine kabisa, maana, meli hiyo itahitaji kuingia bahari kuu na pale Tegeta kujengwe bandari ndogo ya meli kutia nanga.
Ndio, Magufuli kaongea mengi na kapambwa kweli kwenye vyombo vya habari. Kuna tunaotilia mashaka staili hii ya uongozi. Tuna sababu za msingi. Inatukumbusha hata pale Waziri Magufuli alipotumia maneno mengi kutetea kuuzwa kwa nyumba za Serikali. Ni zoezi alilolisimamia Magufuli mwenyewe katika Utawala wa Awamu ya Tatu wa Rais Mkapa.
Uuzwaji wa nyumba za Serikali kwa maana ya Nyumba za Wananchi, ni moja ya vitendo vya ufisadi mkubwa uliofanyika katika Utawala wa Awamu ya Tatu. Waziri Magufuli aliyesimamia zoezi hilo na ambaye pia ni mmoja wa waliofaidika nalo, ana lazima, kwa namna yake, kuwaomba radhi Watanzania kwa dhuluma ile waliyotendewa ambayo kamwe hawataisahau.
Naam. Na kama mawaziri katika Serikali ya Kikwete watacheza kwa staili ya ’ Kila mtu na kipaji chake’ , basi, nahofia, kuwa wenyewe kwa wenyewe watakwamishana uwanjani. Watanyimana hata pasi. Rais Jakaya Kikwete hahitaji Real Madrid, itamnyima ushindi. Na hilo ni Neno La Leo.

( Hii ni sehemu ya makala yangu ya Raia Mwema iliyochapwa jana Jumatano)Maggid

Iringa
Desemba 2, 2010

http://mjengwa.blogspot.com
 
So do you mean ni nguvu ya SODA kwa kifupi Magufuli sio mgeni apo so utashangaa nguvu ya soda inayodumu up to infinite

Njowepo me nashindwa kukataa kukuamini kuwa ni nguvu za Soda. Hebu mwenye kumbukumbu vizuri atujuze, kati ya MBWEMBWE za mawaziri wateule wa mwaka huu 2010 na wale wa 2005 ni zipi zinvunja rekodi ya nyingine???? Me nadhani sio tu nguvu ya soda, ni mbwembwe tu hizi nyingine
 
Natusubiri tuone, ila haikuwa busara kwa Pombe kukimbilia Karimjee, Baraza la mawaziri lilikuwa halijakaa na kuweka mikakati ya pamoja katika utekelezaji wa majukumu tayari yeye kaisha anza mikakati yake binafsi, nadhani hata hakuwa amekuta na bosi wake JK na kupewa JD, lakini cha ajabu kaanza kutengeneza JD yake
 
Maggid ninapenda jinsi unavyoanalyse vitu. (btw, i used to love reading mraba wa maggid..gud old dayz!) Ila kwa hili la kulinganiisha baraza letu na real madrid...naomba uturudishie change!
Baraza liko comprised na underqualified individuals...huwezi walingalisha na cristiano! wamefanya blunders kubwa before na sioni credibility inayowafanya warudi kwenye baraza la mawaziri!
Na kumlinganisha raisi wetu na Mourinho!?? hapo nakataa kabisa...
Duh, nishushie hapo hapo..na change nirudishie!
Shukrani...
 
Maggid,

Buzzwords here are team work and hollistic approach. Kila mtu akija na solutions zake bila kuangalia system nzima ina matatizo gani hawatafanikiwa.

Inatakiwa baraza likae na kuamua vipaumbele vichache na kuvifanyia kazi kwa nguvu zote. kwa mfano matatizo ya usafiri Dar Es salaam yanaunganisha mambo mengi kwa pamoja. Iweje watu wote asubuhi wawe wanaenda sehemu moja na jioni kugeuza? Kwani kuna umuhimu gani ofisi zote kuwa mjini? Mbona Tanesco wako Ubungo na hakuna lililo haribika? Kwanini ofisi mbalimbali za serikali zisihamishiwe pembeni mwa miji ili kupunguza msongamano mjini? Nk.

Utakuta hapo kwamba jawabu ni idara na wizara mbalimbali kujadiliana pamoja kabla ya kuanza implemtations. Ukitumia reli basi wizara ya uchukuzi kama sikosei inahusika wakati ukitumia barabara ni Magufuli na wizara yake.

Mfano wako wa Real Madrid naona una fit vizuri sana maana inawezekana tuna wachezaji wazuri lakini hawawezi kukaa pamoja na kuja na mipango ya maana ambayo wote wanaielewa na utekelezaji ukianza hakuna kuyumba tena.

Prof. Tibaijuka hawezi kufanikiwa bila kushirikiana na kwa mfano wizara ya sheria na katiba. Lakini kukiwa na kitu kimoja na kutengeneza sheria za kupambana na wavamizi wa viwanja basi kuna nafasi kubwa ya kufanikiwa.

Kinachotakiwa ni team work na integrated approach ili kuwa na ufanisi mkubwa.

All in all ninawatakia mafanikio mema ili nguvu isiwe ya soda na yasiishie kwenye maneno bali vitendo na maamuzi yafuate sheria ili isile kwetu tukishitakiwa mahakamani.
 
Na Maggid Mjengwa,

REAL Madrid ya Hispania ni moja ya timu tajiri sana duniani. Mara nyingi, usajili wa wachezaji wa klabu hiyo huwa ni wa kufuru. Real Madrid ni mkusanyiko wa wachezaji nyota. Na hakika, kocha makini anaelewa, kuwa hakuna jambo gumu kama kufundisha timu yenye mchanganyiko wa wachezaji nyota, tena nyota wa dunia.

Kila mmoja nyota, na uwanjani hivyo hivyo. Kila mmoja anataka kuonyesha umahiri wake. Kazi na mafanikio uwanjani ni ya mmoja mmoja, si kazi ya timu. Ndio maana, Real Madrid, pamoja na kuundwa na nyota wengi wa dunia, bado huwa na kibarua kigumu sana kunyakua ubingwa wa Hispania. Juzi tu, wamenyeshewa mvua Barcelona, 5-0!

Baraza limeshaapishwa. 'Joe' Magufuli na ' Harry' Mwakyembe wameanza mchezo kwa kasi ya kutisha. Kabla ya kusanyiko la Jumatatu la Baraza zima la Mawaziri , wao Jumapili walishaingia Ukumbi wa Karimjee. Mbele ya kamera za wanahabari 'wamemwaga cheche'. Yale yale, kuna tulioanza kuchoshwa na mbinu zile zile wakati mazingira ya mchezo yamebadilika. Ndio maana hatupati ushindi. Mitaani kuna hata wanaokejeli; "Usanii mtupu!"

Tumemwona John Magufuli akiongea kwa ukali pale ukumbi wa Karimjee. Anasema ndani ya mwezi mmoja hakuna foleni ya magari Dar es Salaam! Hapa Iringa ninakoishi jamaa mmoja aliuliza; "Hayo magari ya Dar yatakwenda wapi ? Niliiona mantiki katika swali lake hilo. Magufuli akaahidi pia kujenga njia za kupita juu kwa juu. Daraja la Kigamboni, kama NSSF wameshindwa. Tulidhani angeongea na NSSF kwanza kujua wamefikia wapi.Magufuli akasema pia kuwa kunaweza kukawapo na ' ferry' ya kupeleka abiria mpaka Tegeta ili kupunguza foleni za barabarani. Ndio hapa tunachoshwa na wanasiasa. Hilo la ' Ferry ' ya kwenda Tegeta haliwezi kuwa ' Ferry' kwa maana ya Kivuko bali ni usafiri wa meli kwenda Tegeta. Ni suala jingine kabisa, maana, meli hiyo itahitaji kuingia bahari kuu na pale Tegeta kujengwe bandari ndogo ya meli kutia nanga.
Ndio, Magufuli kaongea mengi na kapambwa kweli kwenye vyombo vya habari. Kuna tunaotilia mashaka staili hii ya uongozi. Tuna sababu za msingi. Inatukumbusha hata pale Waziri Magufuli alipotumia maneno mengi kutetea kuuzwa kwa nyumba za Serikali. Ni zoezi alilolisimamia Magufuli mwenyewe katika Utawala wa Awamu ya Tatu wa Rais Mkapa.
Uuzwaji wa nyumba za Serikali kwa maana ya Nyumba za Wananchi, ni moja ya vitendo vya ufisadi mkubwa uliofanyika katika Utawala wa Awamu ya Tatu. Waziri Magufuli aliyesimamia zoezi hilo na ambaye pia ni mmoja wa waliofaidika nalo, ana lazima, kwa namna yake, kuwaomba radhi Watanzania kwa dhuluma ile waliyotendewa ambayo kamwe hawataisahau.
Naam. Na kama mawaziri katika Serikali ya Kikwete watacheza kwa staili ya ' Kila mtu na kipaji chake' , basi, nahofia, kuwa wenyewe kwa wenyewe watakwamishana uwanjani. Watanyimana hata pasi. Rais Jakaya Kikwete hahitaji Real Madrid, itamnyima ushindi. Na hilo ni Neno La Leo.

( Hii ni sehemu ya makala yangu ya Raia Mwema iliyochapwa jana Jumatano)Maggid

Iringa
Desemba 2, 2010

http://mjengwa.blogspot.com

Hii ni siasa, mambo hupangwa vizuri kabla hata mchezo kuchezwa, Magufuli alijua kabisa anrudi ktk wizara yake tangu alipoingia ktk kampeni za ubunge ni kitu alichokuwa anajua wazi.... kila kitu kilishapangwa kujua kwa nini anarudi, hebu soma alama za nyakati na matendo ya wanasiasa wetu utatambua haya................ pili ilikuwa ni kuokoa jahazi ili serekali isiingie ktk madeni yasiyo na msingi.......... fikiria kuwatimua kazi bila sababu za msingi Regional Managers wote 25 na kutangaza vacant posts mpya watu hawa walikuwa na madai yao ya msingi ....... je hili naloni la kusubiri baraza la mawaziri, magufuli anarekodi nzuri ktk wizara hiyo mapungufu yake yasikufanye umchafulie.................. tusubiri tuone tumhukum 2015 au kabla ya hapo kama ataboronga
 
Mwanzilishi wa thread hii nilidhani ni mchambuzi kumbe hakuna kitu. Huyo ni John Magufuli PhD ni namba ya utekelezaji hata wasiomjua wanamkubali sasa sijui umetumwa kuandika upupu gani ili iwe nini. He is creative kwani hayo hayawezekani? wewe umejuaje? Kuna waziri katk wizara hiyo aliyewahi kuyaongea hayo?
 
Tusubiri tuone watakacho deliver kwa watanzania, ninachojua watanzania wengi wanampeda magufuli kwasababu ya uwezo wake mkubwa wa kukariri figures, matukio na agenda za mipango wakati akiwa anajibu maswali bungeni. Pamoja uwezo wake wote, atueleze kwanza kuhusu ule UFISADI mkubwa kabisa wa kuuza nyumba za uma yeye akiwa msimamizi mkuu!

Otherwise, mambo yatakuwa yaleyale tu. Mjengwa mara nyingi sana huwa nina mawazo tofauti na wewe, lakini kwa hili, nakuunga mkono.
 
Maggid sielewi siku hizi umekuwaje, makala zako zinaonekana kama mtu aliyekula za sisiem akabadirika rangi! Unachanganya sana mambo. Mf. unaposema "Real Madrid ni mkusanyiko wa wachezaji NYOTA.." ukalinganisha na Baraza la JK lenye NYOTA wasizidi WATANO napata shida kuelewa lengo lako ni nini? Uwezo wa Magufuli kiutendaji huwezi ukaulinganisha na uwezo wa Kawambwa, Nchimbi, Kabaka, Sofia, Vuai, Mahanga, Chiza, Nagu, Membe, Mkuchika, Mwinyi, Mwandosya, Ngeleja nk nk.

Sisi wananchi mbali na kutegemea utendaji wa kasi na wenye ufanisi toka kwa Magufuli, tuna waangalia wengine kama Tibaijuka, Mwakyembe na Sita, kwa wengine ni utendaji ule ule wa kisanii kwani hawatakuwa na mbinu mpya za utendaji wataendelea kufurahia cheo na kujitengenezea ulaji wao na wategemezi wao.

Hivyo siyo sahihi kulinganisha timu yenye wachezaji wote nyota na ile yenye wachezaji wawili au watatu wakutegemewa. Magufuli kama ulimuangalia vizuri usoni alikuwa AKIMAANISHA kuwa safari hii kama noma na iwe noma yeye yuko kikazi zaidi ndo maana kamng'oa Mrema aliyeshindikana kung'oka TANROAD kwa miaka mingi.

Kwa mtazamo wangu JK angempatia Mwakyembe wizara kamili hasa ya Nisahati na Madini au Sheria na Katiba siyo kumpambanisha na Pombe! Na imani na Magufuli kuwa KABLA ya MIAKA MITANO NCHI itaweza kupitika MKOA hadi MKOA mwaka mzima. Katika serikali ya sisiem mfumo wa utendaji ni mbovu hivyo INATEGEMEA JUHUDI BINAFSI ZA WAZIRI!

Kwa kifupi tunaweza sema Magufuli ni mtendaji mzuri katika Chama kibovu! Naimani Mwakyembe atajitahidi kwendana na kasi ya Pombe ili atendeneze CV ili baadaye akabidhiwe wizara kamili maana mabadiliko ya baraza la mawaziri yanaweza tokea ndani ya miaka hii mitano. Maggid jtahidi kuwa una linganisha vitu kwa usahihi ili watu wajue uko makini na unacho kiandika.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom