Neno La Leo: Hizi Ni Zama Za Mabadiliko | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Neno La Leo: Hizi Ni Zama Za Mabadiliko

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by maggid, Feb 12, 2011.

 1. m

  maggid Verified User

  #1
  Feb 12, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Ndugu Zangu,

  Viongozi Afrika wanapaswa kutambua sasa, kuwa Mwafrika wa mwaka 1975 si Mwafrika wa mwaka 2011. Waafrika wameamka. Viongozi Afrika wana lazima ya kuendana na mabadiliko ya wakati. Hizi ni zama za mabadiliko. Na Mabadiliko ya amani Afrika yanawezekana, mwenye kuyazuia mabadiliko ya amani, atambue, kuwa mabadiliko yenye vurugu hayaepukiki. Hilo la mwisho lina hasara kubwa. Mungu Ibariki Afrika.

  Maggid
  Iringa,
  Jumamosi, Februari 12, 2011
  mjengwa
   
 2. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #2
  Feb 12, 2011
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,314
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Asante Maggid! Mwenye masikio atasikia maana tuna kawaida ya kujifariji kuwa yale ya kule mbali hayawezi kutokea kwenye mji wangu. Tunasahau kuwa wahenga walitufunza mwenzako akinyolewa wewe tia maji...yakija kutokea majuto huwa mjukuu. Ni kweli kabisa mambo yalivyo leo, hatuna budi kufanya mabadiliko ya hiari bila kusubiri yatakayokuja kwa nguvu za umma.
   
 3. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #3
  Feb 12, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,914
  Likes Received: 214
  Trophy Points: 160
  Ujumbe mzuri Mjengwa, ila hueleweki Braza...
  Mara utetee mabadiliko, mara uwe mstari wa mbele kuyapinga....
  Nadhani kwa mwandishi/mchambuzi kama wewe hupaswi kuegemea upande wowote...
  Pale unapotoa uchambuzi kwa kuegemea upande mmoja basi unakuwa ni mshabiki siyo mchambuzi tena...
  Rejea hoja yako dhidi ya CHADEMA kutoka nje ya Ukumbi wa Bunge kupinga kulazimishwa kuungana na wapinzani wengine...
   
 4. a

  alles JF-Expert Member

  #4
  Feb 12, 2011
  Joined: Oct 14, 2006
  Messages: 356
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Anajitahidi kutuhabarisha, lakini shida ni kwamba hana msimamo. Mwandishi mzuri ni yule mwenye msimamo. Ukishaona mwandishi anaandika,na anasahau jana alisimamia nini hujue hapo kuna tatizo. Inawezekana hajui mabadiliko yanaanzia wapi. Mabadiliko yanaanza taratibu kwa kuondoa hofu. Chadema waliiweka kando hofu kwa kukataa kuburuzwa bungeni kwa kutoka nje ukichukulia kwamba wana wabunge wachache ukilinganisha na CCM.Iyo ni njia sahihi ya kupeleka ujumbe kwamba hatuburuzwi. Kwake Mjengwa huu ni huuni(Rejea hoja yako dhidi ya Chadema).Wamisri waliondoa hofu na kukataa amri ya serikali ya kurudi makwao na kupiga kambi Tahir square, kwake haya ndio mabadiliko. Hajui kwamba wote(Chadema na wamisri) wapo kwenye nia moja ya kudai mabadiliko. Jifunze zaidi kutoka kutoka kwa waandishi kama Johnson Mbwambo na wengineo kuwa na msimamo kimaandishi.
   
 5. m

  maggid Verified User

  #5
  Feb 12, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  TANMO,

  Ahsante sana. Sishangai kuwa sieleweki kwa wengine. Jamii yetu haina mazoea ya watu kama mimi. Lakini najua, kuna wanaonielewa. Natumai iko siku utanielewa.

  Maana, kuna wanaofikiri, kuwa Maggid Mjengwa ni CCM. Kuna wanaofikiri kuwa mimi ni CHADEMA, kuna wanaofikiri kuwa mimi ni CUF, kuna wanaofikiri kuwa mimi ni Muislamu. Kuna wanaofikiri kuwa mimi ni Mkristo. Wote hao wanabahatisha.

  Sijapata kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa. Ningependa nikumbukwe, kuwa Maggid Mjengwa alikuwa Mtanzania na Mjamaa aliyejitahidi kufanya yale aliyoamini yana maslahi kwa Tanzania, basi.

  Maggid,
  Iringa,
  Jumapili, Februari, 12, 2011
  http://mjengwa.blogspot.com
   
 6. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #6
  Feb 12, 2011
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Asante Mjengwa bora uwatahadharishe ccm!!!
   
 7. kilemi

  kilemi JF-Expert Member

  #7
  Feb 12, 2011
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 520
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Wapo wanaosema kama sio wao uhuru wa vyama vingi usingekuwepo Tanzania, Tnanategemea pia wasema kama sio wao mabadiliko hayatatokea Tanzania!!
   
 8. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #8
  Feb 12, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,174
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280
  sometimes you speak like a real smart boy
   
 9. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #9
  Feb 12, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,174
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280
  Wengine wanasema Bila CCM Nchi Itayumba
   
 10. N

  Ngonini JF-Expert Member

  #10
  Feb 12, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 2,024
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Bro Magid unataka mabadiliko gani? Mimi najua mabadiliko wanayoyataka wantanzania ni ccm kuiachia hii nchi wajaribu na wengine. Unapokuja na hoja ambazo hazitowi mwelekeo wa hayo mabadiliko basi ni sawa na kwenda mbele hatua mbili halafu unarudi nyuma hatua mbili. Unapowaponda wanaojaribu kudisturb ccm unaturudisha nyuma hatua mbili. Kama wewe ni mmoja wa wanaotaka mabadiliko basi lazima ukubali hata pale wanapolengwa unaowapenda usiumie na kuanza kuwatetea ilimradi wao nimoja wa wanaopinga mabadiliko tunayoyataka.
  Au wewe ndiyo wanaojifariji kuwa mabadiliko si lazima yaletwe na wanaopinga ccm! Kama unafikiri inawezeka kuleta badiliko kwa kupitia ccm hayo ni mabadiliko feki yasiyodumu.
  ccm imesha haribika beyond repair hata kama ukiwahamishia wapinzani wote ccm bado utapata akina mrema,cheyo na wengine kama hao. Je tunaweza kuleta mabadiliko kwa kufanya urafiki na mtu ambaye kwake ni pigo? Nilazima unapo jadiri dhana hii ya mabadiliko hakuna sehemu ya kati, eti mara ccm au chadema,uislamu au ukristo. You have to choose your postion and stand there firmly. Mabadiliko ya sasa hayatatokana na ushawishi wa kisiasa au kikundi cha watu, bali hali halisi inayotukabili. However kunapotokea chama au kikundi kinasikia maumivu kama mwananchi wakawaida anyoumia na kuamua kuunga mkona wanyonge basi hatunabudi kuwapongeza na kuwatia moyo. Waandishi na wachambuzi waoga hawawezi kufika mbali, hakuna kuchoma na kupuliza,kama umeamua kuwa analyst stand on the facts. Tutaweza kushinda na kuleta mabadiliko kama wale wanao thubutu hawatarudi nyuma kwa sababu ya njaa. Moja ya technique ya watawala ni kuwalisha wapinzani wao ili washibe na kusahau ajenda zao.
  Magid chagua msimamo mmoja kama wewe ni mwanamapinduzi, lasivyo unafanya kazi ambayo hautakuja kufikia malengo yako, unless kama kinachokufanyisha hii kazi ni njaa unatafuta wakukushibisha
   
 11. n

  ngoko JF-Expert Member

  #11
  Feb 12, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 574
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Maggid umenena vema , ila nina mashaka makubwa na viongozi wetu kama wanakubaliana na hili ninapojaribu kusoma vichwani mwao naona kama wanaamini KUSINI mwa Jangwa la sahara bado tunahitaji kwenda katika hizo zama za 1975 ..., na kwa mtazamo huo mabadiliko ya amani hayawezekani , tutaendelea kushuhudia uchakachuaji wa matokeo ya chaguzi mbalimbali ili tu ku meet malengo ya watawala lakini .." YANA MWISHO HAYA" , Rais Mubarak alimanipulate uchaguzi akashinda kwa kishindo , leo tunashuhudia mtu yuleyule aliyeshinda kwa kishindo anakataliwa kwa kishindo , nadhani watawala wetu wanapaswa kujifunza kitu hapo .
   
 12. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #12
  Feb 12, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,265
  Trophy Points: 280
  Kwangu mimi mnafki ni mnafki tu, labda utueleze ni lini umejiondoa kwenye payroll ya CCM, sidhani kama napaswa kukuheshimu kama mwandishi huru zaidi ya kukuweka kwenye kundi la waganga njaa na mtaji wenu ni kalamu tu, shame on you.
  Na hapo kwenye RED ndipo watu makini ujulikana kama wako makini kiasi gani, na hapa JF IPO BATANI YA KUEDIT, umeshindwa, sasa nakushauri edit ubongo wako umeshaexpire.
   
 13. m

  maggid Verified User

  #13
  Feb 12, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Matola,
  Asante sana kwa sahihisho kwenye tarehe. Lakini unaonekana pia ni mtu mwenye chuki sana, pole sana.
   
 14. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #14
  Feb 12, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,265
  Trophy Points: 280
  Mkuu mimi sio mtu wa chuki,ninachokichukia hapa duniani kwa sasa ni CCM tu na yeyote yule ambaye ni kibaraka wa CCM, Maggid kwa taarifa yako mimi nilikuwa mmoja wa wapenzi wakubwa wa makala zakomiaka kadhaa nyuma kipindi hicho ulipokuwa mwandishi huru, lakini ninapokusoa leo hii sio kama nimekujuwa hapa JF hapana, kumbuka mimi nilikuwa mpenzi mkubwa sana wa makala zako, na kipindi hicho hata hiyo CHADEMA haikuzaniwa kama itapanda chati kiasi hiki, kwa hiyo nawza kusema nakufahamu ulichokuwa unakiamini na nimeona mabadiliko makubwa upande wako hasa kipindi cha kampeni, jiulize mbona hatumlaumu michuzi? sababu michuzi mimi namtambuiwa kama mpiga picha tu, na NI agent wa CCM, LAKINI WEWE MJENGWAA ni mwandishi, chungeni sana kalamu zenu, swala hapa sio kwamba ukiandike vizuri chama fulanio hapana, swala ni kwamba uwe mwandishi huru na usimamie unachokiamini na usiwe kama kinyonga. mbona heshima Jenerali Ulimwengu haishuki siku zote? unaijuwa siri ya kwa nini Jenerali ataendelea kuheshimika?
  Hitimisho nakuomba radhi kama nilitumia kauli ambazo si kiungwana kwenye post yangu ya kwanza kwenye thread hii. ila msimao wangu uko pale pale ur a not the same Maggid i use to know. ur a trator.
   
 15. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #15
  Feb 12, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kutakuwa na tofauti gani kwani mbona sasa hivi nchi ina CCM na inayumba?
   
 16. mshikachuma

  mshikachuma JF-Expert Member

  #16
  Feb 12, 2011
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 2,853
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Mmmmh.....umeongea vizuri sana kaka Maggid. Lakini siku vijana tukifanya walichofanya Waaegypti na Watunisi
  Je, wewe utaseme na kuandika nini? Utatusaport kimedia au utasema tumetumwa na wanasiasa waroho against ccm?
   
 17. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #17
  Feb 12, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Huu ndio uungwana wa dhati, I lov this.
  Maggid, kindly consider and admit kiuungwana. Pia jitahidi uchambuzi wako usiwe ni wenye mlengo fulani, stand on neutral wise.
   
 18. F

  Fanfa JF-Expert Member

  #18
  Feb 12, 2011
  Joined: Sep 25, 2009
  Messages: 538
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35

  Kwa mara ya kwanza umeongea point. Endelea kuwa na fikira hizo za ukombozi tutafika
   
 19. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #19
  Feb 12, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Uko sawa kabisa Majid, huu ni wakati wa mabadiliko. Inabidi viongozi wa kisiasa wajifunze kwa yaliyotokea Tunisia na Misri.
   
 20. e

  elimukwanza Senior Member

  #20
  Feb 12, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 167
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Maggid acha unafiki kaka,njaa siyo kali kiasi hicho.
   
Loading...